Simba wanajaribu kulazimisha tuamini kisaikojia kuwa Yanga hana nafas, ila wanasahau wao walifungwa mechi mbili na bado wakafika robo fainali

Kwahiyo Yanga ndio amejitoa sadaka kwenye kundi ili wengine wote washinde?
Mkuu, Simba alifungwa mechi mbili ndiyo ila kuna sehemu alichukua points 6 nje ndani. Pia Raja alimsaidia Simba kupiga Horoya nje ndani ambaye ndiye alikuwa mpinzani wa Simba. Zaidi ni kuwa mtu ambaye Simba alimpiga nje ndani alimpunguza makali Horoya ambaye alimpokonya point moja. Na pia ambaye Simba alimpiga nje ndani, Raja naye alimpiga nje ndani ambaye tayari alishampokonya Horoya point moja ambaye huyo Horoya alifungwa pia nje ndani na Raja. Kimsingi waliombeba Simba ni Raja na Vipers vinginevyo hata Simba angeshinda nje ndani bila hao kumbeba ingekuwa ndoto kufuzu. Sasa njoo kwa Yanga. Yanga ameshapokonywa point moja na Kinara wa kundi nyumbani ambaye ana uhakika wa kumfunga marudiano. Kinara wa kundi ameshadondosha point moja nyumbani tena kwa mwarabu mwenzie ambaye huyo mwarabu tayari ameshaweka hesabu zake vizuri mbele ya Yanga kwa kuchukua points tatu. Yan jana Yanga alitakiwa ashinde au kama jinsi alivyotoa sare basi ilitakiwa ni lazima Ahyl ampige CR nyumbani ili advantage ibaki kwa Yanga. Kitu kimeenda OP na hesabu sasa zinagoma. Vinara wawili wa juu wa kundi wameshabebana na wote ni waarabu tena wazuri na mbaya zaidi tayari wote wawili wameshazichanga vyema mbele ya Yanga. Yanga hana advantage nyingine zaidi ashinde mechi zake mbili huku akiomba Ahyl ashinde Algeria. Sasa huo uwezekano wa Ahyl kushinda Algeria upo? Ahyl ana uhakika wa pints at least nne kutoka kwa Medeama na Yanga. CR ana uhakika wa points at least nne kutoka kwa Medeama na Ahyl. Wakati Yanga anarudiana na CR. Jumla CR points 8 Ahyl points 9? Sasa Yanga kama atapata points 6 za CR na Medeama ambazo kimsingi ni za jasho na damu atakuwa amefikisha points 8 ( Hapo ili afuzu yataangaliwa mabao, atatoboa?) Mbaya zaidi ni kuwa hesabu zitafungwa rasmi kama CR atamfunga Ahyl Algeria. Yani ikitokea hivyo basi tunasema game is over! Yanga amejikuta kwenye presha kubwa kwa gemu zake zilizobaki na zote ni ngumu. Kutokana na Presha aliyo nayo na gemu alizobaki nazo including za waarabu mbili na ukiangalia mwenendo wake kwa Mkapa huenda akaharibu zaidi. Aisee hesabu ya Yanga iliharibiwa jana tena bahati mbaya sana gemu zote mbili ziliiharibu Yanga na kuivuruga kabisa. Ni kama mkosi vile.
 
Kibabage angeacha ule usenge wake wa kuchelewesha pasi kwenye final third tungekuwa tunaongea mengine leo

All in all pengo la Lomalisa linaonekana wazi kabisa

On to the next one
Hivi pale anashindwa kufanya maamuzi,hata angebutua tu kipa atajua mwenyewe,au aanze kukota kuelekea goli labda hata penati,ila yeye akasimama kabisa hadi majamaa wakajaa golini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona unasema anaweza fung na CR kwann usiseme wew unawez fungwa na medeam hapa kwako
 

Sasa niambie katika mechi ulizo baki nazo utashinda mechi gani?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Acheni kujifariji shughuli imeshaisha hii mkuu
 
Sasa niambie katika mechi ulizo baki nazo utashinda mechi gani?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Acheni kujifariji shughuli imeshaisha hii mkuu
Daah hapa kolo mwenzangu uliyumba sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…