Simbachawene atetea uamuzi wa kuzuia mikutano ya hadhara. Avuliwe Uwaziri!

Simbachawene atetea uamuzi wa kuzuia mikutano ya hadhara. Avuliwe Uwaziri!

"Kwa wakati ule!" Siyo sasa.. Pia, ndiyo maana hata sasa ktk kujenga nchi vyama vimekubali kufanya siasa za kistaarabu. #Kwa sasa twende mbele kutekeleza maelekezo ya mkuu wetu wa nchi, Mhe. Rais Dk. Samia.[emoji120][emoji120][emoji120]
Siasa za kistaarabu ndio siasa gani ? kwamba tukiwa jukwaani tuvae vizuri au ikoje hiyo ?
 
Hivyo vichwa vya train tu haijakaa Sawa, bado malipo ya mkandarasi wa Umeme kule Chini kule!! Halafu waseme hayapo!! Labda nchi iitwe jina lingine na waje watu wengine kabisa kabisa
Usimuamshe aliyelala
 
Kiuhalisia kila mteule wa Rais ni msaidizi wake. Mteuliwa anakuwa msaidizi wa Rais katika yale ambayo Rais anataka kuyatekeleza. Wala haitegemewi aliyeteuliwa kumsaidia aliyemteua awe kinyume na yule aliyemteua katika yale ambayo aliyemteua alitaka amsaidie, japo yawezekana akamshauri huyo boss wake namna bora ya kutekeleza yale ambayo aliyemteua anataka kuyafanya.

Rais pale anapokosea, ni haki kukosolewa na wananchi wake, lakini haki hiyo haipo kwa walioteuliwa kumsaidia Rais. Wao nafasi yao ipo katika kumshauri. Endapo aliyeteuliwa hakubaliani na yale ambaye aliyemteua anayafanya, na ushauri wake umekataliwa, nafasi aliyo nayo aliyeteuliwa aliyo nayo ni kujiuzulu. Akishajiuzulu, haki yake ya kukosoa na kushauri itamrudia aliyekuwa mteuliwa, sawa na sisi tusjo wateule wa Rais katika nafasi yoyote.

Rais Samia hivi karibuni wakati akitoa kauli ya kuruhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, alitamka kuwa mikutano ya vyama vya siasa, ni ruksa kuendelea kama katiba inavyoelekeza. Kwa maneno mengine, ni kuwa Rais alitaka kusema kuwa uzuiaji wa mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa uliokuwa umefanywa na Rais Magufuli lilikuwa ni kosa kwa sababu ilikuwa kinyume cha maelekezo ya katiba ya nchi.

Baada ya kauli ile ya Rais, ilitarajiwa wasaidizi wake wote wamsaidie Rais katika kulinda tangazo lake ambalo ni takwa la katiba ya nchi.

Simbachawene kujitokeza hadharanai na kutamka kuwa uzuiaji wa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa kulikofanywa na Rais Magufuli ulikuwa ni sahihi kwa wakati ule kwa sababu Serikali iliyoundwa inahitaji utulivu ili kutekeleza majukumu yake, ni dhihaka, iliyokusudiwa kupelekwa kwa Rais Samia kwambia kuwa yeye Simbachawene hakubaliani na maamuzi ya Rais, na kwamba kile alichokimaanisha Rais kuwa uzuiaji wa mikutano ya siasa kwa vyama vya siasa uliofanywa na awamu ya 5 ulikuwa kinyume cha katiba, yeye hakubaliani na hiyo kauli.

Simbachawene kama raia ana haki kutoa maoni yake, lakini hana haki ya kumkosoa boss wake ambaye anamtegemea amsaidie kutekeleza maamuzi aliyoyafanya. Simbachawene alistahili kujiuzulu kwanza kabla ya kumkosoa Rais. Kwa sababu amemkosoa boss wake katika kitu ambacho anastahili kusaidia utekelezaji wake, ni lazima aondolewe kwa sababu hatakuwa na msaada, na anaweza kuwa kikwazo katika utekelezaji wa maamuzi ya Rais.
 
Viongozi waache kuongea kwa kutumia ndimi mbili.

Wanawaahidi wadau wa maendeleo wa ulaya, marekani ya kaskazini na hata sisi raia wa Tanzania kwa kuridhia mikataba ya kuhakikisha mazingira huru ya kisiasa, uhuru wa vyombo vya habari, haki za binadamu, katiba mpya n.k

Ahadi hizo juu ktk ujumla wake ndiyo msingi wa jamii kuleta maendeleo kwa watu, mtu mmoja mmoja, kuvutia uwekezaji wa kutoka ndani na nje n.k kwa kulindwa na serikali yenye watendaji wenye kuamini na kuzingatia sheria na katiba.

