Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) | Special thread
Zile pesa za SHINYANGA mshalipa mliwatapeli watu ili mlipie geust house kule Kagera ama vipi

tatizo la ndugu zetu makanyagio ni kuhamisha focus, we are talking of our performance on the pitch!!! hiyo ndio focus yetu, hizi distration huwa hazidumu kwani ni periodic.

mbona walipolipwa hakuna tena kelele, au unaishi wapi ndugu yetu?
 
Kumbe mshalipa nilikuwa sina habari lakini sio uungwana kuwatapeli watu!!!
 
Kanda2 hawana kitu mwaka huu..njaa tupu kuanzia wachezaji mpaka benchi la ufundi...nimewakuta wachezaji watatu wa Yanga leo pale mgahawa wa hadees wanataka mlo kwa mkopa...yanga walikuwa wanaota mamilioni ya kombe la mabingwa..hahhahaha...hiyo hela ya kupanda pipa alhamisi wanatembeza bakuli na wakifika Congo wanakula kichapo...
 
Hata wagunge magoli kumi....Tarehe 6 Machi tunatangaza ubingwa, halafu siku ya mechi ya watani wa jadi, Yanga walazimika kujipanga mstari kutupigia makofi wakati wa kuingia uwanjani, maana tutakuwa tunacheza nao tukiwa tayari ni mabingwa!

Tena tutapanga simba kids
 
Hivi jamani sisi tusio na updates kwani what happened to Manji?
 
Kala kona? Duh wanalo walikuwa wanalinga nalo sana hawa. lol
 
wamebaki kuringa na hili jengo lao tuu ambayo tayari vifaa vyumbani vimeshanaza kunyofolewa ili wayauze kupata hela ambazo wachezaji wanawadai....hahahha...wanalia wanataka kuanzisha Friends of Yanga.....
 
Jumla ya Sh.Milioni 20 zimetolewa na mdau mmoja kwa ajili ya maandalizi ya timu za Simba na African Lyon zitakazopambana kesho katika mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Uhuru.
Kwa mujibu wa habari zilizoifikia Nipashe, kati ya fedha hizo, Sh. Milioni 10 wamepewa Simba na kiasi kama hicho wamepewa African Lyon kutoka kwa mdau huyo ambaye ni mtu wa karibu na klabu zote mbili.
Chanzo chetu kiliendelea kusema kwamba lengo la kutoa fedha hizo ni kila upande kufanya maandalizi sahihi ya mechi hiyo bila kuwa na kisingizio ukata.
"Si unajua Lyon imekabidhiwa kwa wadau wa Simba, sasa zimetolewa fedha hizo ili kila upande ufanye maandalizi mazuri na vijana waweze kuonyesha kandanda," kilisema chanzo hicho.
Katika hatua nyingine, kocha msaidizi wa African Lyon, Suleiman Matola, amesema kuwa timu yake imepania kuendeleza ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi.
Matola alisema kwamba wamejipanga kufanya mapinduzi katika mzunguko wa pili na lengo ni kuendelea kubaki kwenye ligi hiyo msimu ujao.
"Tutaifunga Simba, vijana wamejipanga na wanajua cha kufanya, sisi ndio wana- mapinduzi," alitamba nahodha huyo wa zamani wa Simba.
African Lyon iliyokuwa mkiani, imeibuka katika mzunguko huu wa lala-salama na sasa hivi imefikisha pointi 18 ikiwaacha Prisons na Toto African wakiendelea kupumulia 'mashine'.
African Lyon iliyoanza Ligi Kuu kwa kutoka sare ya 1-1 na Yanga msimu huu, iko chini ya kocha mkuu Boniface Mkwasa, na sasa inasimamiwa na wadau wa Simba akiwemo, Kassim Dewji ambao wamepewa jukumu la kuiratibu timu hiyo kuinusuru isiteremke daraja.
Simba na Lyon zilipokutana katika mechi ya mzunguko wa kwanza Oktoba 9 mwaka jana, wana Msimbazi walishinda 1-0.

