Simbachawene: Ripoti zinaonesha zaidi ya 40% ya Watumishi wa Umma Tanzania hawafanyi kazi

Ajinyonge hadi afe ili akawe baba wa malaika waovu kuzimu.
 
Serikali huwa haizai inaajiri

Mwajiriwa akiwa mzigo inatupilia mbali huko inatafuta wengine
 
Waliosusiwa yani wamesusiwa na nani ? Nilishawahi kisikia stori za mkurugenzi wa Shirika la Uma fulani aliyesusiwa akapelekwa Dodoma makao makuu kazi yake ikawa kusoma magazeti...hii sikuamini sasa naanza kuona kuna ukweli 😂😂
 
Kuna mwalimu mwenzetu mkongwe alinishangaza kwa kutoa kauli kwamba tumeletwa shuleni kuja kula hela ya serikali bure! Ndio kwanza tulikuwa tumepangiwa kituo hapo kwa mara ya kwanza tukitokea vyuoni. Alidai kwamba hakuna kazi ya kufanya, tukaa wiki nne tu mshahara unatoka na kwenda benki kuuchukua na kuula bure bila kufanya kazi. Alihoji kwani kuna kazi gani hiyo ya kulipwa mshahara? Alizidi kunishangaza kwa kuuita mshahara wetu ni hela ya chai ya asubuhi ya mbunge mmoja!
 
Yaani huyu Jamaa sijui Watumishi walishamfanya nini,hana tofauti na Mwendazake Kwa chuki na Watumishi.

Yeye anafanya kazi gani ya maana?
 
Hakuna Kazi inayofanyika nchi hii.
Naona hapo kuna bango kubwa la e-GA halafu watu wamekutana physically! yaani inaonesha jinsi gani hatufanyi kazi. One day travelling to, one day travelling back, many hours after meeting being idle in Arusha could be saved by video conferencing.
 
Nijambo la kustaajabu kama karibu nusu ya watumishi wa umma hawafanyi kazi. Pamoja na uhaba wa nguvu kazi ulipo bado kuna nguvu kazi inakula mshahara wa serikali na hawafanyi kazi inavyo takiwa. Ikumbukwe kuwa tanzania ina watu walio katika nguvu kazi takribani milioni 25 kati ya watanzania milion 65. Hii inamaana kuwa watanzania milion 49 niwategemezi sasa hawa wacache waliopo bado kuna watu hawatumii nguvu zao vizuri kutumikia Taifa hili. 😪 maendeleo yatatoka wapi? Yani nguvu kazi ya milion 25, ukitoa hapo hawa wavivu , ukitoa hapo jobless na wale wadangaji sijui maendeleo tutatoa wapi

"
#HABARI Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema zaidi ya asilimia 40 ya Watumishi wa Umma hawafanyi kazi licha ya kulipwa mshahara kila mwezi.

Amesema hiyo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni na Tume ya Utumishi wa Umma nchini

Mhe. Simbachawene amesema hayo leo jijini Arusha wakati akifunga Kikao kazi cha tano cha Serikali Mtandao ambapo amesema Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma wanawajibu wa kuhakikisha kila mtumishi anatekeleza majukumu yake ipasavyo.

‘’Watumishi ni lazima wafanye kazi kwani wasipofanya kazi wanakuangusha wewe Mkuu wa Taasisi, lazima tuwe na jamii inayoandaliwa kufanya kazi’’ amesisitiza Mhe. Simbachawene

Amefafanua kuwa kwa mujibu wa tafiti hiyo, wavivu, wazembe, wagonjwa pamoja na waliosusiwa kutokana na vipaji na uwezo wao ni asilimia 40 ya Watumishi wanaolipwa pasipo kufanya kazi

Amewataka Wakuu hao kuwatumia Watumishi wa Umma wenye vipaji na uwezo badala ya kuwafanyia fitina na hujuma hali inayopelekea kurudisha nyuma maendeleo ya nchi

Amesema hali hiyo imesababisha kutokuwepo kwa urithishanaji wa madaraka jambo ambalo limechangia kudhoofika kwa Taasisi pale kiongozi wa Taasisi anapostaafu au kuhama. #EastAfricaTV
 
40 percent is just too much of a burden to shoulder. How did they hire the employees who have no value addition.

Results ya employment ya watoto wa mjomba, shangazi etc Kama wanajuwa ni mzigo, basi wawatoe!!

Kiongozi huwezi kutoa kauli kama hiyo hadharani halafu na solution huna. Ni bora ukae KIMYA

Naona waziri ndio mzigo kama tatizo umeliona unaanza kulalamika bila kutoa maamuzi. You are the biggest problem
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…