Simbachawene atetea uamuzi wa kuzuia mikutano ya hadhara. Avuliwe Uwaziri!

Simbachawene atetea uamuzi wa kuzuia mikutano ya hadhara. Avuliwe Uwaziri!

Waziri wa Nchi, Sera na Uratibu wa Bunge Simbachawene, ni miongoni mwa Mawaziri wa Serikali ya CCM ambaye anaonekana dhahiri kwamba hajaridhishwa na uamuzi wa kuondolewa kwa zuio batili la mikutano ya vyama vya siasa...
Amenukuliwa leo akitetea uamuzi ule wa kidikteta uliojaa uoga na ushamba kwamba ulikuwa halali kwa wakati ule, kwa vile serikali halali iliyochaguliwa na wananchi ilihitaji utulivu ili ilete maendeleo, kwake Simbachawene kuvunja Katiba ndio kuleta maendeleo, huyu ni Waziri, kwamba sasa hivi hawahitaji huo utulivu ili kuleta maendeleo?[emoji817][emoji818]
 
Viongozi wanafiki na wanaotetea uovu kama huyu Simbachawene hawastahili kuwemo kwenye serikali za kileo, kwani ilikuwa lazima aropoke huo ujinga wake? Ni dhahiri kwamba huyu hajaridhishwa na uamuzi wa Rais, ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama chake, NASHAURI AVULIWE UWAZIRI HARAKA.

Hiki kichwa ni chakuliwa haraka sana!
 
Anajua fika kabisa kwamba wapinzani kwakiruhusiwa wapite mitaani kwa mikutano ya hadhara- ofisi za hawa mawaziri zitakuwa hazikaliki kabisa.
 
Viongozi wanafiki na wanaotetea uovu kama huyu Simbachawene hawastahili kuwemo kwenye serikali za kileo, kwani ilikuwa lazima aropoke huo ujinga wake? Ni dhahiri kwamba huyu hajaridhishwa na uamuzi wa Rais, ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama chake, NASHAURI AVULIWE UWAZIRI HARAKA.

Hiki kichwa ni chakuliwa haraka sana!
ni kweli, yaonekana Rais kapata washauri wazuri, tulipokuwa tunakwenda kulikuwa siko kabisa still kuna viongozi waandamizi wa Serikali yetu kama hawa ambao bado wanaamini siasa za 2015 - 2022 zilikuwa sahihi.
 
Kwani kwa sasa kuna maendeleo gani zaidi ya mchwa wa samia kufisidi nchi ...watz tukipata mashine kama jpm hata uchaguzi wa rais hatutaki ni kupoteza pesa bure tunatamani awe rais wa maisha
Aibu sana kwa Wazazi wako
 
Tangu lini tukachagua kwa sera? Tunaangalia mtu,chama au pesa.
Labda huko kwenu, huku kwetu watu hawaangalii chama....tena ukitaja CCM ndo hawaelewi, Kwa mara ya kwanza tangu nipate akili diwani wa CCM alishinda kupitia ule uchafuzi wa 2022, ubunge alinyimwa Azan na mipesa yake akashinda wa CUF....Ila Yule nyooko alikuja kuunga mkono juhudi 🤣
 
Mm kama ni amri yangu baada ya uchaguzi vyama vya siasa visifanye mikutano ya hadhara badala yake mikutano ya ndani iwe ruksa na ikifika mwaka mmoja kabla ya uchanguzi wowote ule mdogo na mkubwa iruhusiwe mikutano ya nje pia.
Katiba haisemi hivyo! Kwanza mantiki ya mikutano ya hadhara sio kupinga maendeleo wala kukosesha utulivu katika umma, Bali ni kuelimisha wananchi juu ya mambo mbalimbali yahusuyo mustakabali mzima wa maisha yao.

Ni fursa ya kuwezesha wananchi kujua serikali yao inawatoa wapi na kuwapeleka wapi? Na wanakopelekwa ndiko au laa?

Zaidi ya yote, nmikutano hiyo ndio huwezesha vyama vichanga vyenye sera mbadala na chama tawala kutangaza sera zao ili kupata uugwaji mkono na ufwasi kutoka kwa wananchi.

Hatua hii kwa ujumla inaweza vyama hivi vichanga kukuwa kimuundo na kimtandao! Chama hakiwezi kushika hatamu za uongozi wa nchi bila kuwa mtandao mzuri wa kimuundo nchi nzima! Ni dosari hii ndio iliyoiangusha CCR Mageuzi ya Mrema uchaguzi mkuu wa mwaka 1995.

Aidha vyama havilamishi raia kuacha shuguli zake kwenda mikutano ya hadhara ,bali ni kwa mapenzi ya raia wenyewe. Hivyo si sahihi kabisa kufanya jitihada zozote za kuzuia mikutano hiyo achilia mbali haki halali za kikatiba.
 
Uamuzi wa kuzuia mikutano ya hadhara haukua wa Magufuli. Ulikuwa ni wa vikao vya juu vya CC mwishoni wakati JPM anaingia, ilionekana...
Hakuna kitu kama hicho! Ule uamuzi ulikuwa uamuzi binafs wa JPM na aliutoa siku alipokuwa akipokea ripot ya Tume ya Uchaguzi!

