Simbachawene: Ripoti zinaonesha zaidi ya 40% ya Watumishi wa Umma Tanzania hawafanyi kazi

40 percent is just too much of a burden to shoulder. How did they hire the employees who have no value addition.

Results ya employment ya watoto wa mjomba, shangazi etc Kama wanajuwa ni mzigo, basi wawatoe!!

Kiongozi huwezi kutoa kauli kama hiyo hadharani halafu na solution huna. Ni bora ukae KIMYA

Naona waziri ndio mzigo kama tatizo umeliona unaanza kulalamika bila kutoa maamuzi. You are the biggest problem
Do you think even for a single day watamuondoa mtoto wa shangazi or mjomba?
 
Mtu anaingia saa tatu na nusu kazini,anazuga saa nne anaenda kupiga chai anakaa huko anarudi saa tano na nusu,anazuga saa sita na nusu ana kwenda lunch anarudi saa nane na nusu
Anazuga kazini saa tisa na nusu huyo kaondoka kwake
Ila yote anajuwa mshahara utaingiaaa....

Ova
 
Aisome Tlaatlaah , Lucas Mwashambwa , johnthebaptist , ChoiceVariable ,

Bila kusahau,
WAZALENDO WOTE WA HUMU NDANI JF.
Let me make this clear to everyone in this esteemed platform,

awamu ijayo ya uongozi wa serikali sikivu ya CCM chini ya kiongozi wetu mpendwa na kipenzi cha waTanzania wote Dr.Samia Suluhu Hassan & Dr Emanuel Nchimbi,

kuanzia kwenye baraza la mawaziri, taasisi, mashirika na mamlaka mbalimbali za umma hadi watendaji wa ngazi za vijiji na mitaa nchini,

hapatakua na kasumba ya kuhamishwa wizara, shirika, kijiji au mtaa, ukivurunda unapigwa chini na unakwenda nyumbani mazima,

hapatakua na mzaha wala kumuonea mtu aibu wala haya kwa uzembe au makosa yake kazini na kwa kuendekeza mazoe kwenye kazi za utendaji za kuwapelekea wananchi maendeleo.

there will be no excuse at all 🐒
 
Nijambo la kustaajabu kama karibu nusu ya watumishi wa umma hawafanyi kazi. Pamoja na uhaba wa nguvu kazi ulipo bado kuna nguvu kazi inakula mshahara wa serikali na hawafanyi kazi inavyo takiwa. Ikumbukwe kuwa tanzania ina watu walio katika nguvu kazi takribani milioni 25 kati ya watanzania milion 65. Hii inamaana kuwa watanzania milion 49 niwategemezi sasa hawa wacache waliopo bado kuna watu hawatumii nguvu zao vizuri kutumikia Taifa hili. 😪 maendeleo yatatoka wapi? Yani nguvu kazi ya milion 25, ukitoa hapo hawa wavivu , ukitoa hapo jobless na wale wadangaji sijui maendeleo tutatoa wapi

"
#HABARI Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema zaidi ya asilimia 40 ya Watumishi wa Umma hawafanyi kazi licha ya kulipwa mshahara kila mwezi.

Amesema hiyo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni na Tume ya Utumishi wa Umma nchini

Mhe. Simbachawene amesema hayo leo jijini Arusha wakati akifunga Kikao kazi cha tano cha Serikali Mtandao ambapo amesema Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma wanawajibu wa kuhakikisha kila mtumishi anatekeleza majukumu yake ipasavyo.

‘’Watumishi ni lazima wafanye kazi kwani wasipofanya kazi wanakuangusha wewe Mkuu wa Taasisi, lazima tuwe na jamii inayoandaliwa kufanya kazi’’ amesisitiza Mhe. Simbachawene

Amefafanua kuwa kwa mujibu wa tafiti hiyo, wavivu, wazembe, wagonjwa pamoja na waliosusiwa kutokana na vipaji na uwezo wao ni asilimia 40 ya Watumishi wanaolipwa pasipo kufanya kazi

Amewataka Wakuu hao kuwatumia Watumishi wa Umma wenye vipaji na uwezo badala ya kuwafanyia fitina na hujuma hali inayopelekea kurudisha nyuma maendeleo ya nchi

Amesema hali hiyo imesababisha kutokuwepo kwa urithishanaji wa madaraka jambo ambalo limechangia kudhoofika kwa Taasisi pale kiongozi wa Taasisi anapostaafu au kuhama. #EastAfricaTV
Ukweli ni kwamba 95% ya watumishi ni wavivu wakubwa!
 
Uimara wa hizo ngazi za juu hufanya hata za chini kuwa imari , ukiona hivyo jua ngazi za juu pia kuna shida.
 
