kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Simba haionyeshi ukomavu kwenye soka hata baada ya kufikisha miaka zaidi ya 80 tangu kuanzishwa kwake.
Kila mtu waliwasikia viongozi wa Simba wakimuaga na kumtakia kheri Morrison huko aendako wakimaanisha kuwa aende mbele kwa mbele huko hata kabla ya msimu kumalizika kuonyesha kuwa hawana kazi nae tena.
Huu ni msimu wa usajili kwa wachezaji duniani kote hivyo Morrison alipaswa kupewa barua yake ili imsaidie kupata timu popote duniani.
Kitendo cha Simba kumnyima barua mchezaji ambae hawana kazi nae hata baada ya mchezaji kuiomba sio kitendo cha uungwana kwa Morrison aliyeitumikia Simba kwa mapenzi makubwa sana.
Kitendo hiki sio tu kwamba kitaipa Simba laana kubwa lakini kitawaohopesha na kiwatia hofu wachezaji wengine wa kigeni kwenye club ya Simba.
Uhasama wa Simba na Yanga usivuke viwango vya mpira. Mpira ni maisha ya wachezaji. Morrison asiposajiliwa hasara haiendi kwa Yanga bali kwa Morrison kwakuwa Yanga Ina wachezaji wengi wazuri kama au zaidi ya Morrison.
Hii itaitia Simba hasara, maana wachezaji wengi wa kigeni ipo siku Simba haitakuwa chaguo lao la kwanza kujiunga nayo.