Kuwatupia Mgosi,Banka na Okwi ni kuiharibu Simba yetu.Mgosi msimu uliopita alikuwa mfungaji bora,msimu huu alianza na majeraha yaliyosababisha ashindwe kuwa kwenye kiwango. Mgosi ni binadamu kama wengine hivyo natumaini akisajiliwa tena atajirekebisha. Banka yuko kwenye kiwango kizuri pamoja na Okwi hivyo nashauri wachezaji hawa wasiachwe.Kukosa ubingwa kwa bao moja isiwe sababu ya kuwaacha wachezaji wazuri.Kwani kama mechi ya mwisho kama tungeshinda na kuchukua ubingwa yote hayo yangesemwa? Lengo isiwe ubingwa tu bali nafasi mbili za juu na kuhakikisha kimataifa tunang'ara.
 
Uwanja Simba kugharimu sh. Bil.75




Kikosi cha Simba



WATAALAMU wa ujenzi wa viwanja vya michezo kutoka nchini Uturuki, wamemaliza tathmini ya ujenzi wa uwanja wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam na wamekadiria utagharimu sh.bilioni 75 za Tanzania .

Akizungumza na waandishi wa habari, mtaalamu wa masuala ya ardhi na ujenzi kutoka kampuni ya Petrolaud, ambayo klabu ya Simba imeipa jukumu la kufanya upembuzi kwa ajili ya ujenzi huo, Mustapha Emre Cakir, alisema ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji walioketi 60,000 na utakuwa na duka kuu, kumbi za muziki na sinema.

Alisema uwanja huo utakuwa wa kisasa zaidi kwani viwanja vingi vya michezo duniani vinatakiwa kuwa na sehemu maalum za kustarehe ili kuhudumia familia na si mambo ya soka pekee, ndiyo maana wanataka uwe na kumbi za sinema na muziki.

"Mradi huu kama ukikamilika utagharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 50 (sh.bilioni 75 kwa hesabu ya dola 1 sawa n ash.1,500), utakuwa uwanja wa kisasa zaidi," alisema.

Alisema kampuni yake ina uwezo wa kujenga uwanja huo kwa miaka mitatu mpaka minne, huku akisisitizia kuwa kampuni yake inauwezo wa kujenga kiwanja bora zaidi na cha kisasa.

Kampuni hiyo yenye makao yake makuu nchini Uturuki ,inamilikiwa na waturuki na ina miaka 20 kwa shughuli hiyo, ambapo kwa mujibu wa mtaalamu huyo aliyeambatana na mwenzake imejenga miradi mikubwa ikiwa pamoja na viwanja vya michezo, majengo ya serikali na miradi mingine tofauti ya ujenzi.

Alieleza kuwa kwa Afrika imejenga miradi 26, huku miradi 20 ikiwa bado inaendelea kujengwa na pia imefanikisha ujenzi wa miradi mbalimbali nchini Marekani

Naye Katibu Mkuu wa Smba, Evodius Mutawala alisema kesho Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo itakaa kupitia taarifa ya ujenzi wa uwanja huo na kukutana na mfadhili wa mradi kisha kulipeleka wazo kujadiliwa kwenye Mkutano Mkuu wa wanachama wa Simba mwezi ujao.

Alisema kuwa uwanja huo ambao wanafikiria ujengwe eneo la Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam unaweza kuwa kitega uchumi kikubwa kwa klabu ya Simba na wanatarajia kuwa wazo la ujenzi wa uwanja huo litakamilika muda si mrefu.

Kwa sasa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam ambao ni wa serikali ndio mkubwa kwa Tanzania ukiwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000 walioketi, ambao uligharimu kiasi cha sh. Bilioni 57 na ulikabidhiwa kwa serikali miaka miwili iliyopita.
 