Let me make this clear to everyone in this esteemed platform,

awamu ijayo ya uongozi wa serikali sikivu ya CCM chini ya kiongozi wetu mpendwa na kipenzi cha waTanzania wote Dr.Samia Suluhu Hassan & Dr Emanuel Nchimbi,

kuanzia kwenye baraza la mawaziri, taasisi, mashirika na mamlaka mbalimbali za umma hadi watendaji wa ngazi za vijiji na mitaa nchini,

hapatakua na kasumba ya kuhamishwa wizara, shirika, kijiji au mtaa, ukivurunda unapigwa chini na unakwenda nyumbani mazima,

hapatakua na mzaha wala kumuonea mtu aibu wala haya kwa uzembe au makosa yake kazini na kwa kuendekeza mazoe kwenye kazi za utendaji za kuwapelekea wananchi maendeleo.

there will be no excuse at all 🐒
Hayati MAGUFURI aliweza kurudisha nidhamu KAZINI MPAKA akaitwa majina ya OVYO Dicteta, roho mbaya...Kuna kipindi mpaka Kuna walio chelewa kazini vitu vyao vilichukuliwa na kupelekwa halmashauli ikabidi wavifuate huko😊

Kwa CCM hii ya mama simuoni huyo mwenye ubavu wa kuwa shurutisha Hawa wazembe wafanye kazi maana hata "MC GREGORY KWENYE THEORY X NA THEORY Y alipata kusema Kuna watu ni wavivu na hawataki kufanya kazi na pia kuna watu ni wachapakazi Sana.

Tuwafundishe watu wetu kua na moyo wa kupenda kazi hata Kama mazingira,malipo hakuna ni ku feel proud kufanya kazi kwa bidii hio ndio iwe spirit yetu..
 
40% takwimu haiko sahihi hata kdg, sema 80% kuna watu hawajui hata ofsn anaenda kufanya nini

hapo hatujazungumzia ambao hawaendi kabisa wanapotelea kwenye ulevi na kamari

nimewahi kuwa napanda daladala na watumishi halmashauri flani unashangaa anahairisha bila sababu na si mara moja wala mbili
 
Nijambo la kustaajabu kama karibu nusu ya watumishi wa umma hawafanyi kazi. Pamoja na uhaba wa nguvu kazi ulipo bado kuna nguvu kazi inakula mshahara wa serikali na hawafanyi kazi inavyo takiwa. Ikumbukwe kuwa tanzania ina watu walio katika nguvu kazi takribani milioni 25 kati ya watanzania milion 65. Hii inamaana kuwa watanzania milion 49 niwategemezi sasa hawa wacache waliopo bado kuna watu hawatumii nguvu zao vizuri kutumikia Taifa hili. 😪 maendeleo yatatoka wapi? Yani nguvu kazi ya milion 25, ukitoa hapo hawa wavivu , ukitoa hapo jobless na wale wadangaji sijui maendeleo tutatoa wapi

"
#HABARI Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema zaidi ya asilimia 40 ya Watumishi wa Umma hawafanyi kazi licha ya kulipwa mshahara kila mwezi.

Amesema hiyo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni na Tume ya Utumishi wa Umma nchini

Mhe. Simbachawene amesema hayo leo jijini Arusha wakati akifunga Kikao kazi cha tano cha Serikali Mtandao ambapo amesema Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma wanawajibu wa kuhakikisha kila mtumishi anatekeleza majukumu yake ipasavyo.

‘’Watumishi ni lazima wafanye kazi kwani wasipofanya kazi wanakuangusha wewe Mkuu wa Taasisi, lazima tuwe na jamii inayoandaliwa kufanya kazi’’ amesisitiza Mhe. Simbachawene

Amefafanua kuwa kwa mujibu wa tafiti hiyo, wavivu, wazembe, wagonjwa pamoja na waliosusiwa kutokana na vipaji na uwezo wao ni asilimia 40 ya Watumishi wanaolipwa pasipo kufanya kazi

Amewataka Wakuu hao kuwatumia Watumishi wa Umma wenye vipaji na uwezo badala ya kuwafanyia fitina na hujuma hali inayopelekea kurudisha nyuma maendeleo ya nchi

Amesema hali hiyo imesababisha kutokuwepo kwa urithishanaji wa madaraka jambo ambalo limechangia kudhoofika kwa Taasisi pale kiongozi wa Taasisi anapostaafu au kuhama. #EastAfricaTV
Sijasoma uzi wako lakini nakupinga vikali 60% ndio wavivu na 40% ndo wanajikakamua kufanya kazi zao tena ili mradi tu. kipindi cha jk ilikuwa kawaida kuwakuta waalimu wanacheza karata ama bao vijiweni muda wa kazi.Dr kumkuta anakunywa muda wa kazi
 
40 percent is just too much of a burden to shoulder. How did they hire the employees who have no value addition.

Results ya employment ya watoto wa mjomba, shangazi etc Kama wanajuwa ni mzigo, basi wawatoe!!

Kiongozi huwezi kutoa kauli kama hiyo hadharani halafu na solution huna. Ni bora ukae KIMYA

Naona waziri ndio mzigo kama tatizo umeliona unaanza kulalamika bila kutoa maamuzi. You are the biggest problem
yes maamuzi yake kama yeye ni yapi
 
Sijasoma uzi wako lakini nakupinga vikali 60% ndio wavivu na 40% ndo wanajikakamua kufanya kazi zao tena ili mradi tu. kipindi cha jk ilikuwa kawaida kuwakuta waalimu wanacheza karata ama bao vijiweni muda wa kazi.Dr kumkuta anakunywa muda wa kazi
Wengine sio wavivu hawajui au hawana uwezo kabisa wa kufanya kazi walizopewa tena wengine wanamatatizo ya akili kabisa lkn unakuta nea yumo eti mwalimu sijui dokta hawa watu wapo jamani
 
Back
Top Bottom