Kisha msishinde mechi zote ukiwa wadau wa timu za ligi ndio hao hao wenyewe timu yao
 
Hahaaaaaaaa,maneno ya mkosaji hayo mtani....MO aliondoka vp kwani kwenu??...Manji bado yupo Yanga bana na anamwaga mshiko kama kawa

Nasikia na Nyinyi Kandambili bado gemu mbili mtangazaje Ushindi wa Pili! Kila la Heri watani
 
Lol....Nimecheka kweli hapa,ngoja na nyie mchukue ubingwa mwaka huu bana,we fikiria siye tumechukua mara 2 mfululizo tungechukua na mwaka huu Msimbazi pasingekalika,bakora zingetembea mpaka basi
 
hahahaha..wanasherekea nafasi ya pili hao Kanda2....

Nasikia wanataka kususia mechi na Lupopo....

Duh kweli maskini akipata makalio hulia mbwata...Simba mwaka huu mnaongea kuchukua ubingwa mpaka basi,mmesahau kabisa kwamba misimu miwili iliyopita mlikuwa mwaukodolea macho tu ubingwa na kuchezea nafasi ya 2 na 3,leo mnaelekea kupata ubingwa mnachooooooooooonga(wakati wenzenu tungechukua ingekuwa mara 3 mfululizo)...lol

Hakuna habari ya kususia mechi ya Lupopo wala nini(japo Simba mnapenda iwe hivyo),Timu yaondoka Alhamis kwenda Lubumbashi so kama ulikuwa unategemea tutasusia mechi umenoa mazee,imekula kwako
 
Haya leo ni Simba na African Lyon. tembezeni makucha kama kawa
 
<H2>Simba, African Lyon zamwagiwa mamilioni
Na Mwandishi wetu

23rd February 2010

Jumla ya Sh.Milioni 20 zimetolewa na mdau mmoja kwa ajili ya maandalizi ya timu za Simba na African Lyon zitakazopambana kesho katika mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Uhuru.

Kwa mujibu wa habari zilizoifikia Nipashe, kati ya fedha hizo, Sh. Milioni 10 wamepewa Simba na kiasi kama hicho wamepewa African Lyon kutoka kwa mdau huyo ambaye ni mtu wa karibu na klabu zote mbili.
Chanzo chetu kiliendelea kusema kwamba lengo la kutoa fedha hizo ni kila upande kufanya maandalizi sahihi ya mechi hiyo bila kuwa na kisingizio ukata.
"Si unajua Lyon imekabidhiwa kwa wadau wa Simba, sasa zimetolewa fedha hizo ili kila upande ufanye maandalizi mazuri na vijana waweze kuonyesha kandanda," kilisema chanzo hicho.
Katika hatua nyingine, kocha msaidizi wa African Lyon, Suleiman Matola, amesema kuwa timu yake imepania kuendeleza ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi.
Matola alisema kwamba wamejipanga kufanya mapinduzi katika mzunguko wa pili na lengo ni kuendelea kubaki kwenye ligi hiyo msimu ujao.
"Tutaifunga Simba, vijana wamejipanga na wanajua cha kufanya, sisi ndio wana- mapinduzi," alitamba nahodha huyo wa zamani wa Simba.
African Lyon iliyokuwa mkiani, imeibuka katika mzunguko huu wa lala-salama na sasa hivi imefikisha pointi 18 ikiwaacha Prisons na Toto African wakiendelea kupumulia 'mashine'.
African Lyon iliyoanza Ligi Kuu kwa kutoka sare ya 1-1 na Yanga msimu huu, iko chini ya kocha mkuu Boniface Mkwasa, na sasa inasimamiwa na wadau wa Simba akiwemo, Kassim Dewji ambao wamepewa jukumu la kuiratibu timu hiyo kuinusuru isiteremke daraja.
Simba na Lyon zilipokutana katika mechi ya mzunguko wa kwanza Oktoba 9 mwaka jana, wana Msimbazi walishinda 1-0.
</H2>Chanzo: Nipashe
 
Back
Top Bottom