Pre GE2025 Simiyu: CHADEMA yapata pigo Wanachama 60 wahamia CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Itilima, Katibu na wanachama wao wahamia CCM.

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, Ndugu Terry Kilugala, na Katibu wake wa Wilaya ya Itilima, Ndugu Gershom Migasa Mipawa, pamoja na wanachama wao zaidi ya 60, wamehamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupokelewa na Katibu Mkuu wake, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Luguru, wilayani Itilima.

Ndugu Kilugala, akizungumza kwenye mkutano huo, amesema mbali na Chadema kuwatumia vibaya viongozi na wanachama wake, kisha kuwaacha ‘watupu’ wakiangaliana wenyewe kwa wenyewe, uongozi wa CCM na utendaji kazi wa serikali yake, chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, vyote vimemfanya arudi nyumbani.

“Tulikuwa tunaenda Mwanza siku mbili kwa ubovu wa barabara, leo tunaenda na kurudi. Lazima tuseme ukweli, CCM imefanya kazi, lakini wenzetu wamebakia kusema uongo na kututumia vibaya. Kuna wabunge wa COVID-19, lakini ndani yake wamo wake zao, alafu huku wanatudanganya.”

Balozi Nchimbi, akiwapokea, amesema:

“Hawa ndugu zetu wameona mbali mapema, maana viongozi wakubwa kama Peter Msigwa kaona shida zao, wewe unasubiri nini? Rudini CCM, na nawapongeza wote mliojiunga na CCM, viongozi pamoja na wanachama. Karibuni sana tufanye kazi ya kujenga taifa pamoja.”

IMG-20241008-WA0125.jpg
IMG-20241008-WA0128.jpg
IMG-20241008-WA0127.jpg
IMG-20241008-WA0126.jpg
 
CHADEMA imebaki jina tu au mkusanyiko wa wasaka Tonge na wachumia tumbo wachache wasio na Dira wala muelekeo zaidi ya maslahi ya matumbo yao kuponya na kuganga njaa tu.
Ccm imebaki na wajinga na wapumbavu wanaojifariji jf wakati mitaan kila Kona mmechapika, Kwa taarifa yako Leo huyo katibu wenu huko maswa uliza alikuwa na genge gani.
 
CHADEMA ndio imekufa kabisa katika mioyo ya mamilioni ya watanzania.ndio maana unaona hata maandamano yalifeli kabisa mpaka kufikia hatua ya kukosekana kabisa watu wa kuandamana zaidi ya Mbogwe ,mke wake na mwanae ambao wana maslahi yao ndani ya CHADEMA
 
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, Ndugu Terry Kilugala, na Katibu wake wa Wilaya ya Itilima, Ndugu Gershom Migasa Mipawa, pamoja na wanachama wao zaidi ya 60, wamehamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupokelewa na Katibu Mkuu wake, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Luguru, wilayani Itilima.

Yaani kumbe watu wakihama basi ofisi nazo zinafungwa?! Waambie moderators wabadilishe kichwa cha habari. Habari zisizo na kichwa wala miguu, yaani Terry Kilugala na wenzake wamekwenda CCM ndo ofisi za CHADEMA zifungwe!?? Upo serious kweli!??

Hata kama ni mapambio na kutafuta teuzi kwenye mikeka ya Samia, hii imezidi! Kuna wakati mnaonekana The Walkers kwenye tamthilia ya The Walking Dead 😃

Kama hayati Magufuli na ubabe wote ule bado ofisi za CHADEMA hazikufungwa sembuse huyu Emmanuel Nchimbi! We una masihara! Acha kufanya mapambio ya ajabu namna hii! Ofisi za CHADEMA haziwezi kufungwa sio na Nchimbi wala Samia! Kuleni chuma hicho!
 
CCM wameshaanza kununua wanasiasa na wanachama

kwa nini wanunue wanasiasa wa upinzani na sio kuwatengeneza ndani ya chama chao
Ukiuliza hivyo unakosea. Hiyo ndio inayoitwa "Si Hasa" Sumaye, Lowassa, Kingunge, Lipumba, Mapesa, Lyatonga n.k. walitengenezwa na CCM lakini wakahamia upinzani
 
Kwa tuhuma hizi za utekaji na mauaji ni ngumu kuamini kuwa kuna wanaowahusudu wenye tuhuma hizo.
 
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, Ndugu Terry Kilugala, na Katibu wake wa Wilaya ya Itilima, Ndugu Gershom Migasa Mipawa, pamoja na wanachama wao zaidi ya 60, wamehamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupokelewa na Katibu Mkuu wake, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Luguru, wilayani Itilima.

Yaani kumbe watu wakihama basi ofisi nazo zinafungwa?! Waambie moderators wabadilishe kichwa cha habari. Habari zisizo na kichwa wala miguu, yaani Terry Kilugala na wenzake wamekwenda CCM ndo ofisi za CHADEMA zifungwe!?? Upo serious kweli!??

Hata kama ni mapambio na kutafuta teuzi kwenye mikeka ya Samia, hii imezidi! Kuna wakati mnaonekana The Walkers kwenye tamthilia ya The Walking Dead 😃

Kama hayati Magufuli na ubabe wote ule bado ofisi za CHADEMA hazikufungwa sembuse huyu Emmanuel Nchimbi! We una masihara! Acha kufanya mapambio ya ajabu namna hii! Ofisi za CHADEMA haziwezi kufungwa sio na Nchimbi wala Samia! Kuleni chuma hicho!
Sasa ofisi zitaendelea vipi bila wanachama na hata viongozi?
 
Back
Top Bottom