Simbachawene awataka viongozi wa walimu wasiokuwa na ajira NETO kufika ofinini Dodoma kwa mazungumzo

Ishu ya ajira, haitatuliwi kwa vikao vya kisiasa, ccm hawana majibu, hatuna shule za kuchukua hawa waalimu wote, waambiwe ukweli! Kwa, elimu ya ualimu,nchi hainauwezo wa kuwapa ajira ya kufundisha! Period.
Waambiwe ukweli kwamba mpaka sasa bado hilo hawalitambui!!! Basi elimu haijawakomboa.
 
We ni mbishi eeh? Kubali yaishe mwana
Hamna mkuu. Point yangu ni kwamba chamsingi mkono uende kinywani haijalishi kwa kazi uliyoisomea au ambayo hujaisomea ili mradi nyumbani baba na mama wanakula.
 
W
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene, amewaita ofisini kwake Dodoma kwa mazungumzo viongozi wa vijana waliojitambulisha kwenye andiko lao kuwa ni “Non Employed Teachers Organisation (NETO)” wenye umoja wao kupitia mitandao ya Kijamii.

“Nimesoma makala yao yenye kichwa cha habari "Ombi la Wahitimu wa Ualimu Vyuo mbalimbali Nchini kati ya mwaka 2015-2023 kwa Serikali, andiko lao ni zuri na linaeleweka ingawa linahitaji ufafanuzi zaidi, hivyo ninatoa wito kwa vijana hao kuja ofisini Dodoma kwa mazungumzo”

Pia soma: Walimu Wasio na Ajira (NETO) wanaongea na waandishi wa habari kuondoa dukuduku lao

View attachment 3246235
Akienda tu watajuta kuzaliwa
 
Hamna la kuwasaidia bana serikali haiwezi kuajiri walimu wote waliopo mtaani bana.
 
Anayesomea upadre ama uchungaji sijasikia akishauriwa kufanya kazi nyingine ama kujiajiri nje ya mimbari za madhabahu!

Pia sijasikia kijana akaenda chuo cha Polisi ama depot ya jeshi kufanya mafunzo kisha akasubirishwa ajira akiwa mtaani.

Kozi za ualimu na nyingine zenye kufanana na hizo ni sawa na mazao ya biashara kwa mkulima: pamba au tumbaku, yakivunwa lazima yauzwe na yakikosa soko lazima Serikali ilaumiwe kwa kutokutimiza wajibu wake.
Umenena vyema mkuu.
 
Umeongea kwa ukali Sana. Wazo langu kwao....kama wako laki tano (mfano tu)
500,000 x Tsh.10,000@=5,000,000,000 yaani Tsh. Bilioni Tano. Watafute namna ya kujiajiri. Ni hayo tu.
Hizo huwa zinaishia kwenye goli la mama na kuwaonga wasanii na wachungaji.
 
Hamna la kuwasaidia bana serikali haiwezi kuajiri walimu wote waliopo mtaani bana.
Ni kweli haiwezi kulingana na aina ya watu wanaotuongoza akina mkenda wanaojali familia zao na maslahi Yao pekee. Je kwanini wasiajiri Kwa kuangalia miaka ya kuhitimu mfano kama mtu kamaliza 2015 ataanza kuajiriwa baadae afuate wa 2016 hatimae 2017 na kuendelea na si hii mtu kamaliza 2024 anakuwa anashindanishwa sawa na aliyemaliza 2015/2016. Hiki ndiyo kinachoumiza na kuathiri wahitimu Hadi wanaanza kuwa na chuki na serikali.
 
Hili washaambiwa sana na sio kwenye Elimu tu kada zote iwe First in first out lakini serikali haielewi inawaita wote inawapa mtihani wa 2024 anapass kwakuwa n fresh madesa bado yapo kichwan wa 2015 anaachwa.
 
Walimu tafuteni shughuli za kufanya kila siku kelele tu aaarg!
Kwanza uelewe mi si mwalimu, hata hivyo pilipili usisozila zakuwashia nini, kuajiriwa ni haki yao, badala tuwasapoti tunawatukana? Mbona tuna roho za kichawi hivi?
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene, amewaita ofisini kwake Dodoma kwa mazungumzo viongozi wa vijana waliojitambulisha kwenye andiko lao kuwa ni “Non Employed Teachers Organisation (NETO)” wenye umoja wao kupitia mitandao ya Kijamii.

“Nimesoma makala yao yenye kichwa cha habari "Ombi la Wahitimu wa Ualimu Vyuo mbalimbali Nchini kati ya mwaka 2015-2023 kwa Serikali, andiko lao ni zuri na linaeleweka ingawa linahitaji ufafanuzi zaidi, hivyo ninatoa wito kwa vijana hao kuja ofisini Dodoma kwa mazungumzo”

Pia soma: Walimu Wasio na Ajira (NETO) wanaongea na waandishi wa habari kuondoa dukuduku lao

View attachment 3246235
Watu hawana ajira unawaita Dodoma watafikaje?

Atume nauli au ticket za Sgr go and return kwa viongozi na awaandalie huduma za kula na kulala wakiwa Dodoma.
 
Back
Top Bottom