Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Kikosi cha Simba kimeondoka jijini Dar es Salaam leo asubuhi kuelekea jijini Arusha kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union utakaopigwa keshokutwa Jumapili kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Simba yenye pointi 51 inahitaji ushindi katika mchezo huo ili kuendelea kuipa upinzani Yanga yenye pointi 55 katika mbio za ubingwa.
Mlinda mlango namba moja wa Simba SC, Moussa Camara mlinzi Che Malone, Kiungo Mzamiru Yasini wataukosa mchezo wa kesho dhidi ya Coastal Union kutokana na majeraha.
Ikumbukwe kuwa Simba iliambulia sare ya 2-2 dhidi ya Coastal Union kwenye mchezo wa mzunguuko wa kwanza msimu huu 2024/25 uliopigwa Uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam.