Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) | Special thread
Simba kamili yaifuata Elan Send to a friend Tuesday, 25 January 2011 00:15 0diggsdigg


patrick%20phiri.jpg
kocha Mkuu wa timu ya Simba,Patrick Phiri

Imani Makongoro
KIKOSI cha wachezaji 21 cha klabu ya Simba kitaondoka kesho asubuhi kwenda Comoro tayari kwa mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa ya Afrika dhidi ya timu ya Elan Club de Mitsoudje.
Timu hiyo itaondoka kwa ndege ya Air Comoro kuanzia saa 2:00 asubuhi na maandalizi yake yamekwisha kamilika kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Godfrey Nyange ëKaburuí.

Kaburu alisema kuwa wachezaji wana morali kubwa na wanaamini watafanya vizuri katika mechi hiyo.

Naye kocha Mkuu wa timu hiyo, Patrick Phiri amesema kuwa pamoja na timu kupata matokeo mabaya ya kufungwa 3-2 na Azam FC, lakini wana matumaini makubwa ya kufanya vyema na makosa yaliyofanyika watayafanyika kazi kabla ya mechi yao ya mwishoni mwa wiki.

Phiri alisema kuwa mechi dhidi ya Atletico na Azam FC imewapa picha halisi ya timu yao na hasa upande wa ulizni ambayo imekuwa ikiruhusu mabao kirahisi.

Alisema kuwa tatizo hilo limekuwa likiigharimu sana timu yake na dawa yake imekwisha patikana na kuwataka mashabiki na wanachama wa klabu ya Simba kusahau matokeo mabaya kwa timu yao.

Alifafanua kuwa walifungwa bao rahisi sana na timu ya Atletico ya Brazil, lakini hakuizingatia sana mechi hiyo kutokana na viwango vya wachezaji na mechi ambayo imemtia simanzi kubwa ni dhidi ya Azam FC ambayo mara kadhaa wamekuwa wakiifunga.

ìHakuna tatizo kubwa na tusaiahu yaliyopita, sasa tuaangalia nini kinafuata na nini cha kufanya, tunaamini kuwa mechi yetu dhidi ya Elan itakuwa ngumu, lakini tutashida,î alisema Phiri.

Katika kikosi chake, Phiri amewaacha wachezaji sita kutokana na sababu za ugonjwa na nyingine ikiwemo viwango. Wachezaji walioachwa ni Joseph Owino na Uhuru Seleman ambao ni wagonjwa na wengine ni ambao hawatakuwemo katika safari hiyo ni Aziz Gilla, Kelvin Charles, Salum Kanoni na kipa namba tatu, Ramadhan Kabali.

Wachezaji wanaondoka ni: Makipa; Juma Kaseja, Ali Mustapha.

Mabeki: Haruna Shamte, Amir Maftah, Juma Jabu, Juma Nyosso, Kelvin Yondani, Meshack Abel.

Wachezaji wa kati (viungo): Mohamed Banka, Abdulhalim Humud, Jerry Santo, Rashid Gumbo, Nico Nyagawa, Hilary Echesa, Patrick Ochan na Amri Kiemba.

Washambuliaji ni: Mussa ìMgosiî Hassan, Emmanuel Okwi, Mbwana Samatta, Ahmed Shiboli na Shija Mkina.
Kwa upande wa benchi la ufundi kutakuwa na kocha mkuu, Patrick Phiri, msaidizi wake, Amri Said, timu meneja, Innocent Njovu na daktari, Cosmas Kapinga.

Mkuu wa Msafara huo ni Ibrahim Masoud ëMaestroí ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ufundi ya Simba na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji.

Kwa upande wa Shirikisho la soka la Tanzania (TFF), litawakilishwa na mjumbe wa kamati ya Utendaji, Shaibu Nampunde.
Wajumbe wengine katika msafara huo ni Swedi Mkwabi, Makamu Mwenyekiti, Godfrey ìKaburuî Nyange na mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage
 
jamani wana jamvi mechi ya leo..alen na simba itatangazwa na radio station gani?..maana matokeo ya yeboyebo ninayo..
 
simba mnyama imetoka sare na timuu ya elan ya huko komoro...tumewakosa kosa sana mabeki wao walikuwa makini sana,rajacasablanka imeiadhibu tuabiyon ya chad magoli 10-1
 
