subiri filimbi upulizwe, ndo utaina maana halisi ya uzi huu. Gamondi yeye anaziba paa pale tu panapovuja (very specific registration), Azam pia kocha anajua ni kwanini anaacha mchezaji na kwanini anaongeza mchezaji (very specific), simba wanakusanya wachezaji (general), "sijui watamfaa kocha?" sijui wataclick? sijui watamwelewa kocha?. Maana kocha mwenyewe anaetumika (kama ni mgiunda) hana uhakika wa kuwa kocha mkuu wa kikosi. Usajili wa wachezaji ni kama kutafuta miwani ya kuonea maandishi, mgonjwa mwenyewe ndiyo achague size yake inayomfaa. Kocha mkuu inakuwa vizuri kama atasema mwenyewe aletewe mchezaji yupi hasa kwenye timu ambayo haikufanya vizuri kwa misimu 3 mfululizo,