Haji ni mwanasiasa.
Na ni mjuzi wa propaganda.
Miongoni mwa Watu waliopelekea kuharibika kwa mambo mengi ya kisoka ni huyu Mtu.
Miaka ya Nyuma kabla mipira haijawa na hawa maafisa habari na wasemaji mbumbumbu soka letu halikuwa na mauongo ya namna hii.
Baada ya kushindwa kusimamia kazi yake kwa kushindwa kuwaeleza wana Simba mambo yanayoihusu timu yao yeye akabubi mbinu ili aendelee kula tu hapo Simba.
Haji akaamua kuingilia mambo ya Yanga, akaanza kukashifu harakati za Yanga, akaamua kuwaita Yanga kila jina ili mradi tu ateke vichwa vya washabiki oyaoya ili apate sapoti.
Kwa hili alifanikiwa lakini ni kwa wapuuzi tu.
Watu wenye akili siku zote hawazikibali harakati za Haji, kwa maana hazina tija kwa soka la kisasa.
Wana Simba wanatakiwa waelezwe na wajue mifumo ya uchezaji, wajue vyanzo vya mapato, malengo na kujuwa namna gani timu yao inajiandaa kwa ajili ya msimu ujao.
Wana Simba wanatakiwa wajue timu yao imelenga kuwasajili akina nani kwa sasa ili kuweza kuleta ushindani kwenye ligi ya mabingwa msimu ujao.
Pia wanasimba wanapaswa kuelezwa mapato na matumizi ya klabu yao, wanapaswa waelezwe mikataba ilioingiwa na klabu yao na kujuwa mambo ya msingi klabuni hapo.
Lakini yoote hayo bado yanabaki kuwa ni siri na msemaji wa klabu haelezi chochote zaidi ya kuhangaika kwenye mitandao ya kijamii akionesha kumpa milioni moja Mzee Mpili.
Hizi ni mbinu mbovu ambazo Haji amebaki nazo na ndio silaha pekee inayomuweka klabuni hapo kwa maana Simba wengi wao ni mbumbumbu na wanafurahishwa sana na porojo za Haji dhidi ya Yanga.
Amini amini nawaambieni hii ishu ya Babra na Haji ni porojo ya kutengenezwa ili tu iwavuruge Yanga na washindwe kujiandaa na Mchezo wao wa Jumapili.
Lakini kwa Bahati mbaya Yanga wameushtukia na wao wanasonga mbele huku wakijiandaa kikamilifu na mchezo dhidi ya watani wao.
Jiulize kwanini kila siku anaeonewa ni Haji tu?!
Mara Haji vs TFF, mara Haji dhidi ya Katabazi, mara Haji vs Waandishi wa Gazeti fulani, mara Haji dhidi ya Kitenge, mara Haji dhidi ya uongozi wa Yanga, mara Haji dhidi ya Kitenge, mara Haji dhidi ya viongozi wenzie wa Simba, mara Haji dhidi ya Babra...
Yeye ni nani haswa mpaka aonewe kila siku?!
Kwa kifupi Haji kaishiwa na ametoka kwenye uhalisia wa kazi yake na kujikita kwenye mipasho, kebehi, blabla, porojo na propaganda.
Haji haongei ya maana bali kila akitoa habari ni za kejeli dhidi ya Yanga.
Wana Simba wanapaswa kuamka sasa na kuwa imara kujuwa mambo ya maana yanayoihusu timu yao na sio hizi audio za kipuuzi tu.