Sasa ni rasmi kwamba Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri, hatakinoa kikosi cha timu hiyo kwenye msimu ujao na badala yake klabu hiyo imeanza mazungumzo na makocha watatu, akiwamo Jean Marie Ntagwabira kutoka Rwanda, anayesema wamefikia pazuri katika mazungumzo.
Kadhalika, kipa namba moja wa klabu hiyo, Juma Kaseja, ameponea tundu la sindano kutemwa katika kikosi hicho.
Habari za ndani ya klabu hiyo yenye makao makuu mtaa wa Msimbazi, hayo ni sehemu tu ya maamuzi ambayo yalifikiwa na Kamati ya Utendaji ya Klabu iliyokutana Jumatano wiki hii jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake, Ismail Rage.
Ingawa kulikuwa na uvumi wa kutemwa kwa Kaseja, uamuzi huo umeshindikana kwa sababu imekuwa ni vigumu kupata kipa hodari wa kuchukua nafasi yake kwa sasa, licha ya kudaiwa kuwa kiwango chake kimeshuka.
Kocha Ntagwabira anayeinoa timu ya Kiyovu ya Rwanda inayocheza ligi kuu ya Rwanda na ikiwa nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo, akizungumza na NIPASHE jana kutoka Kigali, Rwanda alisema yuko tayari kuinoa Simba na uwezo wa kuipa mafanikio anao ikiwa ni pamoja na kuiwezesha kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho mwakani.
Alisema kuwa tayari amekwisha kutuma wasifu wake (CV) kwa uongozi wa Simba na mahitaji yake anayoyataka na kwa kiasi kikubwa wamekubaliana nao.
Ntagwabira alisema kuwa ana uwezo mkubwa wa kuipa Simba mafanikio kutokana na kuifahamu vyema soka la Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki na Kati baada ya kufundisha klabu ya APR, Atraco zote za Rwanda na timu yao ya taifa, Amavubi. “Kwa sasa mimi (Ntagwabira) nimepata ujuzi zaidi ya nilivyokuwa na APR, waniamini ninaweza, niko tayari kutua Dar es Salaam," alisema kocha huyo.
Aliongeza kuwa kwa sasa hana mkataba wowote na Kiyovu na anafanya kazi kutokana na mapenzi yake ya kuendeleza soka nchini kwao baada ya APR kuajiri kocha wa kigeni.
Amewataka viongozi wa Simba kutohofia kumpa ajira hiyo kwa sababu uwezo wa kuwapatia mafanikio wanayoyahitaji anao.
"Kwanza nitahakikisha Simba inachukua ubingwa wa Kombe la Kagame huko Sudan, nimeshawahi kufanya hivyo na hata kuwafunga Simba nikiwa na APR mwaka 2004, nafahamu ninachotakiwa kukifanya, ninaweza," aliongeza kocha huyo ambaye akiwa na Amavubi walifuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2004.
Mbali na kocha huyo, habari kutoka ndani ya klabu ya Simba zinasema kuwa jina la kocha Mganda, Moses Basena, ndilo lililopitishwa na Kamati ya Utendaji ili kuwa kocha msaidizi huku nafasi ya kocha mkuu bado ikiwa inaendelea kufanyiwa kazi.
Taarifa nyingine zinasema kwamba kikao hicho kiliamua nafasi ya kocha kwa kupiga kura jambo ambalo ni kinyume cha taratibu za kiufundi.
Leo Rage anatarajia kuzungumzia mambo mbalimbali yaliyotolewa maamuzi kwenye kikao hicho cha Kamati ya utendaji kilichofanyika Jumatano jioni.
Hata hivyo mapema mwaka huu, Rage aliwahi kutangaza kwamba klabu hiyo imeingia mkataba wa miaka miwili na kocha Phiri.
Mbali na hatma ya Kaseja kuwa wazi, wakali wengine wa timu hiyo waliokalia kuti kavu ni mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi, Mohammed Banka (kiungo), Salum Kanoni (beki), Juma Jabu (Beki), Salim Gilla (beki).
Taarifa za ndani zinasema kuwa wacheza hao mbali ya kudaiwa kushuka kiwango, pia kuna tetesi kuwa walishiriki kwa njia moja au nyingine kuhujumu timu yao wakati Ligi Kuu Bara ikikimbilia ukingoni, hivyo kuikosesha Simba ubingwa.
Simba inakabiliwa na mashindano ya kimataifa yakiwamo ya Kombe la Kagame yatayoanza Juni mwaka huu jijini Khartoum, Sudan.
Mashindano ya Kagame mwaka huu yanatarajia kuwa na msisimko zaidi hasa kutokana na kuongezeka kwa zawadi kutoka Dola za Marekani 60,000 (Sh. milioni 90) hadi kufikia Dola za Marekani 100,000 (Sh. milioni 150).


