Simba wanakusanya wachezaji wapya badala ya kusajili wachezaji wapya

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Wanamkusanyia wachezaji wapya kocha ajae badala ya kusajili wachezaji kutokana na philosophy ya mwalimu. Nimemsikia kocha mpya wa Singida black stars akitoa angalizo kuwa viongozi wamesajili 90% ya wachezaji bila ushauri wake.

Robertihno na Benchikha waligomba kuhusu wachezaji waliowakuta. Sasa hivi Simba wanachezaji kamali (probability) ileile ya kumkusanyia wachezaji kocha mpya ambae hawajamsajili.

Wemefeli kabla ya msimu haujaanza.
 
Uwoga ni ugonjwa mbaya sana hasa ukiwa hujui unaogopa nini. Nilitegemea utopolo wangefurahia na kukaa kimya ili wasiwastue Simba kwamba wanaboronga ili watupige 10, badala yake wamejawa na hofu, uwoga na kukosa matumaini.

Nyerere aliwahi kusema Ukiona adui yako anakusifia sana jiulize umekosea wapi. Ila Ukiona adui yako anakuponda, wewe ziba masikio kama chura kiziwi maana unakuwa unampiga kwenye mshono. Safari hii utopolo wanapigwa kwenye mishono dadeki. Kelele nyingii ila sisi tumeziba masikio.
 
Simba ni nguvu moja ❤️

Na ikifika derby ya Simba na yanga basi nitaweka Bondi gari zangu tatu, BMW X6, CADILLAC ESCALADE, FORD RANGER RAPTOR.
😃😃😃
 
Uwoga ni ugonjwa mbaya sana hasa ukiwa hujui unaogopa nini. Nilitegemea utopolo wangefurahia na kukaa kimya ili wasiwastue Simba kwamba wanaboronga ili watupige 10, badala yake wamejawa na hofu, uwoga na kukosa matumaini.

Nyerere aliwahi kusema Ukiona adui yako anakusifia sana jiulize umekosea wapi. Ila Ukiona adui yako anakuponda, wewe ziba masikio kama chura kiziwi maana unakuwa unampiga kwenye mshono. Safari hii utopolo wanapigwa kwenye mishono dadeki. Kelele nyingii ila sisi tumeziba masikio.
Kwani mtoa hoja ni timu gani?
 
Wanamkusanyia wachezaji wapya kocha ajae badala ya kusajili wachezaji kutokana na philosophy ya mwalimu. Nimemsikia kocha mpya wa Singida black stars akitoa angalizo kuwa viongozi wamesajili 90% ya wachezaji bila ushauri wake.

Robertihno na Benchikha waligomba kuhusu wachezaji waliowakuta. Sasa hivi Simba wanachezaji kamali (probability) ileile ya kumkusanyia wachezaji kocha mpya ambae hawajamsajili.

Wemefeli kabla ya msimu haujaanza.
Mkuu kumbuka kombe wanalokwenda kushiriki lipo mbioni kufutwa na CAF. Kwa hiyo mwekezaji na viongozi wa Makolo ni lazima wafanye mazingaombwe ili kutuliza mzuka wa mashabiki zao.

Wakipigwa zingine tano wasijeanza kulialia. Wakati Makolo wanatembea na historia ya ushiriki wa kombe la klabu bingwa CAF, Yanga inatembea na "future" yake.

Makolo wakiwa na hesabu za kuishia robo fainali. Miamba ina hesabu za kutwaa ubingwa. Ndiyo! Kwa maana ya jumla mlo wa mchana unaweza kuitwa 'lunch" lakini ubora wa chakula na sehemu mlo unapopatikana huwatofautisha sana walaji wa mlo huo na wapishi pia.

Ukienda kupata "lunch" yako kwa mama ntilie pale Tandale Uzuri, si sawa na yule aliyekwenda Serena Hotel.
 
Uwoga ni ugonjwa mbaya sana hasa ukiwa hujui unaogopa nini. Nilitegemea utopolo wangefurahia na kukaa kimya ili wasiwastue Simba kwamba wanaboronga ili watupige 10, badala yake wamejawa na hofu, uwoga na kukosa matumaini.

Nyerere aliwahi kusema Ukiona adui yako anakusifia sana jiulize umekosea wapi. Ila Ukiona adui yako anakuponda, wewe ziba masikio kama chura kiziwi maana unakuwa unampiga kwenye mshono. Safari hii utopolo wanapigwa kwenye mishono dadeki. Kelele nyingii ila sisi tumeziba masikio.
Kwamba kila tundu lililopo kwenye mwili wa Amfibia mwaka huu litakuwa linatoa milio ya pwiii na fwiii.
 
Lakini ni kocha wa Simba regardless of ukocha mkuu. Kwamba Mgunda akishirikiana na bench la ufundi na scouting hawana uwezo wa kujua mahitaji ya timu?
Lakini mwisho wa siku wakija makocha aina Benchika ndiyo hao hao tena wanaotoka hadharani na kulalamika kufundisha wachezaji wasiofundishika! Kisa tu wachezaji wote amewakuta kwenye klabu.
 
Kocha wa timu ni Mgunda, yeye na wenzie wawetoa mahitaji ya wachezaji. Nyie washauri wa timu mnataka wangefanyaje? Wawe wanawapa Uto kazi ya kusajili?

Mnakuwa kama mmeanza kufuatilia mpira juzi. Kwamba ndio mara ya kwanza kuona usajili kutofanya vizuri? Unafeli usajili wa Man U na Chelsea itakuwa usajili wa Simba?
 
Wanamkusanyia wachezaji wapya kocha ajae badala ya kusajili wachezaji kutokana na philosophy ya mwalimu. Nimemsikia kocha mpya wa Singida black stars akitoa angalizo kuwa viongozi wamesajili 90% ya wachezaji bila ushauri wake.

Robertihno na Benchikha waligomba kuhusu wachezaji waliowakuta. Sasa hivi Simba wanachezaji kamali (probability) ileile ya kumkusanyia wachezaji kocha mpya ambae hawajamsajili.

Wemefeli kabla ya msimu haujaanza.
Nasikia kila mchezaji anatembea na passport yake maana hawajuani.😁😁
 
Back
Top Bottom