Kuna mambo mengi tu ambayo yalikuwa yakiamuliwa au kushauriwa au kupendekezwa na hivyo vikao lakini yeye akitoka huku nje anapiga anavyojua yeye au hukuwahi kumsikia akisema yeye ukimshauri ndio umeharibu? Au hujui kama mwenekiti wetu alikua hashauliki?

NI mara ngapi viongozi wa dini waliomba kukutana nae akawapiga chenga na walipotoa ushauri kupitia mahubiri yao ulisikia walivyojibiwa? Vipi viongozi wa dini waliojaribu kukosoa serikali? Kamuulize Kakobe si yupo mpaka leo? Vipi Askofu aliyeambiwa sio raia wa Tanzania ulimsikia!?
 
Waziri wa Nchi, Sera na Uratibu wa Bunge Simbachawene, ni miongoni mwa Mawaziri wa Serikali ya CCM ambaye anaonekana dhahiri kwamba hajaridhishwa na uamuzi wa kuondolewa kwa zuio batili la mikutano ya vyama vya siasa...
Mkuu mbona kama una chuki binafsi na Simbachawene hivi, au kuna mtu anakutumia kumchafua mzee wa watu?. Tambua ya kwamba hata akitumbuliwa hauwezi kuteuliwa wewe kushika huo wadhifa wake.
Pambania mkate wako wa kila siku acha kuwachafulia watu vibarua vyao hiyo ni dalili ya roho mbaya

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Simbachawene ana uhuru wa kutoa maoni yake, timu gaidi acheni kumshambulia
Kwenye serikali kuna collective responsibility
Mimi CCM .Waziri kumpinga raisi openly kwenye press haiko sawa angeongea kwenye kikao cha baraza la mawaziri ana forum hiyo kule

Raisi Samia nampa ushauri wa bure ateue waziri mwingine amwache tu na ubunge
 
Waziri wa Nchi, Sera na Uratibu wa Bunge Simbachawene, ni miongoni mwa Mawaziri wa Serikali ya CCM ambaye anaonekana dhahiri kwamba hajaridhishwa na uamuzi wa kuondolewa kwa zuio batili la mikutano ya vyama vya siasa...
Fanyeni sio kila wakati wa kupiga domo tu siasa. Mtazalisha Mali sangapi!?
 
Waziri wa Nchi, Sera na Uratibu wa Bunge Simbachawene, ni miongoni mwa Mawaziri wa Serikali ya CCM ambaye anaonekana dhahiri kwamba hajaridhishwa na uamuzi wa kuondolewa kwa zuio batili la mikutano ya vyama vya siasa.

Amenukuliwa leo akitetea uamuzi ule wa kidikteta uliojaa uoga na ushamba kwamba ulikuwa halali kwa wakati ule, kwa vile serikali halali iliyochaguliwa na wananchi ilihitaji utulivu ili ilete maendeleo, kwake Simbachawene kuvunja Katiba ndio kuleta maendeleo, huyu ni Waziri, kwamba sasa hivi hawahitaji huo utulivu ili kuleta maendeleo?

Viongozi wanafiki na wanaotetea uovu kama huyu Simbachawene hawastahili kuwemo kwenye serikali za kileo, kwani ilikuwa lazima aropoke huo ujinga wake? Ni dhahiri kwamba huyu hajaridhishwa na uamuzi wa Rais, ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama chake, NASHAURI AVULIWE UWAZIRI HARAKA.

Nakala: Abdulrahman Kinana
View attachment 2469961
jamaa hajasoma alama za nyakati.
 
Simbachawene ana mtoto wake ana matusi balaa.

Alimtukana polisi mwenye umri Wa baba yake matusi ya nguoni Kwa kuwa tu yeye ni mtoto Wa Waziri. Hajali Hata vyombo vya Dola.

Kauli za Chawene ni za dharau.
Wanamdharau sana Dr. mama.

Unazuia Mikutano ya Hadhara Kama kuna uchaguzi Wa huru na haki. Uchaguzi ukiwa Wa huru na haki hata wanaotaka mikutano ya Hadhara wataona aibu baadae ya uchaguzi kuisha.
 
Waziri wa Nchi, Sera na Uratibu wa Bunge Simbachawene, ni miongoni mwa Mawaziri wa Serikali ya CCM ambaye anaonekana dhahiri kwamba hajaridhishwa na uamuzi wa kuondolewa kwa zuio batili la mikutano ya vyama vya siasa.

Amenukuliwa leo akitetea uamuzi ule wa kidikteta uliojaa uoga na ushamba kwamba ulikuwa halali kwa wakati ule, kwa vile serikali halali iliyochaguliwa na wananchi ilihitaji utulivu ili ilete maendeleo, kwake Simbachawene kuvunja Katiba ndio kuleta maendeleo, huyu ni Waziri, kwamba sasa hivi hawahitaji huo utulivu ili kuleta maendeleo?

Viongozi wanafiki na wanaotetea uovu kama huyu Simbachawene hawastahili kuwemo kwenye serikali za kileo, kwani ilikuwa lazima aropoke huo ujinga wake? Ni dhahiri kwamba huyu hajaridhishwa na uamuzi wa Rais, ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama chake, NASHAURI AVULIWE UWAZIRI HARAKA.

Nakala: Abdulrahman Kinana
View attachment 2469961
Simbachawene ni timu Magufuri
 
Back
Top Bottom