Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Watu wengine hata tukiona wanyama wanateswa tunaumia ndio sembuse mwanao?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
We akili ndiyo umeshaazima, askari kufanya kazi Simiyu ndio awe msukuma. Akili umeazima?Wasukuma ukatili umezidi. Tofautisheni ng'ombe na watoto wenu jamani!
unaandika kama unakimbizwa rudi kalete habari kamiliHerbert Gappa (7), Mtoto anayesoma Darasa la Kwanza Shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza iliyopo Mji wa Bariadi mkoani Simiyu, amelazwa hospitalini baada ya kudaiwa kupigwa na kujeruhiwa vibaya sehemu zake za mwili na baba yake mzazi, ambaye ni askari Polisi, Abati Benedicto Nkalango.
Mtoto huyu anayetibiwa katika Hospitali ya Somanda Mjini Bariadi, amekatishwa masomo yake darasani baada ya baba yake kumtendea unyama huu, kinyume cha sheria za nchi na haki za binadamu.
Akizungumzia ukatili huu aliotendewa mtoto huyu wa kiume, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Somanda, Dk. Costantine Emmanuel, amesema madaktari na wauguzi wanaongeza jitihada za kunusuru uhai wa mtoto huyu, nguvu kazi ya Taifa.
Akizungumzia ukatili huu, Mwalimu Benadetha Katendege, anaposoma mtoto huyu, amesema wamegundua shambulio hilo la kudhuru mwili baada ya mtoto huyo kuonekana kukosa morari ya masomo darasani.
Kufuatia hali hiyo, Askari Polisi huyo anayetuhumiwa kutenda ukatili huo kwa mwanaye wa kumzaa, tayari yupo mikononi mwa Polisi, ambapo umma unasubiri kuona hatua gani zitachukuliwa dhidi yake.
Tanzania imesaini mkataba wa kimataifa wa kulinda haki za binadamu, hivyo ni muhimu ukatili huu ukadhibitiwa ili kujenga jamii inayoheshimiana.
Chanzo: EATV