Simba yatuma rasmi ombi kwa Idara ya Uhamiaji kuomba uraia wa wachezaji wake 9 wa kigeni

Kwa maslahi mapana ya mpira naidhinisha wapewe uraia mara 1 hii ni executive order.
 
Hili jambo litamchafua sana mwigulu sema athari zake kisiasa atakuja ziona mbele
 
Kwani utaratibu ukoje kisheria? Anayeomba uraia ndiye anatakiwa kutuma maombi au mhusika anaweza kuombewa uraia hata kama hataki?
 
Ccm kwa hakika wanaiharibu sana hii nchi. Nakumbuka baba yake Dodi Al Fayed alikaa Uingereza kwa zaidi ya miaka 30 lakini hakuwahi kupewa uraia kwa sababu uraia ni true national identity and the reflection of culture of the given people hivyo sio kitu cha kutolewa kijinga jinga kama serikali hii inavyojaribu kufanya.

Siku moja tutashangaa rais wa nchi ya Tanzania anakuwa ni mwenye asili ya Nigeria, Cote D'Ivoire, Ghana au hata Burundi.

Kadri ccm itakavyoendelea kubakia mamlakani ndio hii nchi itakavyoendelea kuharibika zaidi na zaidi.
 
Wakuu hizi habari mnazitoa wapi? Halafu Taasisi kuwaombea wafanyakazi uraia ipo kisheria?
 
Kwanini watu weusi tunakuwa wabinafsi sana?

Mbona mkisikia mtu mweusi amekuwa Rais pale Marekani mnafurahi?

Mkisikia mtu mwenye asili ya Tanzania kachaguliwa kuwa Meya wa London mnafurahi?

Kila siku nawaambiwa watu hii ngozi nyeusi ingekuwa na uchumi mzuri hizo race nyingi zote zingeisoma namba.
 
Sheria zifuate mkondo wake na si kutumia vyeo ndani ya serikali!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…