Simbachawene: Kupata kitambulisho cha NIDA siyo mwarobaini wa kutokuulizwa uraia wako

Simbachawene: Kupata kitambulisho cha NIDA siyo mwarobaini wa kutokuulizwa uraia wako

Mtu asikufananishe na Mgogo. Yaani majibu yake, hayatofautiani na majibu ya Ndugai. Hawa jamaa walizowea kukaa barbarani kuomba. Sio kupewa nafasi za utawala.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene ameeleza kuwa kuwa na kitambulisho cha Utaifa (NIDA), hakuhalalishi mtu kuwa ni Raia wa Tanzania.

Pia soma > Mbunge :Wasiojua vema mashairi ya wimbo wa Taifa na Kiswahili wanaambiwa siyo raia wa Tanzania

Simbachawene ameeleza hayo leo Mei 4, Bungeni jijini Dodoma ambapo amesema kuwa Uraia wa Tanzania una Sheria yake ya Uraia na una mchakato wake hivyo kitambulisho hicho ni kwa ajili ya kuwatambua tu hutolewa hata kwa Wakimbizi na hata kwa Wahamiaji wakazi.

“Kwa sasa tunadhani pengine tukipata Vitambulisho vya Taifa ndio tumepata Uraia wa Tanzania, Uraia wa Tanzania una Sheria yake ya Uraia na una mchakato wake, kitambulisho hiki ni kuwatambua tu na vitambulisho hivi vinatolewa hata kwa Wakimbizi, vinatolewa hata kwa Wahamiaji wakazi,” amesema Simbachawene.

Simbachawene amesema mtu kupata kitambulisho hicho sio mwarobaini wa kutokuulizwa na iwapo itagundulika kuwa mtu sio raia basi atanyang’anywa kitambulisho hicho.

“Ukipata kitambulisho hiki sio mwarobaini kwamba wewe umeshamaliza sasa hutaulizwa hapana, utaulizwa na utanyang’anywa hicho kitambulisho kama tukigundua wewe sio Raia wa Tanzania” amesema Simbachawene.
Mtu kama huyu aliwezaje kupata ubunge na baadae uwaziri?
 
Simbachawene ni "MZIGO" Mh. Mama Samia Suluhu Hassan angalia sana.

Kwamba vitambulisho vya NIDA wanapewa Wakimbizi na Wahamiaji Haramu ni AIBU NA FEDHEHA KUBWA kwa Serikali iliyopo MADARAKANI.

GHARAMA ZA KUTENGENEZA VITAMBULISHO VYA NIDA NI HASARA KWA TANZANIA NA WATANZANIA.

SIMBACHAWENE "JIUZULU " UMESHINDWA KUTETEA MATUMIZI YA SERIKALI.
 
Simbachawene anataka kusema nini in a nutshell?

Kwamba hizi "CITIZEN IDENTIFICATION CARDs" sasa zinatolewa mpaka kwa wahamiaji haramu kwa sababu Wizara yake imejaa watu wazembe, wasiojari na wala rushwa wakubwa kiasi cha kutoa vitambulisho kihohela?
Kwa nchi za wenzetu Simbachawene angepaswa kujiuzulu leo leo. Huo ni UPUMBAVU wa hali ya juu kwa kuwa Tanzania kabla ya vitambulisho vya NIDA ni sawa na Watanzania BAADA ya vitambulisho vya NIDA.

Ni upotevu wa Fedha za walipa Kodi wa Tanzania
 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene ameeleza kuwa kuwa na kitambulisho cha Utaifa (NIDA), hakuhalalishi mtu kuwa ni Raia wa Tanzania.

Pia soma > Mbunge :Wasiojua vema mashairi ya wimbo wa Taifa na Kiswahili wanaambiwa siyo raia wa Tanzania

Simbachawene ameeleza hayo leo Mei 4, Bungeni jijini Dodoma ambapo amesema kuwa Uraia wa Tanzania una Sheria yake ya Uraia na una mchakato wake hivyo kitambulisho hicho ni kwa ajili ya kuwatambua tu hutolewa hata kwa Wakimbizi na hata kwa Wahamiaji wakazi.

“Kwa sasa tunadhani pengine tukipata Vitambulisho vya Taifa ndio tumepata Uraia wa Tanzania, Uraia wa Tanzania una Sheria yake ya Uraia na una mchakato wake, kitambulisho hiki ni kuwatambua tu na vitambulisho hivi vinatolewa hata kwa Wakimbizi, vinatolewa hata kwa Wahamiaji wakazi,” amesema Simbachawene.

Simbachawene amesema mtu kupata kitambulisho hicho sio mwarobaini wa kutokuulizwa na iwapo itagundulika kuwa mtu sio raia basi atanyang’anywa kitambulisho hicho.

“Ukipata kitambulisho hiki sio mwarobaini kwamba wewe umeshamaliza sasa hutaulizwa hapana, utaulizwa na utanyang’anywa hicho kitambulisho kama tukigundua wewe sio Raia wa Tanzania” amesema Simbachawene.

Halafu ye mwenyewe anafanana na wanyarwanda
 
Wagogo nadhani kuna shida kubwa sn, ukianza na Ndugai, Simbachawene + Kabudi yaani hakuna mwenye nafuu hata kidogo
Hivi Kabudi kumbe ni mgogo?
Nilidhani ni Mkaguru
 
Hii nchi inachekesha, kwahiyo kwanza unapewa utambulisho wa uraia halafu ndio uhojiwe uraia wako.
Ni sawa na kumpa mgonjwa panadol halafu ndio umpime kama kichwa kinamuuma. Tanzania tuna safari ndefu sana.
Usikute mradi wenyewe ulikuwa ni dili la kupigia noti tu
 
Waziri anamaanisha kuna wazamiaji ambao wanaweza kuwahonga wafanyakazi wa NIDA ambao sio waaminifu na kuwapa hivyo vitambulisho! Kwa hiyo ikigundulika Kama ulifanya udanganyifu utanyanganywa kitambulisho na hataua za kisheria dhidi yako zitachukuliwa pamoja na hao waliokupa hicho kitambulisho nao watawajibika!!
Wacha kumlisha waziri matango pori yako hapa.
Alichokiongea yeye ndiyo tunakijadili hapa.
 
National Identity Card si ndio NIDA
National ni Taifa
Kwa hivi NIDA ni kitambulisho cha Utaifa
Utaifa ni Uraia au
Nationality ni Utaifa
Citizenship ni Uraia
*** NIDA ilianzishwa kwa lengo gani tuanzie hapa
***Kuna Resident Permit ni Mkaaji ( wakimbizi wageni wahamiaji etc)

Wizara mnajichanganya wenyewe
Huwezi kuwa mkimbizi ukapewa NIDA
Mtoto aliyezaliwa ukimbizini anaweza kuwa NIDA (kama sheria za nchi zinatambua hili kuzaliwa ukimbizini sio lazima uwe na utaifa wa nchi husika)
Simba chawene hajitambui
 
Back
Top Bottom