CHANZO: NIPASHE
 

Habari kamili ni kwamba Simba wamemchagua kocha wa zamani wa URA ya Uganda ambaye pia alikuwa kocha msaidizi wa Uganda The Cranes, Moses Basema kama kocha wao mpya na atatua Bongo May 1 kusaini probation ya Miez 6 kabla ya kusain mkataba mrefu

Hilo la Kaseja ni maigizo tu
Hatemwi huyo, waliosema atemwe ni hasira tu za kukosa ubingwa
 

Afadhali maana Kaseja kutemwa ingekuwa hatari, kweli msimu kafungwa magoli mengi lakini lakini hata beki line imechangia.
 
Mazembe yatolewaaaaaaaaaaaa walichezesha mchezaji sio watu weweeeeeeeee!!


Simba will play Morocco's Wydad Casablanca, who lost to Mazembe in the third round, for a spot in the group stages of the tournament event.
The one-off game will be played at a neutral venue next week.




BBC Sport - Mazembe to appeal Champions League disqualification SEMA MI NJEMBA ITAFANYA UFISADI IBAKIE..
 
unapo ongelea soka la TZ Simba ndio timu inayojulikana kwa mpira wengine siasa huone jezi ccm kabisa,SIMBA OYEEEEEEEEEEEE
 
Mazembe yamtuliza Samatta yaapa kupambana kiume
Mbwana SamattaMWANDISHI WETU, LUBUMBASHI
RAIS wa TP Mazembe, Moise Katumbi amekaa na wachezaji wake akiwemo Mbwana Samatta wa Tanzania aliyeanza mazoezi wiki hii na kuwatamkia kauli moja; "tulieni kila kitu kiko sawa na mtaendelea kulipwa, lakini viongozi tutapambana mpaka kieleweke."

Katumbi yuko katika wakati mgumu kutuliza munkari wa mashabiki wa timu yake wenye hasira baada ya mabingwa hao watetezi kuondoshwa mashindanoni kwa kumtumia mchezaji Janvier Besala Bokungu wa Esperance ambaye alikuwa hajaidhinishwa.

Katumbi aliyemsajili pia Patrick Ochan wa Simba ambaye tayari yupo Dar es Salaam, aliwaambia mashabiki kwenye mkutano maalum juzi jioni mjini Lubumbashi kwamba TP Mazembe imekodisha wanasheria waliobobea kutoka Uswisi na Ufaransa ili kusimamia rufaa yao kwenye Baraza la Usuluhishi wa Mashauri ya Michezo (CAS) kuhakikisha haki inatendeka.

Katumbi, ambaye pia ni Gavana wa Jimbo la Katanga, alisema kuadhibiwa kwao ni njama za siku nyingi za timu za Afrika Kaskazini na kukumbushia jinsi nahodha wao Tresor Mputu alipofungiwa mwaka jana.

"Mwaka jana walikula njama wakamfungia Mputu na bado tulitwaa kombe na safari hii wametumia mechi ya Simba," alieleza Katumbi, akizungumza na mashabiki wapatao 30,000 kwenye Uwanja wa Kenya mjini hapa.

Katika kikao kingine ambacho kilikuwa maalum kwa wachezaji, alisema: "Hatujapoteza uwanja, kwa hiyo kuweni watulivu kuepusha vurugu. Mtaendelea kupata malipo yaleyale na faida zilezile hakuna tofauti. Nyie ni sehemu ya timu kubwa kwenye bara hili la Afrika."

"Tutaendelea kushiriki michuano ya kitaifa, wekeni miguu yenu uwanjani, endelezeni nidhamu kama mlivyokuwa siku zote ili umoja wetu udumu, sisi kama viongozi tufanya kazi yetu."

