Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) | Special thread
[h=3]Zamoyoni Mogela"Glden Boy"[/h]
31264_390426793663_709948663_3877222_7166750_n.jpg

pichani kulia ni Golden Boy akijaribu kumpita Athumani juma Chama kati ni Muhidini Cheupe akihakikisha mambo hayaendi mrama
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Mkandarasi 'aitapeli' Simba, kushitakiwa [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Saturday, 31 December 2011 08:34 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 0digg

Sosthenes Nyoni
UONGOZI wa Simba umesema unakusudia kumshataki mkandarasi wa jengo la biashara la klabu hiyo (jina linahifadhiwa) kwa madai ya kukiuka makubaliano.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage aliyataja makubaliano yaliyofikiwa baina ya klabu hiyo na mkandarasi huyo kuwa ni ujenzi wa msingi wenye uwezo wa kubeba jengo la ghorofa nane.

Alisema kuwa kinyume na makubaliano hayo klabu yake kwa kuwatumia wataalamu wa kitendo cha uhandisi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walibaini kuwa kuwa jengo hilo ambalo kwa sasa lina ghorofa tatu haliwezi kubeba ghorofa nyingine juu na endapo watalazimisha kunauwezekano wa kudondoka.

"Niseme wazi Simba inakusudia kumshItaki mkandarasi wa ujenzi wa jengo letu la biashara kutokana na kukiuka makubaliano.

"Nyaraka za makubaliano zipo na zinaonyesha alitakiwa ajenge msingi wenye uwezo wa kubeba ghorofa nane, lakini yeye ametudanganya," alisema Rage.

Aliongeza kuwa tayari ameshawasiliana na wanasheria wake kwa ajili ya kufungua kesi dhidi ya mkandarasi huyo.

"Nimeshawasiliana wanasheria wangu nafikiri mpaka kufikia wiki ijayo kesi dhidi ya mkandarasi huyu itakuwa imeshafunguliwa," alisema

Rage alisema kwa sasa wapo mbioni kubomoa jengo hilo na kujenga jingine litakalokuwa na ghorofa nane kwa lengo la kuongeza mapato ya klabu yake.

"Huu si wakati wa kutafuta sifa kwa kuifunga Yanga, Simba na Yanga zinafungana hata mimi sijazaliwa, wajibu wa kiongozi ni kubuni miradi, mambo ya timu kufungwa au kushinda ni suala linalowahusu wachezaji," alisema Rage.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Kuna wakati Chairman wetu anaongea kama binadamu. Uamuzi sahihi sana huo unaochukuliwa na klabu na utadumisha nidhamu kwa mali za klabu na kupunguza utegemezi siku zijazo.
Go Simba go...!
 
Kuna wakati Chairman wetu anaongea kama binadamu. Uamuzi sahihi sana huo unaochukuliwa na klabu na utadumisha nidhamu kwa mali za klabu na kupunguza utegemezi siku zijazo.
Go Simba go...!

kweli hapa jamaa kaongea kama kiongozi
 
Kuna wakati Chairman wetu anaongea kama binadamu. Uamuzi sahihi sana huo unaochukuliwa na klabu na utadumisha nidhamu kwa mali za klabu na kupunguza utegemezi siku zijazo.
Go Simba go...!

kasheshe ni pale anaposhika bastola kama Anodi Shwazniga.
 
Hebu tujulishane yaliyojiri jana huko Zanzibar kati ya Mnyama na KMKM
 
Back
Top Bottom