CHIZI VITABU
JF-Expert Member
- Jun 12, 2021
- 1,061
- 2,477
======
Hajj Manara mwisho wake ni leo, Gsm poleni sana yuda iskarioti is out, Ezekiel ni kama vile anapewa miezi miwili ya transition ili kuendeshwa kitofauti na kusafisha u snitch ulisababishwa na tamaa za kuchukua mahela ya kuishi kifahari mjini.
=====
BAADA ya maneno mengi bila vitendo uongozi wa Simba rasmi umekata mzizi wa fitna kwa kuaamua kuachana na Haji Manara kama Msemaji wa klabu hiyo na kumteua Ezekiel Kamwaga kukaimu nafasi hiyo.
Kamwaga anakaimu nafasi hiyo kwa muda wa miezi miwili, katika kipindi hicho atashiriki katika maboresho ya muundo wa utendaji wa idara hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo imeridhia mtakwa wa Manara kuto kuendelea kudumu katika nafasi hiyo.
"Tunamshukuru kwa maneno aliyoyatumia kutuaga wanasimba katika kundi la viongozi wa Simba (Simba HQ), kwa kazi aliyoifanyia klabu katika kipindi alichoshika nafasi na inamtakia kila heri katika shughuli zake,".
"Mara baada ya kukamilika kwa maboresho ya idara ya habari na Mawasiliano na Idara nyingine, klabu itatangaza fulsa mbalimbali za ajira katika kipindi cha wiki chache zijazo," imesema taarifa hiyo.
zaidi, soma: Haji Manara amtuhumu Barbara kuwa na chuki dhidi yake. Amuahidi ataondoka Simba kwani amemkuta