Samatta alipoulizwa kuhusiana na maisha mapya ya Mazembe alisema; "Nina imani kwa kushirikiana na wenzangu katika timu basi tutafanya mambo makubwa, nimefurahia mazingira ya hapa. Mimi si mtu wa kuzungumza ni mtu wa vitendo uwanjani."

Samatta anatakiwa na Simba ingawa klabu hiyo inasaka baraka za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ili kumtumia kwenye mechi yao ya mchujo dhidi ya Wydad Casablanca.
 
wazee kuna uwezekano wa kumtumia samata??
 
Basena: Sina haja na Waarabu
Kocha mpya wa Simba, Moses BasenaOLIVER ALBERT NA DORRIS MALIYAGA
KOCHA mpya wa Simba, Moses Basena, amsema hatawapeleleza Wydad Casablanca ya Morocco kabla ya timu hizo mbili kukabiliana Mei 28 jijini Cairo, Misri.

Timu hizo mbili zitakabiliana kwenye mechi ya mchujo ya kuwania kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza na Mwanaspoti kwenye mazoezi ya timu hiyo wiki hii, Basena alisema kwa sasa anachojali ni kuandaa timu yake.

�Sina haja ya kuwajua, kwani ninachoangalia ni nini ambacho Simba inatakiwa kufanya ili kushinda mchezo huo," aliongeza Basena, raia wa Uganda.

Basena alisema dhana ya kupeleleza timu pinzani haina maana kwani kitu muhimu ni kuandaa timu unayofundisha.

"Hivi kweli niwapeleleze Wamorocco halafu kama timu yangu mbovu itakuwaje," aliongeza Basena, ambaye alisema mkazo wake wa sasa ni kuijenga Simba kucheza kitimu.

Basena alisema kwa sasa anataka kuona timu yake inashambulia vizuri na kujihami kwa ushirikiano mzuri.

Alieleza kuridhishwa na kiwango cha wachezaji wake na kuomba hata kiungo Mkenya Hillary Echessa asajiliwe msimu ujao.

Mwanaspoti, hata hivyo, linafahamu kuwa Echessa hana mpango wa kubakia Simba baada ya kutofurahishwa na mwenendo ndani timu hiyo.

Simba iliondoka jana Ijumaa kwenda Zanzibar kuweka kambi kwa ajili ya kujiandaa na mechi hiyo, ambayo imepangiwa baada ya kushinda rufaa dhidi ya TP Mazembe.
 
Kipa mpya Simba awekwa chini ya Ulinzi
Kipa mpya wa Simba, Mkenya Willis OchiengMICHAEL MOMBURI
KIPA mpya wa Simba, Mkenya Willis Ochieng alitua jijini Dar es Salaam juzi Alhamisi usiku na gari yake aina ya Toyota Prado na jana Ijumaa asubuhi akaanza mambo kwenye Uwanja wa Taifa ingawa alikuwa chini ya ulinzi.

Kwa siku ya jana kuanzia katika hoteli aliyofikia ya National iliyoko eneo la Keko, jijini Dar es Salaam mpaka alipokuwa akitembea mitaani uongozi ulikuwa umemuwekea ulinzi mkali wa makomandoo kuhakikisha haguswi wala kuzungumza na yeyote.

Ochieng, ambaye amewahi kucheza Ligi Kuu za Kenya, Afrika Kusini, Sweden na Finland, alikuwa na kikao kizito na viongozi wa Simba jijini Dar es Salaam jana usiku kwa ajili ya usajili wake.

Mchezaji huyo aliiambia Mwanaspoti: "Nimeamkia mazoezini nimepasha pasha kidogo na wachezaji wengine na kuangalia angalia hali ya mambo inavyokwenda."

"Siwezi kuzungumzia mambo mengi mpaka nikae sana na wachezaji lakini kwa haraka haraka nimeona kwamba ni klabu yenye wachezaji wanaoheshimu taaluma na wanajua nini wanachokifanya.

"Wana mwelekeo na ni watu wanaoweza kufanya kazi nzuri, wamenivutia japokuwa ni siku ya kwanza tu kuwaona. Kama nilivyoahidi awali kwamba mambo yangu mimi ni uwanjani zaidi, mimi si mtu wa maneno.

