Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,480
- 4,775
Kaka Ngoja tuzichange za Milangoni tutakarabati tu si unajua sisi Mgao wa Kagoda haukutupia, Nyinyi Kandambili matajiri bana maana kuanzia Mafisadi Papa hadi Mafisadi Nyangumi yanatoa Msaada! Ngoja Ligi ikiisha tutatumia pesa ya Zawadi ya Mshindi wa Kwanza Kufanya Ukarabati
Heheeeeee,fanyeni hivyo bana,Simba ni timu kubwa sana aisee
Kuhusu mafisadi kuwekeza kwenye soka mi naona pouwa tu sema Simba sijui imekuwaje miaka hii wakakosa wafadhili(kama ilivokuwa kipindi cha nyuma kwa Mohammed Enterprise,NBC Bank na Tanga Cement),mafisadi wengi siku hizi duniani wanaamua kuwekeza kwenye soka(kama type ya akina Abromavich,Berlusconi n.k)
Binafsi nashangazwa mno kuona mpaka leo vilabu vya Simba na Yanga vinakaa kutegemea mapato ya mlangoni ama wafadhili kama akina Manji,hizi timu zingekuwa makini sasa hivi zingekuwa mbali sana kifedha(zingekuwa na mitaji ya nguvu na ya kutosha),zingejitosheleza kwa kila kitu badala ya kutegemea vitu kama kulipa mishahara ya wachezaji kwa kutegema fedha za akina Manji ama Yanga family na Dionis Malinzi ama Friends of Simba
Hivi wanashindwa kweli kutafuta wadhamini watakaowatumia kutangaza biashara zao kwa malipo mfano Arsenal(Fly Emirates),Chelsea(Samsung),Liverpool(Carlsberg),Man Utd(AIG) n.k.Pia timu zinashindwa nini kutengeneza fulana(jezi) zenye majina ya wachezaji wao,kofia,kaptura,majaketi,tracksuits,masweta n.k na kuanzisha maduka maalum kwa ajili ya kuuza bidhaa zao?,ama wanashindwa nini kuanza kuuza hisa pale DSE??,au timu kama Yanga inashindwa nini kuuendeleza uwanja wake wa Kaunda na kuufanya utumike kwa mechi zao za nyumbani za VodaCom Premier League??..Nafasi zipo nyingi tu wanashindwa kuzitumia
Nilichoona so far ni kwamba politiki nazo zinachangia sana kudidimiza maendelao ya vilabu vya soka vya Tanzania,pia viongozi wengi huingia madarakani kwa lengo la kuvitumia vilabu kama vyanzo vyao vya mapato hivyo kupelekea kuwaza matumbo yao wao na familia zao badala ya kufikiria maendeleo ya vilabu vyao..Pia huwa nashangaa kuona malengo ya viongozi kuwa ni(hasa wa Simba na Yanga) kuwa ni kuifunga Yanga ama Simba badala ya kueleza atafanya nini kuiendeleza klabu kiuchumi..Inasikitisha sana
Pamoja sana wakuu wangu katika michezo


