Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Taarifa ya Jeshi la Polisi imesema Januari 24, 2025, saa kumi na mbili jioni katika Kijiji cha Kilulu Kata ya Bunamala Tarafa ya Ntuzu wilayani Bariadi, Jeshi la Polisi kupitia kikosi kazi cha kupambana na uhalifu, kilifanikiwa kumkamata Emmanuel John Maduhu (31), Msukuma na mganga wa kienyeji akiwa na mnyama huyo akiwa hai.
“Mganga huyo alieleza kuwa anamtumia fisi huyo katika shughuli za uganga wa jadi ikiwa ni pamoja na kumtumia kama chombo cha usafiri anapotaka kupaa angani,” imeeleza.
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Mamlaka za Wanyamapori imesema wanaendelea na uchunguzi na mara baada ya upelelezi kukamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
Rai yangu:
1. Naomba Jeshi la Polisi lifanye msako mkali sana kutafuta wanaofuga fisi maeneo hayo, ni wazo zuri sana kuona polisi wakifanya doria nyakati za usiku haswa kuanzia saa 5 usiku mpaka majira ya saa 10 ili kupata wavunja sheria kama huyu mganga. Mikoa ya Simiyu, Shinyanga pamoja na baadhi ya viunga vya Tabora kumekuwa na tatizo hili.
2. Mambo ya kufuga fisi pamoja na kutumia fisi kama usafiri yamekuwa yakisemwa sio leo wala jana, ni mambo ambayo toka zamani watu wamesema, sio wapita njia wa Maganzo wala Tinde, wengi wamesimulia matukio ya kukutana na fisi akiwa anaendeshwa na mtu tena kwa mwendokasi wa kasongo. Badala ya kumkamata toeni elimu kwa watu watumie sayansi zao vyema. Leo mmemkamata huyu kwa kufuga fisi, je mkienda Ukara mtakamata wangapi kwa umiliki na ufugaji wa Mamba? Mganga hana kosa muacheni, Emmanuel hana kosa lolote.
3. Kuna matukio mengi yanahitaji utatuzi wa jeshi la polisi sio kwenda kumkamata mganga na kumfungulia mashtaka ambayo mnajua kabsa wengi wanafanya. Wekeni kambi usiku sehemu tajwa mkaone fisi zinavyotembea mwendokasi wa engine V16. Mwanamalundi angekuwa hai basi naye angekuwa matatani kwa mujibu wa Polisi na Mamlaka za Wanyamapori.