Simba wa Teranga: Kikosi cha dhahabu kilichotikisa Dunia

Ilikuwa ni mechi ya aibu ya karne kwa ufaransa kufungwa na mtumwa wake.
Kumbuka ufaransa aliwahi mtawala senegal.

Ilikuwa ni fedheha kama sio fadhaha iliyotapakaa kuanzia jiji la paris,marseille,lyon hadi bordeux.
Ilikuwa ni ushindi wa senegal dhidi ya mtawala wake(mkoloni) aliyemtawala kwa karne na dahari.

Ilikuwa ni kama kisasi toka kwa senegali dhidi ya mtawala wake wa zamani.
Naamini furaha,shangwe na nderemo ile toka viwanja vya world cup kule korea/japan viliweza kusambaa kutoka mashariki ya mbali,afrika magharibi dakar na hadi katika malalo(kaburini) kwa baba wa taifa la senegali hayati LEOPARD SEDAR SENGHOR ni kama vijana na vijukuu wa senghor(simba wa teranga) walilipa kisasi kwa niaba yake dhidi ya utawala wa kidhalimu wa ufaransa.

Na kwa francophone wote ilikuwa ni ushindi dhidi ya mtawala wao wa zamani.

Hata sisi inshaaalah siku moja twaweza wafunga watawala wetu wa zamani ujerumani na uingereza kwenye world cup tujisikie furaha kama senegal siku ile walivojisikia furaha.
 
Kumbe huyu dogo musonda wa Chelsea ana asili ya Zambia?
Yaah baba na mama yake wote wazambia mzee wake nae pia alikuwa kiungo akiitwa Charles musonda hata hawa nduguze lamisha na tika wamezaliwa Belgium sababu baba yao alikuwa akikipiga club ya inderlecht ya huko nae musonda jr alizaliwa miaka mitatu baada ya ajali ya wachezaji wa zambia kisa cha kupona baba yake ni kwamba hakuanzia safari zambia yeye ilikuwa wakutane huko huko yeye pamoja na kalusha bwalya. Pia kingine kuna waqt huyu landamila kocha wa Yanga alimualika dogo timu ya Taifa akachomoa pana figisu figisu nyingi kuwa musonda na kalusha hawaelewani sasa inasemekana wazazi wa musonda wanamshinikiza dogo badala ya kuchezea chipolopolo bora achague kati ya England ambapo anaweza kupata haki ya kucheza the three lions kutokana na muda aliokaa wingereza au nchi yake ya kuzaliwa yaani ubeligiji.
 
Ahsante mwanamichezo kwa kumbukumbu sahihi.
 
Shukran sana mkuu kwa maelezo mazuri. Inaonekana ww ni mfuatiliaji na mdau mzuri wa soka
 
Kwa Tanzania hii ya akina Mshindo Msolla na Wallace Karia ambayo haina hata dira au sera ya maendeleo ya soka letu kwa miaka mitano mbele. Tusitegemee chochote
 
Likiisha hili la simba wa teranga, ina bidi sasa tulichambue kosi la Nigeria eagles . lile la kina amokachi Daniel, tijan Babangida, Emmanuel amunike. Uche .
 
Likiisha hili la simba wa teranga, ina bidi sasa tulichambue kosi la Nigeria eagles . lile la kina amokachi Daniel, tijan Babangida, Emmanuel amunike. Uche .

Kipindi Senegal anampiga France upande mwingine ilikuwepo Nigeria super eagles , pale walikuwepo kina Aghahowa, ife soji , beki mstaarabu Taribo West , kina finidi George , Babayaro n.k ! Hawa jamaa walikuwa wamekamilika kwa bahati mbaya wakaangukia kundi la kifo wakiwa pamoja na England’ ya kina beckam , Owen , Argentina ya kina ortega na batistuta .

Kama kawaida yao walikuwa wagumu sana kufungika, beki yao ilikuwa ngumu sana tatizo likawa kwenye kufunga pia , wao , Argentina na Germany ndo walikuwa my favorite

Mwisho wa siku Ikabidi waage kwenye makundi ila kwa mbinde sana ...

 

Mwaka 2002 , Kombe la dunia korea kusini na Japan, Mechi kati ya Nigeria na Argentina ilipigwa siku ya jumapili asubuhi mida ya saa tatu asubuhi kwa majira ya africa Mashariki .

Kona ya kumi ilopigwa na Mkongwe Juan Sebastian Veron Ndio iloondoa Matumaini ya waafrica kuendelea hatua ya robo fainali. Katika mechi ili namkumbuka Diego simeon , Huyu Juan sebastian Veron alipotelea manchester.

Katika Kundi hili la kifo Muingeleza alifanikiwa kuvuka pamoja na Mjerumani, Mechi ilofuata muingeleza akalala mbele ya Brazil mida ya mchana. Mjerumani alifanikiwa kufika fainali yeye na Brazil.

Siku ya Jumapili mchana wa saa tisa Ndani uwanja wa Yokohama ,Mjerumani akalala na Vyuma viwili vya mkongwe Ronaldo luis Nazario De Lima.

Wakumbukwe wafuatao:
Oliver Khan,
Gatuso
Idetoshi Nakata,
Suzuki,
Jugen Klinsman Kocha,
Barack namba 6 Ujeruman,
Caf,
Roberto Carlos (alipotelea Real madrid)
Reonaldo,

MIAKA IMEKIMBIA..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…