TIMING
JF-Expert Member
- Apr 12, 2008
- 28,186
- 15,549
Nimerudi kuusoma tena huu utumbo…. Kwakweli tuna watu wa hovyo sanaKosa kubwa la Ahmed Ally ni ubinafsi na kulinda kibarua chake kuliko kupigania ubora wa timu...anatumia nguvu nyingi sana kushindana na kina Ally Kamwe na na akina Hashim Ibwe ili aonekane kama yeye ndo semaji namba1 wa mpira hapa nchini.Simba inahitaji wachezaii wake waambiwe ukweli kwasababu wengi ni maingizo mapya na bado wapo katika mchakato wa kuijenga timu.kusifiasifa tu kiboya ni kuwalemaza wachezaji na kuwafanya wabweteke.Aache kabisa kumuiga ally kamwe na masifa yake yeye tayari anakikosa ambacho kimekaa pamoja mda mrefu na tayari ana timu ya ushindani
Ahemd Ally Hataki kabisa kuuzungumzia mpira ila yeye muda mwingi anautumia kusifia ujinga na kuwaaminisha wanasimba wenzie kua tayari simba ina kikosi bora na kikosi cha ushindani lakini kama wewe ni mtu wa mpira ukiona jinsi simba inavyocheza uwanjani utangundua timu bado ina mapungufu mengi sana ya kiufundi...wachezaji hawajitumi na mda mwingi wanapiga back pass na hata wakilazimisha kwenda mbele mipira mingi inapotea kizembe.Mashabiki wa simba walio wengi wameingia kwenye mtego wa
Ahmed Ally hawataki tena kuikosoa timu yao na sasa wameingia kwnye propaganda kua simba inaonewa na marefa na yanga wananunua mechi kupitia kuhonga marefa na udhamini wa gsm na ndomana wanafanikiwa...ila ukitizama "workrate" ya wachezaji wa yanga uwanjani ambao wananunua mechi na "workrate" ya wachezaji wa simba ambao hawanunui mechi ni mbingu na ardhi.
Kwenye mitandao ya kijamii Ahmed Ally ametengeza group la mashabiki wanaojiita "simba influencer" ambao kazi yako ni kuisifia tu timu hata kama haichezi vzr na akitokea mshabiki yeyote wa simba atakaeiongelea simba vibaya basi ataonekana ni mamluki na ametumwa na yanga.Ahmed Ally anatakiwa awaache wanasimba wawe huru kuelezea hisia zao hata kama ni hisia hasi juu ya timu yao kwasababu kukosoa wakati mwingine ndio kujenga.Hawa influencers wamekua kama machawa wa timu na hawako kwa ajilu ya maendeleo ya timu ila wako kwa ajili ya maslahi yao banafsi kwasababu wanaopewa hela za nauli na posho za safari na kujikimu pamoja na viingilio kokote timu inapokwenda..ila ukiwaona kwa jicho la pili unaweza kuwaona kama ndo wapenzi wa simba namba moja ila kiukweli hawa ni machawa tu wa Ahmed Ally na wapo kwa mslahi binafsi ya matumbo yao na sio kwa maslahi ya timu.Hata waandishi wa habari wanaowahoji kila siku kwenye mitandao pia wanalipwa kwa ajili ya kueneza propaganda zao
Kila mwanasimba sasa anaogopa kuikosoa timu yake kwa propaganda zilizotengenezwa na Ahmed Ally ndomana wachezaji wa simba wanabweteka na hawajitumi kwasababu wanajiona tayari wameshakua wakubwa kwa kauli za kuwasifia kila siku za msemaji wao Ahmed Ally lakini impact yao kiwanjani ni ndogo sana
Wanasimba kama wanahitaji timu yao iwe bora waachane na propaganda za Ahmed Ally badala yake wasifie panapohitajika kusifiwa na wakosoe panapohitajika kukosolewa na pia wakubali kujifunza kutoka kwa watanu wao ambao hakuna ubishi wowote kua kwasasa ndio klabu yenye kikosi bora na ndio mabingwa wa nchi misimu mitatu mfululizo
Mytake:
Ahmed Ally anatakiwa ajiuzulu kazi yake ya usemaji kwa maslahi mapana ya klabu kwasababu yeye ndo adui namba1 wa simbaView attachment 3249216
Huyu mleta mada ni hollow kabisa