Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) | Special thread
luchele musa alipata maumivu kidogo ..ameamka tayari .. dk ni ya 53
 
Si haba, ngoja tukajiulize na kujipanga kwa mzunguko wa pili!
 
juzi nilijuwa tumepata Demu la kulipakata, heeh naona jana limefumaniwa huko chamazi kichupi mkononi likakimbia na kuambulia suluhu ya 3-3....dah
 
Simba ni Simba tu. Habari ndiyo hiyo!

Simba bingwa michuano ya vijana

TIMU ya vijana chini ya miaka 20 ya Simba jana ilitwaa ubingwa wa ligi ya timu hizo ‘Uhai Cup' baada ya kuichapa Azam kwa mikwaju ya penati 6-5 katika fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Karume, Ilala. Katika mchezo huo mkali timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana na kulazimu kuongezwa dakika 30 ambazo hata hivyo ziliisha kwa timu hizo kutoka sare tena ndipo sheria ya changamoto ya mikwaju ya penalti ilipochukua nafasi yake.

Simba walifunga penalti zao zote kupitia kwa wachezaji wao Abdallah Selemani, Ramadhani Singano, Jamal Mwambeleko, Edward Christopher, Haruna Athumani na Wiliam Lugani. Wakati penalti za Azam ziliwekwa kimiani na Mgaya Jaffar, Calvin Idd, Ibrahim Juma,Tumaini Venance na Mussa Kanyagha huku mchezaji Yaluku alikosa kwa upande wa Azam na kuipa Simba ubingwa wake wa kwanza tokea mashindano hayo yaanze karibu miaka mitatu iliyopita.

Simba iliingia fainali za mashindano hayo baada ya kuzifunga timu za JKT Oljoro mabao 5-2 katika mchezo wa robo fainali na baadaye kuwafunga Toto Africans ya Mwanza mabao 4-1 katika mchezo wa nusu fainali. Kwa ushindi huo, Simba imepata Sh milioni 1.5 kutoka kwa wadhamini wa michuano hiyo S.S. Bakhesa, na Azam iliyoshika nafasi ya pili imepata Sh milioni moja.
Kocha mkuu wa mabingwa hao, Selemani Matola aliteuliwa kuwa kocha bora wa mashindano hayo ambapo alipata Sh 500,000 huku mshambuliaji hatari wa timu hiyo Ramadhani Singano akipata nafasi ya mchezaji bora na kupata Sh 400,000.
 
[h=2]MILOVAN ASAINI MKATABA WA MIEZI SITA KUIFUNDISHA SIMBA[/h] 29112011245.jpg29112011238.jpg29112011247.jpg
 
Kiboko ya Papic asaini Simba

JACKSON ODOYO
KAMA Yanga walijua kwamba wameiweza Simba kwa kumchukua Kosta Papic sasa Wekundu nao wamejibu mapigo kwa kumsainisha kocha Milovan Cirkovic mkataba wa miezi sita.

Milovan, ambaye alitua nchini juzi Jumapili usiku ameziba nafasi ya kocha wa Uganda, Moses Basena ambaye ametimuliwa kwa kusitishiwa mkataba ingawa jana Jumatatu ametamka kutolitambua hilo.
Kocha huyo, raia wa Serbia anasifika kwa soka la kasi na kushambulia lenye mvuto jambo ambalo huenda akalifanya kiusahihi zaidi kutokana na kuwa na mastraika wakali kama Emmanuel Okwi, Felix Sunzu na Gervais Kago.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Simba, Ibrahim Masoud Maestro alisema kuwa wamemsainisha kocha huyo mkataba wa miezi sita kuangalia uwezo wake.

Tumemsainisha miezi sita kwanza, kama tukivutiwa naye tutamuongeza mkataba mwingine siku zijazo baada ya kumfanyia tathmini ya kina,"alisema Maestro ambaye ana taaluma ya ukocha.

Habari za ndani zinadai kocha huyo atakuwa akilipwa dola 6000(zaidi ya Sh 10 milioni) kwa mwezi na leo Jumanne atatambulishwa kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kutamka neno kwa mashabiki wa Simba.
Akizungumza na Mwanaspoti katika Hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam, kocha huyo alisema amesaini mkataba huo kwa sababu ana imani na uongozi uliopo madarakani.

Alisema kazi yake kubwa kwa sasa ni kuandaa programu kwa ajili ya kuiandaa timu hiyo na kuipa mataji mbalimbali ikiwemo ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Nimerudi tena Simba na tayari nimesaini mkataba mpya na safari hii nikiwa chini ya uongozi mpya wa timu nina imani mambo yatakwenda vizuri. Maana wamenitafuta wenyewe,�alisema Circovic.
Akizungumzia timu hiyo, Cirkovic alisema; �Ninafahamu kuwa Simba ni timu nzuri na ina wachezaji wazuri na tayari nimepewa rekodi yake kuwa wamepoteza mechi moja, wametoka sare tatu, wamefungwa mchezo mmoja na kizuri zaidi wanaongoza ligi�.
Kuhusu aina ya wachezaji wa timu hiyo alisema, ataangalia mwenendo wa timu kwa kushirikiana na benchi la ufundi na akiona kuna ulazima wa kufanya mabadiliko atafanya.

Kama mabadiliko yatakuwa muhimu nitafanya lakini kwa sasa ni mapema sana kusema hilo kwa sababu ndio kwanza nimesaini mkataba na kazi inayofuata ni kuketi na wachezaji,� alifafanua Cirkovic.

Kocha aliyetimuliwa kazi Basena aliiambia Mwanaspoti jana Jumatatu kwa njia ya simu kwamba hatambui hilo. "Mimi sina taarifa yoyote, najua bado nipo kazini kama wakinifukuza inabidi wanilipe fidia kwa mujibu wa mkataba wangu niliosaini. Hata kama watataka kunipa kazi nyingine itabidi kwanza tulipane halafu ndio tuanze majadiliano mengine.

Simba ina pointi 28 ikiongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Bara ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 27, huku michuano hiyo ikitarajiwa kuendelea mwezi Januari mwakani.
 
Special thread ya Simba sc mbona ipo humu siku nyingi tu!! au mnaingia macho juu humu jamvini? wasiliana na Saint Ivuga atakujuza zaidi.
 
nasikia jamaa ni yanga kwa hiyo anamtishia nyau mtakatifu ivuga..:A S 465:
 
Back
Top Bottom