Nipo hapa Johari Rotana kama moja ya wahudhuriaji. Nipo hapa kuwaletea kinachojiri
Ahmed yupo Live kutuambia nini kitakachojiri.
Sundaland anatangazwa kama mzalishaji na msambazaji wa jezi za Simba Sc. Mkataba ni miaka miwili kwa thamani ya bilioni 2 kwa kila mwaka.
SIMBA YAACHANA NA VUNJA BEI, YASAINI MKATABA WA TSH. BILIONI 4
Simba imesaini mkataba wa miaka miwili wa utengenezaji na usambazaji wa jezi na Kampuni ya Sandaland The Only One, ambapo kwa mwaka mmoja utakuwa na thamani ya Tsh. Bilioni 2
Mdhamini wa jezi wa klabu hiyo aliyepita Vinja Bei alisaini mkataba wa Tsh. Bilioni 1 kwa mwaka
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Salim Abdallah Muhene ‘Try Again’ amesema “Wanasimba watarajie mambo makubwa ikiwemo katika usajili unaofuata wakati tukishuhudia nyumba ya jirani ikiendelea kuungua.”