GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Nichukue nafasi hii adhimu kabisa Kumpongeza Kaka yangu katika Fani ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma Ezekiel Kamwaga kwa Kuteuliwa huku Kukaimu hii nafasi.View attachment 1871232
======
View attachment 1871250
Hajj Manara mwisho wake ni leo, Gsm poleni sana yuda iskarioti is out, Ezekiel ni kama vile anapewa miezi miwili ya transition ili kuendeshwa kitofauti na kusafisha u snitch ulisababishwa na tamaa za kuchukua mahela ya kuishi kifahari mjini.
Ni Mwandamizi Kwangu, Mweledi, Msikivu, Mwelewa na Kubwa kabisa Ezekiel Kamwaga ameiva si tu Kimaadili bali hata kwa Hekima na Busara.
Ana Shule (Elimu) nzuri na pia ni Mzungumzaji mzuri mwenye kujua wapi aseme nini na wapi pia asiseme. Hata alipokuwa na nafasi hii huko nyuma kabla Simba SC haijaiingia katika Mabadiliko aliitendea Haki hiyo (hii) nafasi tuliokuwepo tuna Ushahidi nalo.
Na Kitu pekee ambacho GENTAMYCINE nakipenda kwa Kaka Ezekiel Kamwaga hata akiwa 'Newsroom' kote alikopita ni Mtu asiyependa Makuu Wala Sifa za Kijinga kama si za Kipumbavu kama za Mtangulizi wake aliyekuwa Mnafiki na Chawa.
Tafadhali sana Kaka (Comrade) Ezekiel Kamwaga nimekumwagia Sifa zote hizi kwakuwa GENTAMYCINE nakujua vyema kwani katika Tasnia ya Uandishi wa Habari (hasa za Michezo) nchini Tanzania Wewe si tu ni Mwandamizi bali pia ni Nguli hivyo usiniangushe nikaja Kuumbuka na Kuchekwa hapa.
Yale mema (mazuri) ya Mtangulizi wako Haji Manara yaboreshe Kiufanisi zaidi ila yale yake mengi ya Kipuuzi tafadhali nakuomba mwachie nayo Mwenyewe ili akayaendeleze huko kwa waliokuwa wakimtumia 'Kutuumiza' wana Simba SC kila inapocheza na Yanga SC hasa katika Mechi za Ligi Kuu ya Tanzania (VPL)
Mwisho kabisa nichukue nafasi hii pia Kuupongeza Uongozi wa Simba SC kwa Kumteua Kaka yangu katika Fani Ezekiel Kamwaga Kukaimu nafasi hii na GENTAMYCINE ambaye najua hata nyie ( Viongozi wa Simba SC huwa mnaniheshimu ) niwaombeni tu hata msipoteze muda wenu mwingi Kumthibitisha kuwa Msemaji wetu Mkuu wa Simba SC kwani ana Sifa zote 'tukuka' ya Kushika hicho Cheo na hapa kwa Ezekiel Kamwaga Klabu ya Simba imefanya Usajili wa Thamani Kubwa katika Uongozi na Utendaji wa Klabu.
Ezekiel Kamwaga Mungu akakusimamie.