Simbachawene atetea uamuzi wa kuzuia mikutano ya hadhara. Avuliwe Uwaziri!

Amezingua

Simbachawene bado anamuwaza mZiLaNkeNdE

Hawa ndio wanaotetea legacy katili yake.

Jamaa ni sukuma gang Nini!?
 
Mkuu mbona kama una chuki binafsi na Simbachawene hivi, au kuna mtu anakutumia kumchafua mzee wa watu?. Tambua ya kwamba hata akitumbuliwa hauwezi kuteuliwa wewe kushika huo wadhifa wake.
Pambania mkate wako wa kila siku acha kuwachafulia watu vibarua vyao hiyo ni dalili ya roho mbaya

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
Labda kama anajichafua mwenyewe , video umewekewa pale bado nayo huiamini ?
 
Labda huko kwenu, huku kwetu watu hawaangalii chama....tena ukitaja CCM ndo hawaelewi, Kwa mara ya kwanza tangu nipate akili diwani wa CCM alishinda kupitia ule uchafuzi wa 2022, ubunge alinyimwa Azan na mipesa yake akashinda wa CUF....Ila Yule nyooko alikuja kuunga mkono juhudi 🤣
Ndio nakwambia mkuu Tanzania hii watu hawachagui kwa sera, kuna kuangalia chama(ccm au upinzani) kuna umaarufu wa mtu yeye mwenyewe na mwishoni hela pia inaweza kukufanya ukachaguliwa ila sio sera. Yani wewe sio maarufu kisha uende kugombea kupitia chama kisicho na wanachama wengi yani sio chama maarufu na hela hauna unategemea sera tu...Aisee!
 
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Waziri wa Nchi, Sera na Uratibu wa Bunge Simbachawene, ni miongoni mwa Mawaziri wa Serikali ya CCM ambaye anaonekana dhahiri kwamba hajaridhishwa na uamuzi wa kuondolewa kwa zuio batili la mikutano ya vyama vya siasa.

Amenukuliwa leo akitetea uamuzi ule wa kidikteta uliojaa uoga na ushamba kwamba ulikuwa halali kwa wakati ule, kwa vile serikali halali iliyochaguliwa na wananchi ilihitaji utulivu ili ilete maendeleo, kwake Simbachawene kuvunja Katiba ndio kuleta maendeleo, huyu ni Waziri, kwamba sasa hivi hawahitaji huo utulivu ili kuleta maendeleo?

Viongozi wanafiki na wanaotetea uovu kama huyu Simbachawene hawastahili kuwemo kwenye serikali za kileo, kwani ilikuwa lazima aropoke huo ujinga wake? Ni dhahiri kwamba huyu hajaridhishwa na uamuzi wa Rais, ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama chake, NASHAURI AVULIWE UWAZIRI HARAKA.

Nakala: Abdulrahman Kinana
View attachment 2469961

Hawezi kuvuliwa!
 
Hiki kichwa ni chakuliwa haraka sana!
Simbachawene kasema upinzani wa kistaarabu bi wa facts, suyo matusi. Mfano pekee wa aina hii ni dhana ya mafisadi aliyokuwa anaiibua Dr Slaa wa CHADEMA, ndipo ikajizolea sifa rufufu. Uchoyo na ubinafsi wa Viongozi wa CHADEMA, na uchu wa hela na uchu wa madaraka, sera ya mafisadi wakaiya stone dead pale walipopokea hela za fisadi mkuu Lowassa awe ndiyo mgombea wa CHADEMA wakaanza kumnadi fisadi nchi nzima kwa helicopter. Dr Slaa akajiuzulu, CHADEMA ikashindwa, na Lowassa akarudi CCM. Tangu pale CHADEMA si CHADEMA tena. Utamwamini Mbowe aliyepokea hela? Utamwamini Tundu Lissu aliyemnadi fisadi Lowassa nchi nzima? Kwa hoja ipi?
 
Kuruhusiwa Mikutano ya Hadhara hakumaanishi, kuruhusiwa kuropoka, au ni sawa kuendeleza dhuluma, dhihaki na yanayo fanana nayo.

Sishangai, nina butwaa.

Unaweza eleweka tu bila ya kutoa kejeli-ndio michango ya kuleta Taharuki majukwaani.

I dare any politician kupanda Jukwaani na Kumdhihaki Hayati Raisi. Hata kwa Vijembe...kwani Yumo moyoni mwa watu wengi- Friends and Foes

Humu tuendelee na haya haya,(dhihaki, kejeli, matusi;na yote yahusishwayo na dhuluma) lakini kiuhalisia.... Kibuyu cha Asali kinanywewa. Kitaendelea Kunywewa tukiendelea na mtindo huu.

