Simba yapewa ruhusa rasmi kufanya mazoezi ya mwisho Uwanja wa Mkapa kuelekea Dabi Juni 15

Simba yapewa ruhusa rasmi kufanya mazoezi ya mwisho Uwanja wa Mkapa kuelekea Dabi Juni 15

Leo hii wanaweka barua ya kuruhusiwa kufanya mazoezi na wizara,,sasa sisi inatuhusu nini? Mbona barua ya kuomba kufanya mazoezi ya trh 8 awakuipost mitandaoni? Kuruhusiwa kufanya mazoezi ni jambo la kawaida kwa mwenye uwanja kukataa ama kukubali ivyo sioni kitu icho kama ndio kitaifanya mechi iwepo ni Yale Yale maigizo ya wakina mtanga na bambo!
 
GtUAydqXAAAhf-2.jpg
 
Walete na barua iliyowaruhusu kufanya mazoezi tar 07.
Huwa hakuna ulazima wa kutoa barua hadharani kama hivi, ni maamuzi tu yao kufanya hivi. Muhimu wamehakikishiwa matumizi ya uwanja ili kumaliza minong'ono yote kuhusiana na uwanja utakaotumika na pia ruhusa ya kutumia uwanja kwa mazoezi.

Pamoja na ruhusa na barua hii, Simba inaweza ikaamua hata isiende kufanya hayo mazoezi.
 
WATU WAMEAMUA MWAKA HUU INJINIA KAKIMBIA KESHAONA MSALA HUU KAUANZISHA KUUMALIZA KASHINDWA
 
Klabu ya Simba imeruhusiwa kufanya mazoezi uwanja wa Benjamin Mkapa tarehe 14 Juni 2025, siku ya Jumamosi ambayo ni siku moja kabla ya mechi ya 'DABI' dhidi ya Yanga SC.

Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo imewaandikia barua hiyo hapo juu klabu ya Simba ambayo ndiyo klabu mgeni kwenye mchezo huo ili kuhakikisha kanuni za Ligi Kuu zinafuatwa na kutimizwa. Barua kutoka Wizarani kwenda Simba SC imeandikwa Juni 9, 2025.

===

TAARIFA YA MAZOEZI RASMI YA TIMU TAREHE 14 JUNI 2025

Tafadhali husika na somo tajwa hapo juu.

2. Wizara imepokea barua yako yenye Kumb. Na. SSC/WUSM/09/06/2025/01 ya tarehe 09 Juni, 2025 kuhusu taarifa ya mazoezi rasmi ya timu ya Simba SC tarehe 14 Juni, 2025.

3. Kwa muktadha huo tunawafahamisha kwamba uwanja upo tayari kwa mchezo huo na Wizara haina kipingamizi na timu kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya mechi kwa mujibu wa kanuni. Aidha, Wizara inapenda kusisitiza kwamba itaendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi wa vilabu vyote nchini wanaoomba kutumia uwanja wa Benjamin Mkapa na vingine vyote vilivyopo chini ya Wizara bila ya kukwamisha kwa namna yeyote matumizi ya viwanja hivyo.

4. Aidha, mnakumbushwa kukamilisha taratibu zote za maandalizi ya mechi ikiwemo kushiriki pre-match meeting ambayo huratibiwa na wasimamizi wa ligi kwa mujibu wa taratibu za ligi.

Ze comedy
 
WATU WAMEAMUA MWAKA HUU INJINIA KAKIMBIA KESHAONA MSALA HUU KAUANZISHA KUUMALIZA KASHINDWA
Watu wamemuangalia na kumsikiliza AliKamwe wamemuona kama ka mbwa tu, ka puppy kalikotumwa kubwekabweka. Hamna mtu amekuwa na tyme naye. Wanamsubiri aliye nyuma ya huyo mbwa, aje front aache kujificha kwenye sketi
 
Watangaze na Viingilio... Coz hatujui Kiingilio ni Bei gani
 
Hii barua imeenda kumaliza utata wa tarehe 7 March 2025.
Simba waliomba wizarani au popote kufanya mazoezi siku ile?
Kama hawakutoa taarifa kabla kiongozi aliye piga simu kuzuia wasiingie alikuwa sahihi.
Yanga hawezi kuadhibiwa kwa kosa lisilo lao hawajawazuia Simba.
Hapa wanazidi kujivua nguo,Kumbe inatakiwa barua itoke ndiyo wakafanye mazoezi,Na tarehe 7 hawakuwa na barua.
 
Mbumbumbu fc wanahangaika😀😀 Ombeni na Kibali cha mechi kabisa.
Yooote iyo mnataka mashabiki wenu waingie kwenye mfumo.
Baadae utasikia izo ticket mtatumia Simba Day😃😃
 
Leo hii wanaweka barua ya kuruhusiwa kufanya mazoezi na wizara,,sasa sisi inatuhusu nini? Mbona barua ya kuomba kufanya mazoezi ya trh 8 awakuipost mitandaoni? Kuruhusiwa kufanya mazoezi ni jambo la kawaida kwa mwenye uwanja kukataa ama kukubali ivyo sioni kitu icho kama ndio kitaifanya mechi iwepo ni Yale Yale maigizo ya wakina mtanga na bambo!
Hahahahaha,kwani safari hii wamekataliwa mpk waombe kibali wizarani?
 
#MICHEZO: Klabu ya Simba imethibitisha kupokea barua rasmi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhusu mchezo wa dabi ya Kariakoo ambapo imeruhusiwa kufanya mazoezi katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Tumepokea barua rasmi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuruhusiwa kufanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Mkapa hapo kesho Jumamosi” Simba SC

#Michezo #Hainakuchoka #EastAfricaTV @nickymeena_
 
Back
Top Bottom