Mkuu hatujawasikiliza wahusika huyo kijana wa kiume na binti. Mi sidhani kama hakimu ni mpuuzi kutoa adhabu hiyo ambayo nadhani wewe unaona haifai kwa hilo kosa naamini kuna mazingira fulani hakimu aliyashtukia kwenye maelezo ya hao madogo.
Nakwambia hivi kwasababu mimi kwenye utoto wangu around miaka 16 kuna mama mmoja alinikuta kwake na binti yake nae umri huo huo alivyokuja kusema kwa wazazi wangu alimpanga mwanae aseme nilimlazimisha huku tulikubaliana ( halafu nilikuwa mrefu kabinti kadogo dogo unaweza kuamini yaani) sijui walimalizana vipi na wazazi wangu baadae ila nahisi alitaka kuomba hela.
Sent from my M10_Max using
JamiiForums mobile app
Sawa.
Lakini hapa tunaijadili hukumu na sababu alizotoa huyo hakimu kwanini katoa hiyo hukumu.
Na Kama hakimu amewashtukia Kama unavyosema, sheria inamtaka kubainisha wazi ni kipi amebaini kwa mtuhumiwa na muhanga mpaka kutoa hukumu hiyo.
Kama amegundua walipatana ilipaswa kuwa bayana kwenye hukumu na sio sentensi moja tu kwanini kaagiza faini ya shilingi laki 3.
Hapa dhana ya kwamba binti alikubali na hiyo faini ni malipo ya hilo tendo inaishi?
Maana Kama kabakwa kweli hiyo laki 3 inamsaidia vipi katika kujitibu kimwili na kisaikolojia?
Kumbuka sheria ipo kwa ajili ya kurekebisha na kutoa muongozo + onyo kwa waliopo pembeni kutokutenda kosa Kama hilo.
Tukio lako haliwezi kuwa ndio kipimo cha matukio yote.
Kama ambavyo wewe ulinusulika kusingiziwa wapo wanaotendewa jinai na kusingiziwa kwamba walitaka wenyewe.
Mfano rahisi ni humu kwenye hii topic, michango mingi inahalalisha kitendo kilichotokea na ku support hukumu.
Mabinti wengi sana wanapitia unyanyasaji wa kingono na kuharibiwa psychology ya mapenzi, ngono na mahusiano.
Wengi kwa kuogopa stigma Kama hii humu ndani hukaa kimya na kuyaishi manyanyaso hayo siku zote za maisha yao.
Sasa wengi huziba shimo la maumivu hayo kwa kuwa malaya (anajiona hana thamani tena) na wengine kuwa wakorofi kwenye mahusiano yao ya ndoa na jamii kwa kuishi na hasira za kutendwa na kunyanyaswa.
Mwili wa mtu ni mali ya mtu mpaka pale Katiba ya nchi inapoguswa.
Halafu Kama kuna mazingira ya mapatano kati yao ama kujuana, kwanini mbakwaji kajeruhiwa mwili?
Waandishi pia wanaoleta Habari wawe wanatupa na background ya tukio na picha halisi ya mazingira wakati wa tukio.