Amani iwafikie.
Kete kubwa kwenye mikutano itakuwa ni kumponda na kumkejeli Jiwe kwa jinsi alivyokandamiza demokrasia, alivyoua na kuteka watu hasa aliotofautiana nao ki mitazamo, alivyopora mali za watu and the list is endless.
Baada ya hapo tuone nyie aliye kwenye mioyo yenu reactions zenu zitakuwaje, huu mchiriku wa eti asisemwe ndiyo unazidi kuongeza dhamira ya watu kumsema.
Mliobwia asali enzi za Jiwe waacheni wenzenu nao wabwie, kutesa kwa zamu.
 
Mkuu mbona kama una chuki binafsi na Simbachawene hivi, au kuna mtu anakutumia kumchafua mzee wa watu?. Tambua ya kwamba hata akitumbuliwa hauwezi kuteuliwa wewe kushika huo wadhifa wake.
Pambania mkate wako wa kila siku acha kuwachafulia watu vibarua vyao hiyo ni dalili ya roho mbaya

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
Kalikoroga mwenyewe huyo, it's not personal bali haya yote ni matokeo ya kauli zake.
Kwa kifupi anavuna alichopanda.
 
Kete kubwa kwenye mikutano itakuwa ni kumponda na kumkejeli Jiwe kwa jinsi alivyokandamiza demokrasia, alivyoua na kuteka watu hasa aliotofautiana nao ki mitazamo, alivyopora mali za watu and the list is endless.
Baada ya hapo tuone nyie aliye kwenye mioyo yenu reactions zenu zitakuwaje, huu mchiriku wa eti asisemwe ndiyo unazidi kuongeza dhamira ya watu kumsema.
Mliobwia asali enzi za Jiwe waacheni wenzenu nao wabwie, kutesa kwa zamu.
Kawadanganye wengine.... Kawadanganye ...Wazungu, Waarabu, Wahindi na Neanderthral wengine...

Hata hivyo sidhani kama wanaamini Uongo na Propaganda hasi inayoelekezwa kwa Hayati Raisi. Wanakusoma.

. Hii ni Tanzania. Jamhuri ya Muungano wa Watanzania na sio ya Maharamia.

Mtateseka sana....ngoja niende Kimara.
 
Simbachawene kasema upinzani wa kistaarabu bi wa facts, suyo matusi. Mfano pekee wa aina hii ni dhana ya mafisadi aliyokuwa anaiibua Dr Slaa wa CHADEMA, ndipo ikajizolea sifa rufufu. Uchoyo na ubinafsi wa Viongozi wa CHADEMA, na uchu wa hela na uchu wa madaraka, sera ya mafisadi wakaiya stone dead pale walipopokea hela za fisadi mkuu Lowassa awe ndiyo mgombea wa CHADEMA wakaanza kumnadi fisadi nchi nzima kwa helicopter. Dr Slaa akajiuzulu, CHADEMA ikashindwa, na Lowassa akarudi CCM. Tangu pale CHADEMA si CHADEMA tena. Utamwamini Mbowe aliyepokea hela? Utamwamini Tundu Lissu aliyemnadi fisadi Lowassa nchi nzima? Kwa hoja ipi?
Unaweza kutuwekea hapa kiasi ambacho Mbowe alipokea kutoka kwa Lowassa ?
 
Waziri wa Nchi, Sera na Uratibu wa Bunge Simbachawene, ni miongoni mwa Mawaziri wa Serikali ya CCM ambaye anaonekana dhahiri kwamba hajaridhishwa na uamuzi wa kuondolewa kwa zuio batili la mikutano ya vyama vya siasa.

Amenukuliwa leo akitetea uamuzi ule wa kidikteta uliojaa uoga na ushamba kwamba ulikuwa halali kwa wakati ule, kwa vile serikali halali iliyochaguliwa na wananchi ilihitaji utulivu ili ilete maendeleo, kwake Simbachawene kuvunja Katiba ndio kuleta maendeleo, huyu ni Waziri, kwamba sasa hivi hawahitaji huo utulivu ili kuleta maendeleo?

Viongozi wanafiki na wanaotetea uovu kama huyu Simbachawene hawastahili kuwemo kwenye serikali za kileo, kwani ilikuwa lazima aropoke huo ujinga wake? Ni dhahiri kwamba huyu hajaridhishwa na uamuzi wa Rais, ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama chake, NASHAURI AVULIWE UWAZIRI HARAKA.

Nakala: Abdulrahman Kinana
View attachment 2469961
Hajitambui huyo mhawiii
 
Back
Top Bottom