kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Simba hawana uongozi wenye weledi Wala kocha wa level ya Simba, labda nianze kwa kusema hivyo.
Freddy Michael fungafunga wametangaza kutaka kumuuza kwa timu ambayo hawaijui kama itamsajili baada ya kufaulu vipimo, lakini kabla ya kumuuza tayari wameleta mchezaji mpya wa kigeni (Ateba) kuziba nafasi ya fungafunga ambe kaenda tu kwenye majaribio na vipimo kutokana na maelezo ya Ahmed Ally, msemaji wa Simba..
Baada ya Yanga kukitabaruku kiksi kipya cha Simba kwenye mechi ya ngao kocha na uongozi kama sehemu yao ya kujitetea kwanini simba imefungwa Wanataka kumuacha Freddy hata baada ya kwenda nae preseasn na baadae kumtangaza kuwa mchezaji wao wa msimu huu, na baada ya dirisha kubwa la usajili kufungwa katika ligi nyingi. Simba wanawadanganya mashabiki wao kuwa wamemuuza Freddy ambae wamemuacha.
Hata kama huna akili huwezi kuwaelewa, Yaani kumuuzia mtu chakula ulichokitupa jalalani tayari. Huku ni kuminya haki za mchezaji huyu ambae kama ungemuacha mapema huenda angepata timu hapa nchini na kwingine kabla ya madirisha mengi ya usajili kufungwa.
Lakini je, US Algers wasipomtaka Freddy ataelekea wapi? Hii ina maana kuwa ama Freddy aendelee kubaki Simba na Ateba aondoke au wapumguze mchezaji wa kigeni mwingine kikosini au Simba wafungiwe kucheza mpira, maana huwezi kuacha mchezaji wakati madirisha ya usajili yamefungwa, ataenda wapi?