Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) | Special thread
Kuna MAshabiki wanashangilia uku wakiwa na bendera ya CHADEMA
 
mpira unaochenzwa na cmba imebidi watu wasimame majukwaani mpaka raha
 
Mpira umeisha,
simba tunaongoza ligi kwa pointi 33 huku tukiwa na mchezo moja tofauti na yebo yebo wenye pointi 32 na mchezo mmoja zaidi....
Hongera Simba
 
mpira unaochenzwa na cmba imebidi watu wasimame majukwaani mpaka raha
Ila hatujapata mfunguaji mwenye uchu wa magoli kama tunacheza mpira mzuri mfano mechi ya juzi yaani ilikuwa tufunge siyo chini ya goli 6...
 
Shukrani kwa wakazi wa Dodoma kwa kuja kwa wingi na kuwapa wachezaji moyo uku wa2 wanacheza na kushangilia wakimbeba Kaseja juu juuu
 
Mpira umeisha,
simba tunaongoza ligi kwa pointi 33 huku tukiwa na mchezo moja tofauti na yebo yebo wenye pointi 32 na mchezo mmoja zaidi....
Hongera Simba

Safi sana. Rage naye itabidi aanze kupeperusha bendera ya CDM
 
11th February 2011



[FONT=ArialMT, sans-serif]Uongozi wa klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam umesema kuwa mechi ya marudiano kati ya timu yao na Elan de Mitsoudje ya Comoro itachezwa kwenye uwanja wa Uhuru na kiingilio cha chini katika eneo la mzunguko ni Sh. 3,000.[/FONT] [FONT=ArialMT, sans-serif]Wapinzani wao wa Simba, Elan walitarajiwa kuwasili nchini jana jioni baada ya juzi kukwama kwa zaidi ya saa tatu katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hahayam uliopo Moroni baada ya ndege waliyokuwa wakiisubiri kushindwa kuondoka nchini Afrika Kusini ambako ilipeleka abiria wengine.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Akizungumza jana, Afisa Habari wa klabu ya Simba, Clifford Ndimbo, alisema kuwa maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na kilichobaki ni kuwasubiri wapinzani wao wawasili.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Ndimbo alitaja kiingilio cha juu katika uwanja huo maarufu kama 'Shamba la Bibi' Jumapili kuwa ni Sh. 20,000 kwa eneo la viti maalumu, jukwaa kuu ni Sh. 15,000 na jukwaa la kijani ni Sh. 8,000.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema kuwa waamuzi ambao wanaotoka Rwanda pamoja na kamisaa wa mchezo huo utakaofanyika kuanzia saa 10:00 jioni watawasili nchini leo.[/FONT] Simba.jpg
[FONT=ArialMT, sans-serif]Aliongeza kuwa nyota wao nane waliokuwa katika timu ya taifa wameshajiunga na wenzao na habari za faraja kwao ni kurejea mazoezini kwa beki wao, Joseph Owino na viungo Emmanuel Okwi na Rashid Gumbo ambao walikuwa majeruhi.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]"Ila katika mechi ya Jumapili tutamkosa Echesa (Hillary) na nahodha Nyagawa (Nico) ambaye anaumwa malaria na daktari amesema akae nje kwa siku tano," alisema Ndimbo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Aliongeza kuwa kabla ya mechi hiyo ya Klabu Bingwa Afrika haijaanza mchana kutakuwa na mchezo wa utangulizi ambapo Simba B itachuana na wenzao wa Downbrakers.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Naye Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ,'Kaburu', alisema kuwa uongozi umejiandaa vyema kuhakikisha kwamba timu inashinda na kusonga mbele katika mashindano hayo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kaburu alisema kuwa mashabiki wanatakiwa wafike uwanjani kuishangilia timu yao na wasiwe na hofu yoyote kuhusiana na kiwango cha nyota wao.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]"Simba iko sawa sawa, wachezaji wote wanafahamu jukumu walilonalo, tuko nyumbani tutautumia uwanja wetu vizuri, tunataka kusonga mbele," alisema kiongozi huyo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema pia Jumapili uongozi wa Simba unatarajia kutambulisha na kuanza kuuza jezi maalumu za klabu hiyo na akawataka wote waliokuwa wanatumia nembo ya klabu kuacha kuitumia kwani atakayemakatwa atafikitishwa katika vyombo vya sheria.[/FONT]




CHANZO: NIPASHE
 
ushindi hapa ni lazima, na safari hii hakuna kuwadharau hawa jamaa, lazima wachezee kichapo tu.God bless SSC
 
Back
Top Bottom