Simba hawakucheza chini ya kiwango kabisa.
Watu wengi wanachukulia Simba kutokufunga ndo wamecheza chini ya kiwango angalia ni timu ipi iliposes mpira sana kama siyo simba?
Tuache unafiki
Simba walizidiwa mbinu na tatizo jingine simba walikaa muda mrefu bila mechi tofauti na wapinzani wenzao.
Na hata wanapokuja watu wanasema korona imeisaidia sana simba kufika hapo muelewa sana maana wakati ligi yetu ikiendelea mataifa mengi walikuwa hawachezi
Tatizo ni plan ya simba, simba wanastaili moja tu ya kucheza yaani viunngo wegi .
Wakijua hasa kuwa hatari wanayoweza kuipata ni kurehusu kapombe apande hivyo wakampangia jamaa mwenye nguvu, na kumfanya kapombe asipande, jamaa akagundua siyo kapombe tu Bali hata shabalala ndo akaamua kumwingiza mchezaji mwingine dkk ta 35 Tu akimpa jukumu la kumbana asipande .
Simba ikibanwa mafullbeki wake hawawezi tokea pembeni watataka kupitia Kati na jamaa walikuwa wameshawawin katikati kabisa .
Jamaa waliwaacha wacheze mpiara wao wakatumia counter attack kuwamaliza .
Walikuwa na nidham ya mchezo Sana walipokuwa hawana mpira walirudi wote au kuacha mtu mmoja mbele walikuwa wanapanua uwanja ili kueanyima Simba kukimbia na one touch zao za karibu karibu.
Simba wamecheza sana lkn walizidiwa mbinu na kaizer chiefs