John Gregory
JF-Expert Member
- Jul 14, 2019
- 1,137
- 2,147
Napenda kutumia nafasi hii kuwaasa wananchi wachukue tahadhari kwani Simba wamekuwa wazururaji tena hawana lengo wala shughuli yoyote ya maana wanayofanya mjini na wakati mwingine wanaweza kuwadhuru bila sababu yoyote.
Simba hao wenye hasira kali ambayo haijafahamika chanzo chake wamekuwa wakizurura hapa na pale kuanzia mitaa ya Msimbazi mpaka nyanda za juu kusini huku wakivamia na kusumbua makazi ya wananchi na baadhi yao wamekuwa wakiuawa kiume.
Natoa rai hatua za haraka zichukuliwe ili kuepusha madhara zaidi. NAWASILISHA