Wachezaji wa timu ya Simba wameendelea kukonga nyoyo za mashabiki wake kwa kuendeleza wimbi lake la ushindi wa mfululizo baada ya kuihukumu Prisons ya Mbeya tatu, na kuwaruhusu wahukumiwa hao kupata kamoja tu kwa kukimbia kiwanjani.
Magoli ya Simba yalifungwa na Mussa Hassan 'Mgosi' aliyefunga mabao mawili na Nico Nyagawa aliyefunga moja wakati lile la kufutia machozi la Prisons lilifungwa na mchezaji Misango Magae na hivyo, badi mwisho wa mechi, Simba 3 Prison 1. Timu hizo zilikipiga katika uwanja wa Uhuru. Timu ya Simba SC ilimaliza mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya soka Tanzania kwa kuweka rekodi ya kutokufungwa mechi yoyote. Katika mzunguko wa pili, Simba imegeuza upande wa pili wa wembe na kuendelea kunyoa vipara kila timu wanayokutana nayo.
Ingewezekana, Liverpool FC, ingekopa tuushindi tudogo tokakwa Simba walao tuwasaidie kuepa hili balaa la kichapo wanachosiribwa 'left and right' katika msimu huu wa soka la Uingereza. mwe!
Heko Simba Sports Club!