"Nikishamalizana na Simba nitaelekeza nguvu zangu zaidi uwanjani na kutumia kipaji changu kuhakikisha Simba inafanya vizuri, mimi ni mzoefu, Juma Kaseja ni mzoefu na wachezaji wengine wote vilevile kwa hiyo sina wasiwasi. Ninajiamini na naiamini kazi yangu," alisisitiza Ochieng.

Simba imepanga kumsajili kipa huyo lakini endapo itashindikana imepanga kumrudia kipa namba moja wa APR, Jean Claude Ndoli ambaye naye amesisitiza kuwa yuko tayari muda wowote timu ikimuita Dar es Salaam.
 
Wapangaji waishitaki SimbaUONGOZI wa Simba chini ya Mwenyekiti wake, Ismail Aden Rage umepelekwa Mahakama ya Ardhi wilaya ya Ilala na mpangaji wake Haji Abdukarim kwa uamuzi wao wa kutaka kuwaondoa kwa nguvu kwenye jengo la klabu hiyo wapangaji wote.

Kesi hiyo ya wapangaji wa Simba dhidi ya uongozi uliopo madarakani hivi sasa imepangwa kusomwa Mei 25 katika mahakama hiyo, na wapangaji hao wanadai kuwa wana mkataba halali kukaa kwenye jengo la Simba na mikataba waliyonayo siyo batili kama ambavyo viongozi wa sasa wana dai.

Wapangaji hao walipangishwa na uongozi wa Simba uliokuwa chini ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Simba, Kasim Dewji mwanzoni mwa mwaka 2000 kwa mkataba wa miaka 10, na mkataba huo ulimalizika Aprili 31.

Hata hivyo; imedaiwa kuwa kabla ya kumalizika kwa mkataba wa awali wapangaji hao wawili Haji na mwenzake waliingia tena mikataba mipya mwaka 2007 ambayo wameanza kuitumia rasmi Mei Mosi.

Hivi karibuni Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alitangaza kuwaondoa wapangaji hao ndani ya saa 48 kwa hati ya mahakama iwapo hawatatii agizo lao la kuingia mikataba mipya na uongozi uliopo madarakani na kwamba mikataba waliyoingia na uongozi uliopita chini ya Hassan Dalali ni batili.

Rage alitangaza kuwaondoa wapangaji hao wakati akinadi bajeti ya Simba kwa mwaka ujao kuwa ni shilingi bilioni 1.5 ambazo watazitumia kwenye shughuli za uendeshaji wa klabu huku shilingi milioni 375 zikitumika kwa usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

"Natoa saa 48 wapangaji wenye mikataba batili waje waingie mikataba mipya na uongozi wangu kinyume cha hapo tutawaondoa, hatutaki kuingia mikataba ya ubabaishaji sisi mikataba yetu ni mikataba ya mwaka mmoja mmoja, nataka Simba ijiendeshe yenyewe na sitakubali kuona mali za Simba zinateketea kinyume cha taratibu," alisema Rage hivi karibuni.

Lakini, imekuwa kinyume baada ya wapangaji hao kukimbilia mahakamani na kuufungulia uongozi huo wa Simba mashtaka na kugoma kuondoka ndani ya jengo hilo kwa madai kuwa wao ni wapangaji halali.

Akizungumzia suala hilo, Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala alisema: "Tumeshindwa kuwaondoa kutokana na kesi ambayo ipo mahakamani, wameufungulia uongozi kesi wanadai wana mikataba halali," alisema Mtawala.
 
Kwa maneno maneno, ni vigumu Simba kufuzuFrank Sanga
INAWEZEKANA mashabiki wa Simba wakawa na furaha kwa sababu ya kupata nafasi ya chee ya kucheza na Wydad Casablanca ya Morocco katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeipa nafasi hiyo Simba baada ya kubainika kuwa TP Mazembe walimtumia Janvier Besala Bokungu isivyo halali.

CAF iliridhika kuwa Bokungu hakuhamishwa kihalali kutoka Esperance ya Tunisia na hivyo ikafuta ushindi wa jumla ya mabao 6-3 ambao Mazembe iliupata dhidi ya Simba.

