Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Klabu ya Simba imeruhusiwa kufanya mazoezi uwanja wa Benjamin Mkapa tarehe 14 Juni 2025, siku ya Jumamosi ambayo ni siku moja kabla ya mechi ya 'DABI' dhidi ya Yanga SC.
Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo imewaandikia barua hiyo hapo juu klabu ya Simba ambayo ndiyo klabu mgeni kwenye mchezo huo ili kuhakikisha kanuni za Ligi Kuu zinafuatwa na kutimizwa. Barua kutoka Wizarani kwenda Simba SC imeandikwa Juni 9, 2025.
===
TAARIFA YA MAZOEZI RASMI YA TIMU TAREHE 14 JUNI 2025
Tafadhali husika na somo tajwa hapo juu.
2. Wizara imepokea barua yako yenye Kumb. Na. SSC/WUSM/09/06/2025/01 ya tarehe 09 Juni, 2025 kuhusu taarifa ya mazoezi rasmi ya timu ya Simba SC tarehe 14 Juni, 2025.
3. Kwa muktadha huo tunawafahamisha kwamba uwanja upo tayari kwa mchezo huo na Wizara haina kipingamizi na timu kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya mechi kwa mujibu wa kanuni. Aidha, Wizara inapenda kusisitiza kwamba itaendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi wa vilabu vyote nchini wanaoomba kutumia uwanja wa Benjamin Mkapa na vingine vyote vilivyopo chini ya Wizara bila ya kukwamisha kwa namna yeyote matumizi ya viwanja hivyo.
4. Aidha, mnakumbushwa kukamilisha taratibu zote za maandalizi ya mechi ikiwemo kushiriki pre-match meeting ambayo huratibiwa na wasimamizi wa ligi kwa mujibu wa taratibu za ligi.