Toka Geneva
23 March 2022

AHADI ZA MH. GEORGE SIMBACHAWENE MBELE YA JUMUIYA YA KIMATAIFA
Awamu ya 6 ya serikali ya CCM, mmesaini mikataba mingi ya kukubali kufungua milango ya demokrasia, uhuru, haki ya kukusanyika n.k bila kusahau katiba yetu inaruhusu shughulu za kisiasa. Sasa huku kubabaika kunatoka wapi

NGOJA TUKUMBUSHANE
Serikali na vyombo vyake ikiwemo taasisi, idara zake zifahamu kuwa mwaka huu 2022 huko Uswisi (Switzerland) waziri wa Sheria na Katiba Mh. George Simbachawene mbele ya Umoja wa Mataifa katika Kamisheni ya Umoja wa Mataifa Kuhusu Haki za Binadamu kuwa Tanzania iliridhia kuacha kukandamiza na kubinya haki za msingi nyingi ikiwemo hili la wananchi kuwa na haki kujadili, kushauri na kuelekeza nchi yao iende vipi.

23 March 2022
Geneva, Switzerland

Mikataba 252 ambayo Tanzania iliridhia na inayogusa haki zote ikiwemo UWAZI ni kama ifuatayo

Video : Mh. George Simbachawene akihutubia UMoja wa Mataifa kuhusu haki haki na kuuhakikishia ulimwengu kuwa haki zote ktk awamu ya 6 zinazingatiwa



Tanzania yaridhia haki ya wananchi kushirikishwa katika ngazi zote, kujadili mustakhabali wa nchi yao, haki ya jumuika, haki ya kuzungumza, wananchi kuwa na haki ya kuwaambia watawala nini wakifanye, uhuru wa habari, kufunguliwa vya vyombo vya online pia magazeti, imeridhia mikutano ya vyama vya siasa kufanyika.

GEORGE B. SIMBACHAWENE, Minister of Constitutional and Legal Affairs of Tanzania, said Tanzania was a strong proponent of the Universal Periodic Review mechanism which brought together State actors, civil society and development partners. As the Government pursued the goal of realisation of human rights for all Tanzanians, the recommendations were given the highest consideration. All 252 recommendations were disseminated to State and non-State actors, including the National Human Rights Institution as well as civil society, in both mainland Tanzania and Zanzibar. As a result of broad-based consultations, Tanzania had accepted to implement 167 recommendations, which were in compliance with the Constitution of the United Republic of Tanzania and the Constitution of Zanzibar.

The recommendations aligned with policies, laws and programmes which called for the promotion and protection of civil, political, economic, social and cultural rights, emerging human rights issues, anti-corruption efforts, environmental conservation and development priorities of Tanzania. The Government affirmed its commitment to implementing all the accepted recommendations, which had been deemed strategic and effective interventions for the promotion and protection of human rights. 65 recommendations had been noted; those were recommendations that were not in alignment with the Constitutions, policies, laws, traditions, beliefs and culture of Tanzania, or which required further consultations before making a conclusive decision. The Government strived to ensure that all Tanzanians were provided with equal civil, political, economic, social and cultural human rights.

Discussion

Speakers applauded the Government of Tanzania for progress made in strengthening its institutional frameworks for the promotion and protection of rights and fundamental freedoms. Strides had been made in the area of social development, including the introduction of fee-free primary education and remote learning during the COVID-19 pandemic. Speakers further commended Tanzania on the establishment of the National Commission for Human Rights, which was in accordance with the Paris Principles. Speakers noted steps taken to curb child labour, as well as the measures taken by the Government toward ensuring freedom of expression and the right to information, which included entering into dialogue with media practitioners and amending some pieces of legislation. Tanzania’s acceptance of close to 75 percent of the recommendations showed real commitment to further promoting and protect the rights of all persons on its territory. The acceptance of recommendations prioritised expenditures in health including specialised care and services for people living with albinism, as well as scaling up investment in education.

