Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) | Special thread
Kwanza ningependa kumpongeza mwenyekiti wa SSC kwa kuweza kuchaguliwa kuwa mbunge wa kule Tabora , na pili kuna habari njema kwa wana SSC ,habari yenyewe hii hapa:
Klabu ya soka ya simba sport ya jijini dar es salaa inatarajia kujenga uwanja wake binafsi mara baada ya mwenyekiti wa klabu hiyo kukiri kuwa kutumia viwanja ambavyo siyo vyakwao wanatumia gharama nyingi zaidi kiwanja hicho kitakacho ingiza watu 30000 kitajengwa katika eneo la klabu hiyo lilopo bunju nje kidogo ya jiji la dar es salaam ambapo pia utazungukwa na maduka kama kiwanja cha santiago bernnabeu cha real madrdi nchini hispania aidha kalbu hiyo imeshaiteua klabu ya giadas ya uturuki kujenga uwanja huo kwa bei nafuu simba imeshafanya makubaliano na ambayo yaliwakilishwa na geofrey nyange enginear ,francis waya mbunifu na evoudius mtawala mwanasheria ilikusaidia kwa haraka uanzaji kazi wa uwanja huo .
na inasemekana uwanja wenyewe utaisha baada ya miaka miwili.kila la kheri klabu letu
 
Haya ndiyo maendeleo tunayoyataka kwenye timu yetu....safi sana viongozi wa Simba na hongera sana rage

Lakini kafanye kazi uliyotumwa na wana Tabora na siyo kuwatumikia mafisadi....
 
Haya ndiyo maendeleo tunayoyataka kwenye timu yetu....safi sana viongozi wa Simba na hongera sana rage

Lakini kafanye kazi uliyotumwa na wana Tabora na siyo kuwatumikia mafisadi....

hili nalo neno
 
Mnyama( SIMBA) leo anaingia uwanjani kusaka pointi tatu mhimu za mwisho kwenye round hii ya kwanza, pambano hilo linapingwa kwenye uwanja wa majimaji, simba itawakosa Juma kaseja aliyefungiwa na TFF kwa madai alikataa kushikana mkono na mgeni rasimi (Kandoro) kwenye mechi yao na Yanga iliyo pingwa kwenye uwanja wa CCM kirumba wachezaji wengine itakao wakosa ni pamoja na Nicodemas Nyagawa na Uhuru Seleman walio majeruhi......Mungu ibariki Simba tumalize mzunguko huu tukiwa tuna watimulia vumbi watani wetu aka sare sare.....
 
tuko pamoja mkuu updates kama kawaida ................................
 
tuko pamoja mkuu updates kama kawaida ................................
Nilienda kuangali mechi ya Arsenal...
Simba 2 na majimaji 0...Goli la kwanza limefungwa dkk ya 79 na Jerry Santo na goli lapili limefungwa na Emmanual Okwi... tukutane mwakani tena
 
Nilienda kuangali mechi ya Arsenal...
Simba 2 na majimaji 0...Goli la kwanza limefungwa dkk ya 79 na Jerry Santo na goli lapili limefungwa na Emmanual Okwi... tukutane mwakani tena

safiii saaana WEKUNDU WA MSIMBAZI.
 
Nilienda kuangali mechi ya Arsenal...
Simba 2 na majimaji 0...Goli la kwanza limefungwa dkk ya 79 na Jerry Santo na goli lapili limefungwa na Emmanual Okwi... tukutane mwakani tena

:director::coffee:
 
...
Simba 2 na majimaji 0...Goli la kwanza limefungwa dkk ya 79 na Jerry Santo na goli lapili limefungwa na Emmanual Okwi...
TFF wameamua kutuhujumu. Kule kwenye official website yao wameandika Majimaji ilipata goli. Kuna viongozi humu wafuatilie? Nimechukua kipande hiki kutoka HAPA
attachment.php
 
hawa TFF watendaji wao ni watu wa kukurupuka sana, chagueni haraka afisa habari na mtendaji maana mnapoelekea si kuzuri
 
TFF wameamua kutuhujumu. Kule kwenye official website yao wameandika Majimaji ilipata goli. Kuna viongozi humu wafuatilie? Nimechukua kipande hiki kutoka HAPA
attachment.php

unabidi tuwasiliane na viongozi wa simba ...
 
