Simiyu: Baada ya kulalamika Dampo la Kidinda kwenye makazi ya watu, tangazo latolewa, kifaa cha kuhifadhi taka chawekwa

Simiyu: Baada ya kulalamika Dampo la Kidinda kwenye makazi ya watu, tangazo latolewa, kifaa cha kuhifadhi taka chawekwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
photo_2023-07-06_11-32-54.jpg

Siku chache baada ya Mdau wa JamiiForums.com kutoka Simiyu kudai kuwa Wananchi wa Mtaa wa Majengo, Halmashauri ya Bariadi wako katika wakati mgumu kutokana na harufu kali na chafu inayotoka kwenye jalala ambalo pia limetawaliwa na moshi mwingi kutokanana uchomaji taka unaofanyika kila siku, hatua zimeanza kuchukuliwa.

Awali, Mwenyekiti wa Mtaa, Maduhu Nyanda na Diwani wa Kata, Kija Bulenya alidai wamepeleka malalamiko katika Ofisi ya Mkurugenzi lakini hawakusikilizwa.

Ndipo Mkuu wa Kitengo cha Usafi na Udhibiti Taka Halmashauri ya Mji, Peter Subadi akasema “Lilikuwa dampo dogo, ongezeko la watu limefanya uchafu umekuwa mwingi, tunalifunga wiki hii.”

Sehemu ya hatua iliyochukuliwa ni kuweka tangazo linalopiga marufuku kutupa taka lakini kimewekwa kifaa cha kuwekea uchafu eneo hilohilo.

Tangazo hilo linaelekeza kuwa uchafu upelekwe Dampo rasmi lilipo Kilometa 9 kutoka mjini panaitwa Kidulya.

Wakati huohuo, wenye matoroli wanaendelea kupeleka taka eneo hilo ila wanaweka kwenye hicho kifaa.
photo_2023-07-06_11-32-59.jpg

photo_2023-07-06_11-33-02.jpg

photo_2023-07-06_11-32-53.jpg


Mkuu wa Kitengo cha Usafi na Udhibiti Taka Halmashauri ya Mji, Peter Subadi
Anafafanua: Uongozi umepiga marufuku eneo hilo kutumika kama Dampo lakini tumeweka kontena la kubebea taka ambalo litatumika kuhifadhi taka kwa wale wanaozoa mitaani.

Tumewawekea hilo kontena wakati tukitafuta mzabuni wa kuzoa taka kwa kuwa kubeba taka na kupeleka Kidulya (kwenye Dampo Kuu) ambapo kuna umbari mrefu kutoka hapo eneo la tukio.

Pia Soma:
~
Halmashauri ya Bariadi yaanzisha Dampo katikati ya makazi ya Wananchi
~ Dampo la Kidinda Bariadi linaanza kurudi, baadhi ya watu wanatupa taka usiku. Hatua zichukuliwe haraka
 
Back
Top Bottom