Simba yatozwa milion 3 kwa imani za kishirikina kwenye mchezo dhidi ya Yanga ilipofungwa 2-0

Frank Wanjiru

Platinum Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
25,686
Reaction score
46,842
Klabu ya Simba Sc imetozwa faini ya jumla ya Tsh milioni tatu kwa makosa matatu waliyoyafanya katika mchezo namba 184 wa Derby ya Kariakoo dhidi ya Yanga Sc uliomalizika kwa Yanga Sc kushinda 2-0 katika dimba la Benjamin Mkapa mnamo Juni 25, 2025.

Kwa mujibu wa taarifa ya leo Julai 17, 2025 ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Simba Sc imeadhibiwa kwa kutozwa faini ya Tsh milioni moja kwa kosa la kushindwa kuhudhuria mkutano wa wanahabari uliofanyika kwenye ukumbi wa Benki ya Taifa ya Biashara Dar es Salaam Juni 24, 2025 kinyume na matakwa ya Kanuni ya 17:58 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Katika hatua nyingine kikao cha Kamati ya TPLB kilichofanyika Julai 15, 2025 kimetoa uamuzi wa kuiadhibu Simba Sc kwa kuitoza faini ya Tsh milioni moja kwa kosa la kushindwa kuhudhuria kikao cha kitaalam cha maandalizi ya mchezo (MCM) Juni 24, 2025 kinyume na matakwa ya Kanuni ya 17:2(2.2) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Aidha Simba Sc imeadhibiwa kwa kutozwa faini ya milioni moja kwa kosa la kuingia kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kupitia mlango usio rasmi kuelekea mchezo huo uliochezwa Juni 25, 2025, kinyume na matakwa ya kanuni ya 17:21 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo, adhabu ambazo zimetolewa kwa mujibu wa kanuni ya 17:62 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
 
hawa jamaa wanawekeza sana katika haya mambo. ukisikia fulani sijui msaliti basi jua ni haya mambo. ila makolo ni balaa.
 
Kuna swali nataka kukuuliza japo kichwa Cha Habari na content havina uwiano, ila swali langu kwanini unaichukia Simba..? Yan najiuliza chuki yako kwa Simba imekusaidia nini maishani...mbona kama ni umaskin uliokithiri kuichukia timu yenye wachezaji wanaolipwa pesa nyingi..grow up !
 
Yaani uchawi mfanye nyie halafu lawama unipe mimi,kwanza umesoma Uzi wote?
 
Yaani uchawi mfanye nyie halafu lawama unipe mimi,kwanza umesoma Uzi wote?
Unaichukia Simba huna lolote. Huna credible source kudhibitisha kua Simba imefanya uchawi. Kupita mlango usio rasmi ni la ajabu nchi hii kwa timu za Simba na yanga? Mbona yanga inapita milango isiyo rasmi nao ni wachawi? Naamini chuki yako kwa Simba inakusaidia kupata japo mkate tu kwa ajili ya watoto wako.
 
Hela nyingi na ushirikina vinaenda sambamba, Simba acheni mambo ya ushirikina, hayawasaidii, ona sasa mnaloga na bado mnapigwa, si ujinga huu, naona mbadili mganga, badala ya kuwaloga yanga anawaloga nyie
 
Ule nyingi na ushirikina vinaenda sambamba, Simba acheni mambo ya ushirikina, hayawasaidii, ona sasa mnaloga na bado mnapigwa, si ujinga huu, naona mbadili mganga, badala ya kuwaloga ya ga anawaloga nyie
Watumie huu ujumbe na yanga pia. kama kuingia milango isiyo rasmi ni uchawi basi hata yanga nao wachawi mana wameshaingia milango isiyo rasmi mara nyingi tu...uchawi wa yanga kwenye Ile mechi niseme ulikua mkubwa zaidi ya Simba ...hongereni kwa kushinda kichawi.
 
Mkuu unajielewa kweli wewe,kwa hiyo hizo adhabu mimi ndio nilizozitoa badala ya TFF?kumbe husomagi habari kwa undani ndio maana unaishiaga kutukana watu matusi humu
 
Bora Yanga mchawi wao yupo "very" simba mnatapeliwa na mwekezaji, wachezaji, uongozi hadi waganga...kuna kitu hakipo sawa hadi mzee saidi anaisifia yanga
 

Attachments

  • 60ee1407a06495cdae6c80ea0968eff6.mp4
    5.8 MB
Jamani hi kali..
Kwani yeye ndo ameitoza faini hyo simba?
Watu wengne bhana kama wa papua guinea tu
 
Jamani hi kali..
Kwani yeye ndo ameitoza faini hyo simba?
Watu wengne bhana kama wa papua guinea tu
Huyo dogo ana msongo wa mawazo maisha yake magumu sana ndio maana kaamua kuwa Chawa wa MO,kazi kubwa anayoijua ni matusi tuu.
 
hawa jamaa wanawekeza sana katika haya mambo. ukisikia fulani sijui msaliti basi jua ni haya mambo. ila makolo ni balaa.
Hivi mtu unapigwa mara Tano mfululizo unaendeleaje kwenda kuroga? Sema ushirikina kwenye vilabu ni miradi ya watu. Kuna watu wanakula pesa nzuri na waganga. Hata wewe ukisikia mtu anasema akupeleke kwa mganga kuwa makini, wengi wanakula na waganga.
 
Sijaona huo ushirikina au ndio waandishi wa shule za kata??
 
hii ni habari,kwa kuwa wewe ni kolo umeona na kutafsili kama mleta mada ana chuki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…