Simba tumefungwa lakini nimeridhika

Simba tumefungwa lakini nimeridhika

chamakh

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2010
Posts
1,075
Reaction score
1,343
Leo tarehe 25 kwenye mechi ya Ngao ya Jamii Yanga SC wamefanikiwa kuwafunga Simba SC kwa goli 1-0.

Pamoja na matokeo hayo binafsi nimeridhika Sana na kiwango pamoja na competitiveness waliyokuwa bayo Wachezaji wetu. Timu ilitengeneza nafasi za kutosha jambo ambalo ndilo la kuangalia.

Pamekuwa na lugha ya ukosefu wa Muunganiko lakini timu yetu imeweza kucheza vyema kiulinzi na hata kiushambuliaji
 
Ongera kwa wacheazaji wetu kwa kuweza kupunguza idadi ya magoli kwa kuwachezea utopolo rafu la sivyo leo magoli yangekuwa mengi

IMG-20210925-WA0031.jpg
 
Kama Simba itacheza hivi msimu huu,itanyanyaswa sana na vitimu vidogo.

Mpira sio show off,mpira ni mipango ya ushindi.

Kuna wakati unatarajia kuwe na kasi kufanya mashambulizi unaona mtu anapiga back pass.

Mwalimu hajapata mfumo mzuri wa kuziba pengo la Luis na Chama.

Wachezaji hawakuwa aggressive wakiingia 18 za yanga.

Mwaka huu tukubali kuanza kujenga kikosi.Ubingwa tumuachie yanga
 
Hatimae mikia FC wameridhishwa!


[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Jicho langu la kimpira naona timu ni nzuri sana, isipokuwa beki ya kushoto na kulia kuna shida kidogo na beki ya kati lazima yule Kennedy acheze either na wawa ama onyango, onyango na wewe wako slow pamoja, kufungwa japo inauma, lakini ndiyo matokeo ya mpira
 
Back
Top Bottom