DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Jumatatu, Desemba 8, 2025, wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari, Simbachawene amesema aina ya ukamataji unaofanywa na baadhi ya askari ikiwemo kuvaa kininja, kutovaa sare rasmi za polisi na kwenda kuwakamata watuhumiwa majumbani usiku haukubaliki na unapaswa kusitishwa.“Ukamataji ninaoupenda mimi ni ule wa kisheria. Askari anaenda, anaripoti kwa mjumbe, mtu anajulikana yupo kazini kwake. Ya nini uende kumkamata nyumbani kwake umevaa kininja? Tumekubaliana kwamba kuwe na ukamataji wenye staha,” amesema.
Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi linapaswa kuzingatia uwiano kati ya ukubwa wa kosa na hatua zinazochukuliwa ili kuepusha matukio yanayoweza kuwatia hofu wananchi.
“Masuala ya kiusalama ni mengi. Mambo kama haya lazima yaendane na tukio lenyewe. Si kosa dogo tu, mtu kaposti kitu mtandaoni halafu anakamatwa usiku na askari wenye silaha nzito. Tumekubaliana haya hayawezi kuendelea,” amesema na kuongeza kuwa baadhi ya mbinu hizo zimekuwa zikichochea chuki za wananchi dhidi ya polisi na kuathiri taswira ya jeshi hilo.