Simbachawene: Kupata kitambulisho cha NIDA siyo mwarobaini wa kutokuulizwa uraia wako

Simbachawene: Kupata kitambulisho cha NIDA siyo mwarobaini wa kutokuulizwa uraia wako

Waziri anamaanisha kuna wazamiaji ambao wanaweza kuwahonga wafanyakazi wa NIDA ambao sio waaminifu na kuwapa hivyo vitambulisho! Kwa hiyo ikigundulika Kama ulifanya udanganyifu utanyanganywa kitambulisho na hataua za kisheria dhidi yako zitachukuliwa pamoja na hao waliokupa hicho kitambulisho nao watawajibika!!
mbona wewe unaakili kubwa ya kuchambua kuliko waziri mwenyedhamana? Ameshindwaje sema hivi km kweli ni hivi of which maelezo yako makes total sense of it according to me.
Anyways waweza sema msomi Yule kumbe ni Sawa n'a std7 maana huko chuo labda alikua mla chabo na vibuti mpaka anamaliza degree.
 
Hakika Tanzania tuna viongozi wa ajabu sana.

Sasa kama anayajua hayo ilikuwaje taifa likaingia hasara ya mabilion kwa kuandaa na kusambaza hivyo vitambulisho?
Mimi nafikiri waziri anatakiwa kujua kwamba hicho kitambulisho cha Taifa kupatikana kwake kulifuta misingi ya kiraia mfano mzaliwa wa Tanzania ,Uraia wa kujiandikisha kama hao wakimbizi ambao walikana uraia wao na kusajiliwa kama raia wa Tanzania ,sasa anaposema hata wakimbizi wanayo hicho kitambulisho anamaanisha nini???hao siyo wakimbizi tena bali ni raia wa Tanzania ..Jitahidi kuwa smart Mheshimiwa Waziri ......
 
Hajui tofautisha Alien ID na Citizen ID
 
Simbachawene umekosea Nchi yeyote Duniani ukiweza kupata hiyo card yao ya uraia ni raia ujue angalia matatizo yapo wapi na si kuja kutamka hayo maneno ungekua kwenye nchi wanazohoji kwa kauli hiyo leo usingekua Waziri...
 
"Tumepata Waziri wa Ajabu kweli kweli". (kwa sauti ya TAL)
 
Mimi nafikiri waziri anatakiwa kujua kwamba hicho kitambulisho cha Taifa kupatikana kwake kulifuta misingi ya kiraia mfano mzaliwa wa Tanzania ,Uraia wa kujiandikisha kama hao wakimbizi ambao walikana uraia wao na kusajiliwa kama raia wa Tanzania ,sasa anaposema hata wakimbizi wanayo hicho kitambulisho anamaanisha nini???hao siyo wakimbizi tena bali ni raia wa Tanzania ..Jitahidi kuwa smart Mheshimiwa Waziri ......
Upo sahihi ndugu yetu
 
Hivi vitambulisho hadi wengine tumeshavisahau maana tangu mwaka juzi mwezi wa 10 nijiandikishe hakijatengenezwa mpaka leo zaidi ya kupewa namba.

Na hivyo kinaisha muda nafikiri nitakipata zikiwa zimebaki siku kadhaa kiwe takataka
 
Hakika Tanzania tuna viongozi wa ajabu sana.

Sasa kama anayajua hayo ilikuwaje taifa likaingia hasara ya mabilion kwa kuandaa na kusambaza hivyo vitambulisho?
Wengi wa hao wanaoitwa viongozi ni wagonjwa wa akili. Kiongozi mwenye akili timamu hawezi kutoa tamko la kipumbavu kama hilo akaendelea kubaki hapo alipo.
 
Wengi wa hao wanaoitwa viongozi ni wagonjwa wa akili. Kiongozi mwenye akili timamu hawezi kutoa tamko la kipumbavu kama hilo akaendelea kubaki hapo alipo.
Inasikitisha sana na bado naamini mama Samia atafikiria mara ya pili juu ya huyu waziri
 
Hivi vitambulisho hadi wengine tumeshavisahau maana tangu mwaka juzi mwezi wa 10 nijiandikishe hakijatengenezwa mpaka leo zaidi ya kupewa namba.

Na hivyo kinaisha muda nafikiri nitakipata zikiwa zimebaki siku kadhaa kiwe takataka
Inaomekana huu ulikuwa ni mpango wa awamu ya 5 kupigia noti
 
This guy must be stupid, hata kama ni kweli hakutakiwa kusema hivyo hadharani. Muulize Passport ninini na ili upate passport lazima uwe na NIDA ID. Lol
Kauli ya kipumbavu kabisa kutoka kwa mtu kama waziri wa mambo ya ndani. Sasa faida kitambulisho nini na gharama zote hizi kutengeneza vitambulisho fake? nchi zote duniani wanatoa vitambulisho vya uraia na kuna vya wageni na vinaandikwa wazi huyu mwananchi na huyu ni mkaaji tu. Nadhani wanaingiza siasa wanamwinda mtu huwezi kuweka sheria juu ya sheria. Sasa atuambie raia ni nani labda ni yeye tu na mgogo mwenzake Ndungai. jinga kubwa hili konda la bus.
 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene ameeleza kuwa kuwa na kitambulisho cha Utaifa (NIDA), hakuhalalishi mtu kuwa ni Raia wa Tanzania.

Pia soma > Mbunge :Wasiojua vema mashairi ya wimbo wa Taifa na Kiswahili wanaambiwa siyo raia wa Tanzania

Simbachawene ameeleza hayo leo Mei 4, Bungeni jijini Dodoma ambapo amesema kuwa Uraia wa Tanzania una Sheria yake ya Uraia na una mchakato wake hivyo kitambulisho hicho ni kwa ajili ya kuwatambua tu hutolewa hata kwa Wakimbizi na hata kwa Wahamiaji wakazi.

“Kwa sasa tunadhani pengine tukipata Vitambulisho vya Taifa ndio tumepata Uraia wa Tanzania, Uraia wa Tanzania una Sheria yake ya Uraia na una mchakato wake, kitambulisho hiki ni kuwatambua tu na vitambulisho hivi vinatolewa hata kwa Wakimbizi, vinatolewa hata kwa Wahamiaji wakazi,” amesema Simbachawene.

Simbachawene amesema mtu kupata kitambulisho hicho sio mwarobaini wa kutokuulizwa na iwapo itagundulika kuwa mtu sio raia basi atanyang’anywa kitambulisho hicho.

“Ukipata kitambulisho hiki sio mwarobaini kwamba wewe umeshamaliza sasa hutaulizwa hapana, utaulizwa na utanyang’anywa hicho kitambulisho kama tukigundua wewe sio Raia wa Tanzania” amesema Simbachawene.

Naamini baada ya kuutangaza ujinga kuwa ni adui, ujinga umejiongeza na kukaa ndani ya watu. Hapa ujinga umejitokeza kutoka kwa mwenye mamlaka ya uwaziri
 
Back
Top Bottom