Kwa maana hiyo, Simba itacheza na Wydad Casablanca katika mchezo mmoja kwenye 'uwanja huru' na atakayefuzu atatinga Nane Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Juzi Jumapili, CAF ilipanga makundi na ratiba ya Nane Bora, na iwapo Simba itaifunga Wydad Casablanca itajikuta katika Kundi B katika Nane Bora ya Ligi ya Mabingwa.

Hiyo ina maana kuwa Simba itakuwa ugenini mjini Cairo Julai 15 kucheza na Al Ahly ya Misri, kabla ya kuivaa Esperance na baadaye MC Alger ya Algeria.

Ukiangalia kundi hilo B, katika timu hizo; Al Ahly, Esperance na MC Alger utagundua kuwa Simba ndiyo timu dhaifu kuliko zote hapo.

Lakini hata kabla ya kujadili kuhusu hatua hiyo ya Nane Bora ni vyema Simba wakajua kuwa wana mtihani mgumu kuikabili Wydad Casablanca na ndiyo maana ninawashangaa wanaoshangilia.

Ukiondoa wachezaji wachache ambao walikuwa na kikosi cha Taifa Stars na baadhi waliokuwa na vikosi vya timu za mikoa katika Kombe la Taifa, ni dhahiri kuwa wachezaji wengi wa Simba walikuwa mapumzikoni na wengi hawajafanya mazoezi ya maana tangu kumalizika kwa Ligi Kuu Bara zaidi ya mwezi mmoja uliopita.

Wakati Simba wakikosa mazoezi na mechi za kirafiki, wenzao wa Casablanca bado wapo katika ligi na siku kumi zilizopita walicheza na TP Mazembe, hivyo wapo fiti zaidi kimchezo kwa sasa.

Tatizo jingine kwa Simba ni kuwa wachezaji wake wengi nyota walishutumiwa kuwa waliihujumu na kuifanya ikose ubingwa, hivyo viongozi wakakosa imani na wachezaji hao.

Zaidi ya wachezaji nyota sita wa Simba walioshutumiwa, sidhani kama watacheza kwa kujituma katika mechi hiyo ya Wydad Casablanca.

Viongozi wa Simba badala ya kujisifu kwa mambo madogo waliyoyafanya ni vyema wakawaita wachezaji hawa na kuwaomba radhi kwa kuwadhalilisha, vinginevyo ninapata shaka na mchezo huo.

Lakini tatizo kubwa zaidi ni kuwa Simba imetimua benchi lote la ufundi na sasa wanaye kocha mpya, Moses Basena wa Uganda ambaye hawajui wachezaji wa Simba wala hajui fomesheni waliyokuwa wakiitumia.

Sidhani kama atakuwa na muda wa kuijenga Simba kuweza kupambana na Wydad Casablanca ndani ya wiki moja kabla ya mchezo.

Tatizo jingine ni viongozi wa Simba kuzungumza mpaka kupitiliza kana kwamba ni mara ya kwanza kushika uongozi.

Wanatamba, wanajisifu na baadhi ya viongozi wanajifagilia wao binafsi kuwa ndio wameifanya Simba ishinde rufani hiyo.

Sidhani kama hilo ni ukweli, wanaoweza kukubali hilo ni wanachama wale ambao wamezoea 'Ndio Mzee', lakini rufani ni barua ambayo inaweza kuandikwa na Ofisa Habari tu au Katibu Mkuu kwa hiyo hakuna la ajabu hapo.

Acheni blabla, wekeni mikakati ya kuifunga Wydad ili mtinge Nane Bora katika Kundi B.
 
Nimeperuzi jamvini sioni updates zozote, mechi inakaribia kuanza. Ambaye ana access na mechi atupe matokeo.

UPDATES:

Mpaka half time - Casablanca 0 - 0 Simba

Match imeisha - Casablanca 3 - 0 Simba
 
Kwa nini usianze na Simba; i.e
Simba v/s Wydad Casablanca ?

Sina uhakika ni nani aliyeanza kufuzu, kwani ndo angekuwa mwenyeji, nimetumia kigezo cha venue kuwa Arabuni kuwapa uenyeji Wydad...
Natumai hakijaharibika kitu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…