PostGE2025 Simbachawene: Ya nini uende kumkamata mtu nyumbani kwake umevaa kininja? marufuku polisi wasiovaa sare kukamata watu

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Ibilisi akikuambia Leo ni jumatatu hatakama ni kweli usikubaliane nae.
 
Huyo anapiga kelele tu. Yeye katoa katazo hilo kwa polisi. Kesho polisi wataamriwa na abduli au ofisi kubwa wateke mtu unadhani watamsikiliza simbachawene?
 
Gz huo moto mnaopelekq yanaa za kupoteana ..yashaanza kutengana kwa kauli zao
 
Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura, kuhakikisha ukamataji wa Watu unafuata taratibu za kisheria na amepiga marufuku Polisi kuwakamata Watu kibabe wakiwa wamevaa kininja, wakiwa bila sare na silaha kubwa.
G7pPyoAXwAAbsem.jpg
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema amemwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi, Camillus Wambura, kuhakikisha kuwa ukamataji wa watuhumiwa unafanyika kwa kufuata misingi ya sheria na kwa kuzingatia staha.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Jumatatu, Desemba 8, 2025, wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari, Simbachawene amesema aina ya ukamataji unaofanywa na baadhi ya askari ikiwemo kuvaa kininja, kutovaa sare rasmi za polisi na kwenda kuwakamata watuhumiwa majumbani usiku haukubaliki na unapaswa kusitishwa.

“Ukamataji ninaoupenda mimi ni ule wa kisheria. Askari anaenda, anaripoti kwa mjumbe, mtu anajulikana yupo kazini kwake. Ya nini uende kumkamata nyumbani kwake umevaa kininja? Tumekubaliana kwamba kuwe na ukamataji wenye staha,” amesema.

Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi linapaswa kuzingatia uwiano kati ya ukubwa wa kosa na hatua zinazochukuliwa ili kuepusha matukio yanayoweza kuwatia hofu wananchi.

“Masuala ya kiusalama ni mengi. Mambo kama haya lazima yaendane na tukio lenyewe. Si kosa dogo tu, mtu kaposti kitu mtandaoni halafu anakamatwa usiku na askari wenye silaha nzito. Tumekubaliana haya hayawezi kuendelea,” amesema na kuongeza kuwa baadhi ya mbinu hizo zimekuwa zikichochea chuki za wananchi dhidi ya polisi na kuathiri taswira ya jeshi hilo.

Chanzo: Mwananchi
Unprofessionalism imetamalaki TANPOL. Mchana kweupe, polisi (wakiwa na sare zao) watakamata mtu, watampoteza na kisha TANPOL itasema kwamba waliomkamata hawakuwa polisi. TANPOL ni genge la majambazi, bila kujali wamevaaje!
 
Tena waambatane na Polisi Kata wa kata husika na uongozi wa serikali ya mtaa uwe na taarifa ya hilo zoezi labda kama wanakamata majambazi au magaidi
 
Wakuu tusirudi nyumba,ukiona wanaanza kunena kwa lugha jua kunakaribia kupambazuka,walikuwa na nafasi ya kuyasema haya mapema ,kwanini wasubiri damu za watoto wetu zimwagike ndo waje na ngonjera hizi
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema amemwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi, Camillus Wambura, kuhakikisha kuwa ukamataji wa watuhumiwa unafanyika kwa kufuata misingi ya sheria na kwa kuzingatia staha.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Jumatatu, Desemba 8, 2025, wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari, Simbachawene amesema aina ya ukamataji unaofanywa na baadhi ya askari ikiwemo kuvaa kininja, kutovaa sare rasmi za polisi na kwenda kuwakamata watuhumiwa majumbani usiku haukubaliki na unapaswa kusitishwa.

“Ukamataji ninaoupenda mimi ni ule wa kisheria. Askari anaenda, anaripoti kwa mjumbe, mtu anajulikana yupo kazini kwake. Ya nini uende kumkamata nyumbani kwake umevaa kininja? Tumekubaliana kwamba kuwe na ukamataji wenye staha,” amesema.

Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi linapaswa kuzingatia uwiano kati ya ukubwa wa kosa na hatua zinazochukuliwa ili kuepusha matukio yanayoweza kuwatia hofu wananchi.

“Masuala ya kiusalama ni mengi. Mambo kama haya lazima yaendane na tukio lenyewe. Si kosa dogo tu, mtu kaposti kitu mtandaoni halafu anakamatwa usiku na askari wenye silaha nzito. Tumekubaliana haya hayawezi kuendelea,” amesema na kuongeza kuwa baadhi ya mbinu hizo zimekuwa zikichochea chuki za wananchi dhidi ya polisi na kuathiri taswira ya jeshi hilo.

Chanzo: Mwananchi
Sasa serikali imeanza kuelewa mambo ya msingi.
Na waliotenda hayo uko nyuma wafanywe nini?
 
Bashungwa mwanaharamu kabisa, ameiongoza hii wizara kama genge Fulani la vibaka
 
Nawajua sana Tatizo
Kwahiyo polisi hawajui wajibu wao... Nchi hii imejaa wahalifu wakikatiba
Mifumo imeingiliana hii tabia aliyoisema Simbachawene ya Askari kuvaa kininja inatumika kule Zanzibar kukamata Watuhumiwa wowote wale na kule Zanzibar polisi hawana nguvu kuna vikosi vya SMZ ndiyo vina nguvu, Sasa Mfumo wa Zanzibar umeingizwa Tanganyika, Askari wanaojifunika using ni Vikosi kutoka Zanzibar, ndiyo Maana Simbachawene kasema ukamataji huo ni mgeni hapa nchini na yeye hajui hizi tabia ni Za Zanzibar.
 
Back
Top Bottom