Simba yawaonesha Yanga namna ya kufuzu robo fainali

Simba yawaonesha Yanga namna ya kufuzu robo fainali

Msimu uliopita kuna timu ilitoa somo la jinsi ya kucheza fainali na sio kuishia robo, msimu huu kaishaingia anapiishia mwenzie ngoja tuone kama na huku atatoa somo hilo au lah
Kama hiyo timu ilicheza na wababe sawa ila kama ilicheza na vitimu vya kajificheni silioni somo..
 
Nimeandika pumba!! Naujua mpira kuliko unavyofikiria Simba mseme kwenye ligi ila kweny CAF champion ni Habari nyingine
Kama unajua mpira je Yanga imefuzu robo fainali kwenye mechi ipi?
 
Nimeandika pumba!! Naujua mpira kuliko unavyofikiria Simba mseme kwenye ligi ila kweny CAF champion ni Habari nyingine
Kwenye CAF champions league si mnaishiaga kwenye hatua ambayo Yanga imeingia au kuna kipi kipya tofauti na hiko?
 
Kama hiyo timu ilicheza na wababe sawa ila kama ilicheza na vitimu vya kajificheni silioni somo..
Embu kwanza kwa kunitajia wababe ili niwajue.
Maana Tp Mazembe alikuwepo kule alipigwa nje ndani. Au ulikuwa unakusudia wababe kama vile bingwa wa Algeria aliyekula goli nne?
 
Sisi tulikua tunashiriki kwa kanuni, na nyie washiriki wa halali mlikua mnakwama wapiiiii?? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kwani na nyie mlikuwa mnakwama wapi tena kwa miaka mingi tu?

Kwa maneno mengine, ukiacha miaka hii mitano ikiwemo kama miwili ya kushiriki kwa kanuni, huko nyuma mlikuwa mnafeli wapi?

Mbona hilo swali hujiulizi kabla ya kutuuliza sisi?
 
Kwani Yanga walikosa magoli mangapi?

Mbona hata Yanga alimchapa mtu(Coffee ya Ethiopia) bao 6-1 kutinga hatua ya makundi mwaka 1998?
Walisababisha msiba mkubwa sana Iringa mjini, watu 13 walifariki dunia baada ya basi la Fresh ya Shamba kuligonga daladala (hiace). Konda wa fresh ya Shamba alichukua gari pasipo ruhusa ya dereva akawa analiendesha zigzag style kusherehekea ushindi wa yanga
 
Yanga kaingiaje hapo? Yanga alikuwa anawatizama humu miguu ipo mezani na pembeni yupo popcorn, sasa anaingiaje ?
 
Ndio nimeshangaa, yaani Yanga imefuzu tokea wiki iliyopita halafu mtu anakuja kuandika pumba hapa. Inawezekana mpira ajui huyo anafikiria labda Yanga imefuzu jana.
Ilitakiwa aandike kabla makolo hajacheza
 
Embu kwanza kwa kunitajia wababe ili niwajue.
Maana Tp Mazembe alikuwepo kule alipigwa nje ndani. Au ulikuwa unakusudia wababe kama vile bingwa wa Algeria aliyekula goli nne?
Endelea kukaza fuvu sina muda wa kubishana najua unaelewa..
 
Kwani na nyie mlikuwa mnakwama wapi tena kwa miaka mingi tu?

Kwa maneno mengine, ukiacha miaka hii mitano ikiwemo kama miwili ya kushiriki kwa kanuni, huko nyuma mlikuwa mnafeli wapi?

Mbona hilo swali hujiulizi kabla ya kutuuliza sisi?
Nakuuliza wee badala ya kujibu unajiuma uma, miaka mingi kuzidi nyie? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwani Yanga walikosa magoli mangapi?

Mbona hata Yanga alimchapa mtu(Coffee ya Ethiopia) bao 6-1 kutinga hatua ya makundi mwaka 1998?
Hii mada inazungumzia kutinga robo fainali.
Achana na hatua ya makundi.

Ukitaka kuzungumzia hatua ya makundi fungulia thread yake.
 
Back
Top Bottom