SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Rekodi za Simba msimu huu zimebezwa sana kiasi kwamba watu wamekuwa wanazungumza mambo yasiyo na uhalisia ili tu ajenda zao binafsi ziaminiwe.
Kuna takwimu nyingi zinazothibitisha kwamba Simba ya msimu huu haijafanya vibaya kama tunavyoaminishwa.
Leo nakumbushia kuwa Simba mpaka sasa, zikiwa zimebaki mechi 2-3 kumalizika kwa msimu, Simba ndiyo timu iliyopoteza mechi chache zaidi kuliko zote ikiwa imepoteza mechi 1 tu msimu mzima mpaka sasa.
Kuna takwimu nyingine nyingi za namna hiyo mfano, Simba ndiyo timu iliyofunga magoli mengi, ndiyo timu iliyofungwa magoli machache, nk. Huko kimataifa mchambuzi mwanayanga Ramadhani Mbwaduke amesema mara kwa mara kuwa ukiangalia takwimu mbalimbali za uwanjani, Simba ya msimu huu ni bora kuliko zile za misimu iliyopita.
Ni kweli Simba haijabeba kombe lolote msimu huu ila ni dhahiri juhudi zilifanyika na namba hizi hazidanganyi.