Phiri ajiwekea malengo ya kufika hatua ya makundi Afrika Send to a friend Monday, 08 November 2010 20:58 0diggsdigg

patrick%20phiri.jpg
Kocha wa Timu ya Simba,Patrick Phiri

Andrew Kingamkono, Songea
KOCHA wa Simba, Patrick Phiri amejiwekea lengo mahususi msimu huu la kuhakikisha timu yake inafuzu kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Katika mahojiano maalum na Mwananchi, Phiri alisema Ligi ya Mabingwa Afrika inazikutanisha klabu bora zinazotoka katika ligi bora barani humo, hivyo ni mapema mno kwa sasa kuanza kuwaza ubingwa wa michuano hiyo ambayo itakamilika Jumamosi kwa mchezo baina ya TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), mabingwa watetezi dhidi ya Esperance ya Tunisia jijini Tunis.

"Lengo la kwanza tulilojiwekea kama klabu msimu huu ni kuhakikisha timu yetu inafuzu hatua ya makundi baada ya hapo tutaangalia ni nani tuliopangwa nao ili kuanza kufikiria hatua nyingine inayofuata ."

"Miaka minane imepita tangu Simba ilipofuzu kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo, hivyo hatuna budi kujipanga vizuri na kuhakikisha msimu huu tunafikia lengo hilo," alisema.

"Msimu uliopita tulifikia raundi ya pili, tulishinda mechi zote dhidi ya wapinzani wetu kutoka Zimbabwe, lakini tukafungwa kule Misri na kutolewa, tumeliona hilo tunalifanyia kazi ili lisijirudie tena msimu huu.

"Nashukuru viongozi wangu (Simba SC) msimu huu wako makini na wamepania kurudisha heshima ya klabu kwa kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika."

Mzambia huyo aliongeza kuwa ukiangalia ubora wa ligi zote za Afrika, utakuta Tanzania inashika nafasi ya 23, hivyo ina maana unapotaka ubingwa ni lazima kuhakikisha unashinda dhidi ya timu 22 bora kutoka nchi nyingine.

"Tunahitaji mikakati thabiti na nia ya dhati kwenye jambo hili na kuachana na mawazo ya kutwaa ubingwa wa ndani pekee, wote wachezaji na viongozi tunalazimika kuwaza hili kwanza."

Mabingwa hao wa Tanzania Bara wanategemea kutupa karata yao ya kwanza kwenye michuano hiyo ya Afrika Januari 28, wiki mbili baada ya kufunguliwa kwa pazia la raundi ya pili ya Ligi Kuu huku watani zao, Yanga wao wakicheza michuano ya Kombe la Shirikisho.

Vigogo hao wa soka nchini wameshindwa kutuliza kiu ya Watanzania wengi wenye hamu ya kuona klabu yao ikifika japo fainali ya michuano hiyo mikubwa ya Afrika kama ilivyokuwa mwaka 1993, wakati Simba ilipolala kwa Stella Abidjan ya Ivory Coast kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam baada ya kufanya vizuri ugenini.
 
Hizi threads zipo kimya sana siku hizi! Jamani tupo juu ,jamaa wameamka juzi baada ya manji kukimbia nchi kwa muda kupisha uchaguzi mkuu,wamemjadili kocha na mambo kibao eti hawakubali sisi kuwakandamiza chini,sasa wanataka kuanza ligi kwa vile manji karudi.

Yaani wanatafuta shuka kumekucha!
 
TFF wameamua kutuhujumu. Kule kwenye official website yao wameandika Majimaji ilipata goli. Kuna viongozi humu wafuatilie? Nimechukua kipande hiki kutoka HAPA
attachment.php
Usijali ndugu yangu kule tiftif kuna mgonjwa mmoja wa akili anafanya kazi asiyoijua("Jumapili" Kayuni)
 
Wadau wa Msimbazi,je tunahitaji kuongeza nguvu ktk dirisha dogo la usajili? Kama tunahitaji,ni ktk nafasi ipi?
 
Wadau wa Msimbazi,je tunahitaji kuongeza nguvu ktk dirisha dogo la usajili? Kama tunahitaji,ni ktk nafasi ipi?
Binafisi sijaiona simba msimu huu na imekubwa na majeruhi sana ya kuna wakati tulikuwa na majeruhi zaidi ya watano tena wote first eleven lakini nimeona kocha amependekeza wachezaji wawili na wanaangalia utaratibu wakuona kama wanaweza kumtumia Boban kwa mkopo...
 
Back
Top Bottom