Mimi sio mwanasiasa wala mwanachama wa chama chochote cha kisiasa, na wala sio social scientist bali nipo kwenye natural sciences. Kwa mujibu wa research nazofanya mojawapo ni qualitative ambayo haihitaji empirical data, tunapata conclusions kwa human perceptions, feelings, thoughts, says, mitazamo, mazungumzo, reactions, nk nk.
Kwa ujumla utafiti wangu usio rasmi qualitatively, naona Chadema ni lidude moja kubwa mno na linalotisha sana kwa kutazama namna reactions, na qualitative data zilizopo humu JF, radioni, social media zingine, TV, blogs, Polisi, jeshini, mitaani, magengeni, chats, groups za chawas etc. hamna siku chadema haijatajwa mara 10 hadi 20! Kuanzia mama yao/yetu akilala, akiamka, akiongea, akiwaza, chadema inazunguka kichwani kwake, makondeko kule kwa landrover kila akiamka, makalai kwenye mizunguko yake ya perdiem, joni nchambi, mcheza kiduku wa daslam, hapi, mkumbwa, cc yote ya ccm, machawa wazoefu na wapya kote mitandaoni, mwashamba, talalalah, choicevariable, yohana mbatizaji, na wengine lukuki. Polisi ndio wakisikia kuanzia kaka yao mkubwa anayevaa official dress na buti hata kwenye sherehe ikulu kama yupo vitani ndio wanapagawa kabisa na kuitana nchi nzima, na kuwasha mazimamoto yao ya kipigaji. Hili dude linawatisha sana kisaikolijia.
My conclusion kwa haya naona chadema sasa niifananishe na maji kwa kweli, yani ni lazima uyatumie tu ili uishi, kuna watu kwa kuitajataja tu wamepata uwaziri, ukuu wa wilaya, ukuu wa mikoa, ubunge, uchawa rasmi, ukatibu-kata na uenezi wa ccm, wengine wakapigwa na pesa, wengine ubalozi, wengine ucovid-19 sasa hii si sawa na maji tu wandugu??
Yani utake usitake utayanywa, usipoyanywa utayaoga, usipoyaoga utafulia, usipoyafulia utapikia, usipopikia utaoshea hata tongotongo. Ili tumbo lako lisitirike kwa sasa we andika, taja, waza, ongea kuhusu chadema, ukiongelea mwengine unafutika tu kama upepo. Relavance yako itakuja kwa kusema chademaaaaa, chademaaaa hata kama huna logic km mwashamba.
Yani kuna watu wasipotaja chadema wanapotea so ili wawe relevant lazima kila siku waje na uzi kuhusu chadema tu, gosh!! Wengine hata spelling hawajui lkn chadema ipo midomoni mwao kutwa kucha.
No offence hii ni perception ya jamii ya watanzania kuanzia mama yetu shuka chini hadi kwa machawa wa level za chini kbs kama hapa nilipo cholesamvula. 😀😎😕