Other speakers took note of the challenges faced by Tanzania in implementing some of its human rights obligations under Article 12(3) of the African Charter which recognized the right to seek and obtain asylum in other countries, as well as the 1951 Convention relating to the Status of Refugees. Speakers regretted that Tanzania did not receive any recommendations on the rights of sex workers, urging the Government to repeal the Penal Code provisions criminalising acts associated with sex work, place a moratorium on the arrest and harassment of sex workers under vagrancy laws, and revise and harmonise national legislation in line with regional and international human rights instruments. Tanzanian authorities continued to weaponise the law to target the opposition and critical voices, using non-bailable offence provisions under the Criminal Procedure Act to detain people for unreasonable periods of time. The State should ensure accountability for election-related human rights violations and guarantee post-election human rights reforms to reverse the Government’s increasing repression and crackdown on civic space.

The Vice-President of the Council informed that out of 252 recommendations received, 167 enjoyed the support of Tanzania, while 65 had been noted. Additional clarification was provided on 20 recommendations, indicating which parts of the recommendations were supported and which parts were noted

Concluding Remarks

GEORGE B. SIMBACHAWENE, Minister of Constitutional and Legal Affairs of Tanzania, said Tanzania continued to accord great significance to the Universal Periodic Review, as it played a key role in the promotion and protection of human rights in the country. Tanzania was committed to implementing the accepted recommendations, as they would have a direct impact on the realisation of human rights and sustainable development of the country. The Universal Periodic Review was a continuous process, and the Government would continue to address the remaining challenges through dialogue, in collaboration with all stakeholders. It would also continue to strengthen its internal mechanisms and promote engagement with all non-State actors and development partners. The Government, under the stewardship of Tanzania’s first female President, would meet the aspirations and objectives of the Universal Periodic Review mechanism during the coming fourth cycle.

Link: Conseil des droits de l’homme : Examen périodique

https://www.ungeneva.org › 2022/03
Human Rights Council Adopts Outcomes of Universal Periodic ...

23 Mar 2022 — 23 March 2022 Meeting Summaries. The Human Rights Council in a midday meeting adopted the outcomes of the Universal Periodic ....
 
Siasa za kistaarabu ndio siasa gani ? kwamba tukiwa jukwaani tuvae vizuri au ikoje hiyo ?
Kuvaa vizuri pia ni ustaarabu ndugu yangu. Unawezaje kuwa kiongozi halafu unavaa kihunihuni? 😀😀😀
 
Ujinga mtupu!kila zama na mambo yake,akishasema haikuwa sahihi ili iweje?kwamba wapewe muda ambao hakutumia?maisha yanaenda mbele,vyama vya siasa vilikuwepo kuanzia miaka ya 40 Huko lakini vikafutwa miaka 60 mpaka 90 je unataka turudi nyuma kuanza kuulizana?
 
Uongo utakusaidia nini Aisee ?
Mkuu hapo kuna uongo upi?
hamkukataa tozo?
hakukupinga bwawa la umeme?
hamkususia mchakato wa katiba?
hampingi maendeleo?
hampewi mafunzo na CDU na KAS?
hampeleki hela Bunge la Ulaya ili Tanzania isemwe vibaya?
hampingi serikali kukopa?
Mkuu nambie hapo uongo ni upi?
 
Ni wazi Simbachawene hajafurahishwa na haya maamuzi.
443022DF-C6D5-4803-B50B-A9F2C26F8258.jpeg
 
mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani hasa chadema hawana jipya la kusema ila hotuba yao sehemu nyingi itakuwa ni kumkashifu jpm
 
Ni wengi walioumia, sasa ule ubunge wa mbeleko kwishnei, tutachagua kulingana na Sera.
Pia ruhusa ya mikutano itatufanya tuwaone wabunge wetu huku mikoani, upinzani ukiliamsha dude, wabunge lazima watapita pita majimboni.
Asante Samia.
Tokea upinzani uhanzishwe haujawahi kuwa na nguvu pale Dodoma, hivyo hakina Simbachawene bado wapo sana.
 
Kwa kelele hizi utadhani irrelevance ya vyama vya siasa vya upinzani ilisababishwa na zuio la Magufuli. Magufuli alichofanya kwa muda mfupi ni kutuonyesha rangi halisi za wanasiasa. Wawe wa upinzani, wawe wa CCM.

Mtu ka Lissu hivi hata baada ya kuruhusu mikutano ya hadhara ni kitu gani atasema ili watu tumchukulie serious?
Mkuu kumbe hata wewe ni mtu wa kuchukuliwa seriously?
😆😆😆😆
 
Back
Top Bottom