Simiyu: Wakamatwa kwa kumteka mtoto kisha kumuua baada ya kukosa hela

Simiyu: Wakamatwa kwa kumteka mtoto kisha kumuua baada ya kukosa hela

Frank Wanjiru

Platinum Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
25,686
Reaction score
46,842
Watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu kwa mahojiano kuhusiana na tuhuma za kumteka mtoto mdogo mwenye umri wa Miaka Mitano na kudai fedha kiasi cha shilingi Milioni tano kutoka kwa Baba mzazi wa mtoto huyo kabla ya kumuua mtoto huyo baada ya kuzikosa fedha hizo.

Kwa mujibu wa taarifa ya leo Agosti 19, 2026 iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, tukio hilo lilitokea mnamo Agosti 6 2026 katika Kijiji cha Gulung'washi Kata ya Malampaka Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu ambapo mtoto huyo aitwaye Samike Mponeja Maleche alitekwa akiwa anachunga mifugo na watu hao waitwao Yumba Mayala Miaka 22, Zakayo Shija (28) na Seba Buchenja (30) wote wakazi Malampaka ambao hapo awali hawakuweza kutambuliwa.

Jeshi la Polisi Mkoa Simiyu lilianza uchunguzi pamoja na kufanya msako maeneo mbalimbali na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao watatu na baada ya mahaojiano na kukusanya ushahidi mbalimbali watuhumiwa hao walieleza kwamba walimteka mtoto huyo ili waweze kujipatia fedha kiasi cha shilingi milioni tano kutoka kwa baba yake mzazi.

Walipofanya mawasiliano na Baba mzazi wa mtoto huyo na kushindwa kuwatia kiasi hicho cha fedha waliamua kumnyonga mtoto huyo na kutundika mwili wake juu ya mti ili kupoteza ushahidi. Watuhumiwa hao waliwaongoza Askari Polisi hadi walipo tundika mwili wa mtoto huyo na sasa uchunguzi unakamilishwa ili hatua nyingine ili ziweze kufuatwa.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limetoa wito kwa baadhi ya wananchi wanaoendekeza tabia ya kujaribu kujipatia kipato kwa njia zisizo halali kuicha kwani njia hiyo hailipi na madhara yake ni makubwa kwa watu wengine na kwao pia.
 
Back
Top Bottom