Simbachawene: Ripoti zinaonesha zaidi ya 40% ya Watumishi wa Umma Tanzania hawafanyi kazi

Simbachawene: Ripoti zinaonesha zaidi ya 40% ya Watumishi wa Umma Tanzania hawafanyi kazi

Shotocan

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2023
Posts
6,650
Reaction score
12,711
Waziri anayehusika na utumishi Simbachawene asema asilimia 40 ya wafanyakazi wa serikali ni mizigo

swali kwa nini hawaachishwi kazi? Wapishe wengine?

Serikali kwa nini inaendelea kuwakumbatia?

-------

3(1).JPG

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesema zaidi ya asilimia 40 ya Watumishi wa Umma hawafanyi kazi licha ya kulipwa mshahara kila mwezi.

Amesema hiyo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni na Tume ya Utumishi wa Umma nchini

Mhe. Simbachawene amesema hayo leo jijini Arusha wakati akifunga Kikao kazi cha tano cha Serikali Mtandao ambapo amesema Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma wanawajibu wa kuhakikisha kila mtumishi anatekeleza majukumu yake ipasavyo.

‘’Watumishi ni lazima wafanye kazi kwani wasipofanya kazi wanakuangusha wewe Mkuu wa Taasisi, lazima tuwe na jamii inayoandaliwa kufanya kazi’’ amesisitiza Mhe. Simbachawene
4.jpeg

5.jpg
Amefafanua kuwa kwa mujibu wa tafiti hiyo, wavivu, wazembe, wagonjwa pamoja na waliosusiwa kutokana na vipaji na uwezo wao ni asilimia 40 ya Watumishi wanaolipwa pasipo kufanya kazi

Amewataka Wakuu hao kuwatumia Watumishi wa Umma wenye vipaji na uwezo badala ya kuwafanyia fitina na hujuma hali inayopelekea kurudisha nyuma maendeleo ya nchi

Amesema hali hiyo imesababisha kutokuwepo kwa urithishanaji wa madaraka jambo ambalo limechangia kudhoofika kwa Taasisi pale kiongozi wa Taasisi anapostaafu au kuhama.

Aidha, Mhe. Simbachawene amesema kumeibuka tabia ya baadhi ya Watendaji wakuu hao pindi Mtumishi mwenye sifa za ziada anapohamia kwenye Taasisi anayoiongoza hupata hofu na kutompangia najukumu kwa hisia kuwa ametumwa kumchunguza a au kuchukua nafasi yake

Ameeleza kuwa tabia hiyo kwenye utumishi wa umma haikubaliki na wale wenye tabia hiyo wajirekebishe haraka kwani Taasisi hizo wanazoziongoza ni za umma na sio mali yao binafsi

Katika hatua nyingine, Kutokana na ongezeko la matumizi ya simu kwa wananchi, Mhe. Simbachawene amezitaka Taasisi za Umma kutoa huduma za kidijitali kutokana na fursa hiyo

Vilevile, Mhe. Simbachawene amezitaka Taasisi za Umma ambazo hazijaanza kutumia mfumo wa kidijitari wa e-Mrejesho ziingie mara moja la sivyo zitachukuliwa hatua kali na Ofisi anayoiongoza.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao, ( e-GA) Mhandisi Benedict Ndomba aliwashukuru washiriki wa kikao hicho cha jumla 1526 ya ushiriki wao ambapo jumla ya mada 18 ziliwasilishwa ikiwa ni pamoja na kujiwekea mikakati ya kukabiliana na changamoto za usalama wa mtandao Serikalini.

Amesema kikao hicho kimejadili changamoto mbalimbali zinazoikabili Serikali Mtandao pamoja na kuweka mikakati madhubuti ya kuchangamkia fursa ya kujifunza teknolojia mpya zinazoibukia ili kuendana na mabadiliko yanayotokea duniani kote.
2.jpeg
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Mhe.Festo Kiswaga ameishukuru e-GA kwa kuendelea kuuamini Mkoa wa Arusha ikiwa ni mara ya tano sasa vikao hivyo vimekuwa vikifanyika Mkoani humo hali iliyopelekea Mkoa huo kuwa wanufaika wakubwa wa kiuchumi pamoja na kuwa wadau namba moja wa matumizi ya Serikali Mtandao.

Naye Katibu Mkuu-IKULU, Bw. Mululi Mahendeka amesema Ofisi yake itasimamia na kufanyia kazi maazimio yote yaliyowasilishwa leo na kuhakikisha utekelezaji wake unawasilishwa katika kikao kijacho

Pia, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya e-GA, Dkt. Jasmine Bunga amesema kikao kazi hicho kimekuwa muhimu kwa washiriki ambapo mbali ya kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili pia wamejiwekea mikakati ya kuendelea kujenga Serikali ya kidigitali.

Amesema lengo ya kujiwekea mikakati hiyo ni kuhakikisha Serikali inapiga hatua kubwa kwenye matumizi ya mifumo ya TEHAMA itakayoleta tija na ufanisi wa hali ya juu katika utoaji wa huduma bora za haraka na za uhakika kwa wananchi.

Pia soma ~ Waziri Simbachawene alikiri 40% ya Wafanyakazi ni Wazembe, Wavivu, incompetents, so kwanini Serikali iendelee kuwabeba?
 
Ukisikia Boss anasema mfanyakazi wake ni mzigo, tambua kuwa Boss ni mzigo x100 zaidi yake.
Wenda halipi mshahara mzuri, mazingira ya kazi siyo mizuri, vitendea kazi hakuna, maombi yao hayatekelezwi kwa wakati.
Simbachawene wewe ni waziri Mzigo hapo UTUMISHI.
 
Waziri anayehusika na utumishi Simbachawene asema asilimia 40 ya wafanyakazi wa serikali ni mizigo

swali kwa nini hawaachishwi kazi? Wapishe wengine?

Serikali kwa nini inaendelea kuwakumbayia?
Hili alishasemaga prof Assad. Prof alisema Asilimia 70 hawana uweledi
 
Waziri anayehusika na utumishi Simbachawene asema asilimia 40 ya wafanyakazi wa serikali ni mizigo

swali kwa nini hawaachishwi kazi? Wapishe wengine?

Serikali kwa nini inaendelea kuwakumbayia?
Je vitendea kazi anawapa?
Masilahi yao wanapata vilivyo?
Kama wapo hao mizigo basi ni kwasababu yake kutotimiza majukumu yake kwahiyo yeye mwenyewe ni mzigo
 
Waziri anatoa mlio sasa raia tuchukue hatu gani kama yeye yuko kwenye nafasi ya watunga sera na wafanya maamuzi
 
Waziri anayehusika na utumishi Simbachawene asema asilimia 40 ya wafanyakazi wa serikali ni mizigo

swali kwa nini hawaachishwi kazi? Wapishe wengine?

Serikali kwa nini inaendelea kuwakumbayia?
Vipi hajaeleza asilimia ya viongozi mzigo au nao ndio wana dondokea kwenye hiyo 40%?
 
Back
Top Bottom