Sijui hiyo TP Mazembe itakuaje kama tunatoa Draw na wakomoro
 
Mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam walirejea nchini jana wakitokea Comoro walikopata sare ya 0-0 katika mechi yao ya kwanza ya Ligi ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya wenyeji Elan club de Mitsoudje.
Akizungumza muda mfupi baada ya kutua kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana, kocha Patrick Phiri wa ‘Wekundu wa Msimbazi' alisema kuwa soka la Comoro limebadilika na hivyo wataongeza juhudi katika maandalizi ili washinde katika mechi ya marudiano.
Alisema kuwa makocha wazawa wa Comoro wamenolewa vya kutosha na wakufunzi wa soka kutoka Ufaransa wanaopelekwa kupitia programu za FIFA na hivyo, wapinzani wao ni washindani katika michuano ya ligi ya klabu bingwa na sio wasindikizaji kama ilivyozoeleka katika miaka ya nyuma.
Alisema Wacomoro wamebadilika na klabu ya Mitsoudje inatumia nguvu na hivyo watalazimika kujipanga vyema ili kukabiliana nao katika mechi ya marudiano na hatimaye na kuwang'oa.
Wakati huo huo, beki wa kutumainiwa wa Simba, Joseph Owino anatarajiwa kurejea nchini kesho akitokea kwao Uganda alikokwenda tangu Desemba kumalizia masomo yake ya Utawala na Biashara.
Akizungumza na NIPASHE, Makamu Mwenyekiti wa Simba, Goefrey Nyange ‘Kaburu', alisema kuwa beki huyo alitarajiwa kufanya mtihani wake wa mwisho Jumatatu na jana alitakiwa kuanza safari ya kurejea klabuni kwao.
"Tumemkosa kwa muda mrefu … sasa anarejea na kocha hatakuwa na hofu yoyote kwa sababu kikosi chake kitakuwa kimekamilika," alisema Kaburu.
Aliongeza kuwa kikosi chao kitafanya mazoezi leo kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya African Lyon itakayochezwa keshokutwa Alhamisi kwenye uwanja wa Uhuru.
 
Phiri awaonya nyota Simba






[FONT=ArialMT, sans-serif]Kocha wa mabingwa wa soka nchini, Simba, Patrick Phiri amesema ataendelea kuwaweka benchi wachezaji wake nyota ambao hawataonyesha kiwango, baada ya kumuacha nje ya kikosi kipa chaguo la kwanza Juma Kaseja katika mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Afrika ugenini kwa Comoro kwa klabu ya Elan Mitsoudje.

[FONT=ArialMT, sans-serif]Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu, Phiri alisema kikosi chake kwa sasa kinakabiliwa na mechi za ligi kuu ya Bara na za mashindano ya kimataifa hivyo ili kufanya vizuri ni lazima wachezaji wajitume kwa uwezo wao wote.
View attachment 21851
[FONT=ArialMT, sans-serif]"Tunakabiliwa na mechi za ligi kuu na tayari tumeshapitwa kwenye msimamo wa ligi na pia tuna mechi ngumu na muhimu ya marudiano ya Ligi Klabu Bingwa Afrika, wachezaji wanatakiwa kujituma, sitakuwa tayari kumtumia mchezaji ambaye hatakuwa makini," alisema Phiri.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kaseja, ambaye aliomba msamaha kufuatia makosa yake ya langoni yaliyoigharimu Simba katika mechi yao iliyopita ya Ligi Kuu ya kichapo cha 3-2 kutoka Azam, aliachwa nje ya kikosi kilichotoka sare ya 0-0 dhidi ya Mitsoudje katika mechi yao ya kwanza ya Ligi ya Klabu Bingwa na Mzambia huyo amesisitiza kwamba "hataangalia sura" katika kupanga kikosi chake. Kipa chaguo la pili, Ally Mustafa 'Barthez' alisimama langoni Comoro.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Phiri alisema kuwa mchezo wa marudiano dhidi ya Mitsoudje utakuwa mgumu na hivyo wanapaswa kujiandaa vya kutosha.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Simba walianza mazoezi jana ya kujiandaa na ligi kuu na dhidi ya Wacomoro hao watakaocheza nao kati ya Februari 12 na 13 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.[/FONT]
CHANZO: NIPASHE
[/FONT]
[/FONT]
 
wachezaji wanaoiwakilisha simba: Ally Msitafa, Hurana Shamte, Juma Jabu, Meshack Abel , Kelvin Yondani, Jerry Santo, Rashid Gumbo, Patrick Ochan, Bwana Samatta, Musa Hassan Mgosi na Amri kiemba.

African Lyon: Lucas, Zahri, Zuberi ubwa, Hamis Yusuf, Rashid, Mohamed Samatta, Bakari ommary,Adam Kigwande,Hamis Sabiti
 
Back
Top Bottom