Ladies & Gentlemen, welcome to Mzizima Derby!!!
Ndio ni Mzizima Derby, Simba Vs Azam Fc wanakutana katika mchezo wa raundi ya pili ya ligi kuu ya NBC.
Ni mchezo wa kukata na shoka, ambapo mtoto hatotumwa dukani.
Huku kuna Ahoua, Ateba na Mpanzu wakati kule kuna Fei toto, Sillah na Akaminko.
Simba wakiwa nafasi ya pili na alama 50 watajaribu kupunguza alama dhidi ya vinara wa ligi Yanga.
Azam wako nafasi ya tatu wakiwa na alama 43 wakitafuta nafasi ya kuwakilisha nchi kimataifa.
Mchezo utapigwa saa 1:00 usiku katika dimba la Benjamin Mkapa na utakuwa mubashara Azam Sports 1HD na TBC Taifa.
Live updates zitakuwepi hapa