THOMASS SANKARA
JF-Expert Member
- Nov 13, 2014
- 2,055
- 4,695
Ilikuwa ni mechi ya aibu ya karne kwa ufaransa kufungwa na mtumwa wake.mechi ile ilichezwa siku ya ijumaa mchana ,ikiwa ni mechi ya ufunguzi wa kombe la dunia, ikihusisha bingwa mtetezi France na timu toka africa,
Mashabiki takribani elfu 60 hawakuamini bingwa mtetezi akidhalilishwa na timu changa toka africa.
watu kama kina Zidane, david trezegut, bathez, viel, thiery henry, Christian kalembeu.
daaah Miaka imekimbia.
Kumbuka ufaransa aliwahi mtawala senegal.
Ilikuwa ni fedheha kama sio fadhaha iliyotapakaa kuanzia jiji la paris,marseille,lyon hadi bordeux.
Ilikuwa ni ushindi wa senegal dhidi ya mtawala wake(mkoloni) aliyemtawala kwa karne na dahari.
Ilikuwa ni kama kisasi toka kwa senegali dhidi ya mtawala wake wa zamani.
Naamini furaha,shangwe na nderemo ile toka viwanja vya world cup kule korea/japan viliweza kusambaa kutoka mashariki ya mbali,afrika magharibi dakar na hadi katika malalo(kaburini) kwa baba wa taifa la senegali hayati LEOPARD SEDAR SENGHOR ni kama vijana na vijukuu wa senghor(simba wa teranga) walilipa kisasi kwa niaba yake dhidi ya utawala wa kidhalimu wa ufaransa.
Na kwa francophone wote ilikuwa ni ushindi dhidi ya mtawala wao wa zamani.
Hata sisi inshaaalah siku moja twaweza wafunga watawala wetu wa zamani ujerumani na uingereza kwenye world cup tujisikie furaha kama senegal siku ile walivojisikia furaha.